Hivi vijana wengine mnaharakisha nini kuoa?

Hivi vijana wengine mnaharakisha nini kuoa?

aisee mamito pole sana kwa hayo

cha kufanya hebu tafuta wazee na ukoo wenu mkae mjadili na mmumwambie maisha ya ndoa yalivyo asidhani ni pipi kwenye ndoa kuna mengi ataweazaje kumlea mtoto wa watu huku hana kitu yaani ajishughulishi yeye mwenyewe ni mtegemezi kwenu ongeeni naye uenda kashalishwa ukubwa anataka kulenga na nazi yake nzima sijui kama ataiweza huyo

kingine nendeni kwa watumishi wa Mungu yaani mchungaji wako wewe na mumeo na huyo kijana akapate ushauri toka kule asiharakishe kuoa kwani kupo ataoa tu cha muhimu ajipange maisha kwanza na namna atakavyoweza kukaa na binti wa wa watu aisidhani kuoa ni masuala ya kitandani tu la hasha ni masuala mbalimbali ya maisha yako huko atuulize siye tuliopo kwenye ndoa tutamwambia mambo yakoje.

Ahsante shosti ntajitahidi kufanya hivyo.....
 
Sasa huyu ni kumpa live na mumeo pia wakufundwa mweeee ndoa si kukojozana ni zaidi
Mume wangu ni mtu mzuri sana ila kwenye tatizo anakua na Hasira sana ndio mana anasema mwache afanye yakishamkuta atajua,yani namuomba mungu anipe umri niwalee hawa watoto lakini nikifunga jicho wamepotea,sababu hata mdogo wake alipotaka kuoa wakaja kumwambia akasema kama anataka kuacha shule sababau ya mume sawa,mie nilibaki mdomo wazi........
 
Natamani uwe hata dada yangu wakufikia ili uje umshauri mama yangu.Kwa kweli anavyonilazimisha kuoa mpaka huwa na kosa amani.kila ninavyomueleza haelewi kwani anachodai anahamu na harusi achangiwe na wenzake.Wewe ni mama bora hongera usichoke kumpa darasa kijana hata akisema humpendi endelea tu.ipo siku atakukumbuka na kuona umuhimu wako.
 
Ahsante,lakini amenikosea sana kukubali sema hajakubali mbele yake manake wanamuogopa baba yao mimi ndio nilomwambia kua mtoto amesema anataka kuoa ndio yeye akasema Vizuri ndio nikamwambia atamuweka wapi huyo mke anasema kama vile ni kitu cha kawaida si atakaa hapa nyumbani.....

nooo,,, suala la kuishi nae hapo, nakuomba tena sana dada yangu...uwe na msimamo thabiti......mshauri mwenzio bila bugudha atakuelewa....
 
Acha aoe tu! ila gangamala hata kwa mume wako kuwa akishaoa hakuna kukaa hapa yeye na mke wake. Tena ulitakiwa uite kikao cha familia mumeo, huyo kijana na wewe, ulikosea kumsikiliza wewe mwenyewe ai ungewahi kwa mumeo umwambie then uitishe kikao cha familia.
 
Natamani uwe hata dada yangu wakufikia ili uje umshauri mama yangu.Kwa kweli anavyonilazimisha kuoa mpaka huwa na kosa amani.kila ninavyomueleza haelewi kwani anachodai anahamu na harusi achangiwe na wenzake.Wewe ni mama bora hongera usichoke kumpa darasa kijana hata akisema humpendi endelea tu.ipo siku atakukumbuka na kuona umuhimu wako.
Ahsante,mimi pia angefikia umri wakuoa na anao uwezo ningemshauri aoe sio kwasababu ya kuchangiwa vyