Hivi Waganda wana matatizo gani na Kiswahili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Waganda wana matatizo gani na Kiswahili

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Omugasi, Jun 23, 2009.

 1. O

  Omugasi Member

  #1
  Jun 23, 2009
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani hawa wenzetu wanaboa kishenzi! mimi wakati mwingine nashindwa kuwaelewa lengo lao..Ebu fikiria eti wanajifanya hawajui kuongea kiswahili? nani kasema ? Wanyarwanda, wakongo wengi wao ni wazuri wa kuongea hii lugha.Kichekesho huwa nakiona kwa hawa wenzangu tunapokuwa mazingira yanayotukutanisha na wakenya, eti wenyewe hawakijui, na hata mtu akitamka ni kama yule mzungu anaye jifunza kiswahili.
  Siyo kama nawataka sana waongee kiswahili lakini nawaonea huruma kwani wanajishahua lakini hawana lugha ya taifa.. ukimuuliza anakwambia kiingereza, na uingereza wasemeje?
   
 2. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Ni kweli ndugu wengi hawajui kiswahili... ni ajali ya kihistoria ikiwa ni pamoja na madhara ya vita Tz waliyopigana kumg'oa Iddi Amin Uganda.Askari wetu walikuwa wanaongea kiswahili lakini pia majambazi na wahalifu wakawa wanaitumia lugha hiyo katika matukio.Hii ikajenga chuki dhidi ya kiswahili ambapo kilionekana ni lugha ya majambazi!
   
 3. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kweli wanaboa. Pia kingereza chenyewe na accent yao tofauti. Kuna binti alisoma mlimani 4 yrs law, siku nikamtumia email ya kiswahili, eti akajibu nimempa wakati mgumu. Ila si wote
   
 4. G

  Gashle Senior Member

  #4
  Jun 24, 2009
  Joined: Mar 30, 2007
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Inabidi wabadilike kwa kweli. Pamoja na kuelewa kwamba kuna historia inayohusisha kiswahili na mambo yasiyo mema kwao, wanapaswa kuwa na mtazamo chanya. Kwangu mimi nalichukulia kwa jinsi hii; kujifunza lugha nyingi kwa kadri ya uwezo wako ni kwa manufaa yako katika ulimwengu huu wa utandawazi. Wenzao wa Kenya wanajitahidi kuibia ibia Kiswahili na kujichanganya Tanzania, kwa Waganda wanakuwa na wakati mgumu, maana hata Watanzania wenyewe wanakuwa na kama kuwashangaa, wakiwaona kama watu wenye dharau.

  Si lazima waishi kwenye historia, wanapaswa wabadilike waende na wakati. Kwa hivi sasa wanahitaji Kiswahili pia ili kuwafanya wajichanganye vema Afrika ya Mashariki. Sisi huwa tunakutana na wengine, tumeshawaimbia haya mashairi wee, tukaachoka. Tukasema, dawa yao hawa ni kuwa tukiwa kwenye social events, Kiswahili kwa kwenda mbele, mwanzo wakawa wanalalamika, lakini wanaenda wanajifunza taratibu maana wanajiona wako wameachwa.

  Shime Waganda, jifunzeni Kiswahili.
   
 5. Mtabiri

  Mtabiri Senior Member

  #5
  Jun 24, 2009
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 152
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nami nakubaliana na factor ya kihistoria kwamba ile vita jamaa imewakwaza sana. Mpaka sasa ktk mafunzo yao ya uaskari wanatumia kiswahili,wahuni wote wanatumia kiswahili,wezi,matapeli(au wayaye kama wanavyoitwa pale Kampala) wote wanatumia kiswahili. Hivyo mtu akitumia kiswahili anajengewa dhana kwamba either ni kibaka,au askari au tapeli fulani wa mujini.
  Tuwape pole ktk hilo ndugu zetu hawa. Sio kosa lao maana hata presidaa wao ingawa alisoma huku TZ kiswahili chake ukikisikia mh!!!
  Na kiingereza wanachojitapa nacho matamshi yao kama vile wanaongea vernacular "goingi,whati,comingi backi,oldi paki,city skweya",unawaelewa kwa hisia vinginevyo unatoka kapa!
   
 6. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Halazimishwi mtu kupenda Kiswahili. Wakenya walikuwa hivyo hivyo. Na hata baadhi yetu wanaona sifa kujifanya kiswahili kimewapiga chenga. Waganda kutothamini kiswahili ni uamuzi wao. Na ni hasara yao. Tusipoteze muda kuwabembeleza. Sababu zao si za msingi. Mbona waliotuuza kama bidhaa, kubaka ndugu zetu, kuwahasi babu zetu na kutufananisha na nyani n.k, lugha zao bado tunazienzi? Pamoja na hao waganda. Wanadhani wakiongea kiingereza cha kembrij au kiarabu cha Saudi ndiyo watakubalika? Walie tu.

  Amandla........
   
 7. D

  Dina JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2009
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Wala usiwachukie sana ndugu, ni kweli Waganda wengi hawazungumzi Kiswahili. Kiswahili cha Wakenya ni kizuri mara mia ya kile cha Waganda. Wala usikwazike, labda tu uwashauri nao wakipe kipaumbele.
   
 8. M

  Mchagaa Member

  #8
  Jun 24, 2009
  Joined: Jul 31, 2007
  Messages: 20
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Na kweli umesema. Hawa Waganda mambo yao sielewi kabisa. Watajifanya hawajui Kiswahili lakini kadri mnavyo endelea na mazungumzo, unasikia atoa contribution. Swala langu ni hili, kama huelewi lugha mbona unachangia katika mazungumzo? Huo sio utapeli kweli au ndio sophistication.
   
 9. J

  Jafar JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2009
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Usiwalaumu sana Waganda, actually tunatakiwa tuwasaidie kukijua kiswahili. Waganda kutopenda kiswahili kinatokana na historia ya nchi yao. Enzi zile za Idd Amin Dada (RIP), kiswahili kilikuwa kinatumika sana na watu wake wa karibu, hasa hasa Jeshi. Kwa kuwa wanajeshi walikuwa wanyanyasaji, wabakaji na sifa zote mbaya walikuwa nazo, hivyo basi huko mtaani ukiongea kiswahili ulikuwa unatengwa, maana inawezekana 100% wewe ni wa Amin na unahatarisha maisha ya watu. Idd Amin mwenyewe alikijua kiswahili.

  Historically, mpaka leo waganda wana kasumba hiyo.
   
 10. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mkuu, hapa umenena! Waganda si tu kwamba wengi wao hawakijui kiswahili, lakini pia hawakipendi. Unajua kwa nini? kwa sababu waganda kwa tabia yao ni watu wa kujisikia bora sana, na wanaona vyao tu ndiyo bora na vizuri. Nakumbuka nilikuwa na rafiki yangu mmoja hap Tz mganda daima alikuwa anasifia vya kwao tu: mara konyagi yao ni bora kuliko ya TZ, bia ya kwao umegemwa vizuri zaidi, kahawa ya kwao juu, wasichana wa kwao bomba, nk, nk. Ajabu na kweli!

  Kumbe wana aina ya majivuno na madharau kwa watu wengine. wao kujifunza na kuongea kiswahili wanaona ni kujidhalilisha, kujishusha, kutoonekana wa maana.
   
 11. S

  Shangazi JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Naungana na wewe coz nilishawahi kumuuliza mganda mmoja akaniambia ukiongea kiswahili ni kama jambazi au muuwaji wakikumbushia walivyofanyiwa na askari wa TZ wakati wa iddi amini.

  Ila pia si mnajua hawa jamaa lugha na tabia wanafanana na wale jamaa zetu wa BK infwact, kina ngambire stupid?
   
 12. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #12
  Jun 24, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ata namimi wananikera sana hawa jamaa,kwanza lugha yao yenyewe mbaya.
  Tatizo la Uganda i am told kiswahili wanaona kama lugha ya Jeshi so ukiwa fluent wanajua wewe mjeda.Kiswahili pia kilitumika wakati wa vita ya Uganda so wanachukulia pia kama watakuwa wanajiundermine si unajua tuliwadunda!I think hiyo ndo tatizo
   
 13. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #13
  Jun 24, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mkuu, umenivunja mbavu! Kweli nimecheka sana. Humu JF wakati mwingine ni mwa kuja kutoa tension za maisha. Nimecheka mpaka mbavu zaniuma.
   
 14. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #14
  Jun 24, 2009
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  daughter of a woman,stick to the gaddam topic,dont you dare bring in this 'ngambire' idiotics.Hopefully me has been understood.kind regards
   
 15. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #15
  Jun 24, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kilicho nishanga mie pale siku moja mama mmoja wa kikenya aliponisikia nasema yule mwanamke) aliniambia kwa kenya kusema mwanamke ni matusi nikawambia lugha yangu nimezaliwa nayo tena sina lugha nyingine ya makabila halafu unanambia ni matusi ?
   
 16. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #16
  Jun 24, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Ee wakenya kiswahili chao ndiyo hivo tena. Ila cha ajabu kule ng'ambo wakenya ndiyo wanaotambuliwa zaidi kwamba ndiyo wazungumzaji wa Kiswahili na si watanzania. Aisee, wale jamaa wanajua kujiweka mbele na kujitangaza.
   
 17. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #17
  Jun 24, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mimi nilidhani ni wahindi tu ndiyo una tatizo nao? Kumbe hata wahaya wanakusumbua! Kwa mtindo huo, ni watu gani unaowakubali? Tatizo la sumu ya ubaguzi ni kuwa haina mipaka. Ukishakuwa bigot basi utabaki hivyo hivyo.

  Amandla........
   
 18. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #18
  Jun 24, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Umenikumbusha siku moja mimi na rafiki yangu mganda tukaongelea juu ya vita ya Amin. Jamaa alikasirika kuona kuwa walidundwa. Na yeye alisema wazi kwamba ile vita iliwadhalilisha sana. Anasema mpaka leo wanajiona wanyonge sana mbele ya watanzania. Yaani ni kama watoto wetu baada ya kile kipigo. Anasema kiliwanyenyekesha. Huwa hawapendi kkuzungumzia hiyo kitu.
   
 19. m

  mokant Member

  #19
  Jun 24, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unajua waganda ni watu wa majivuno sana sasa ona kiingereza chenyewe wanachoongea kwa hakika hawana lafudhi sahihi yaani wanaboa kishenzi
   
 20. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #20
  Jun 24, 2009
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  hii TANZANIA yetu, sijui ina matatizo gani leo hii,mtanzania anamcheka mganda kwa lafudhi ya kiingereza?untill when tutapokubali ukweli we will always remain behind. REALITY ni kwamba east africa kiingereza tuwaachie waganda na wakenya we still not there yet
   
Loading...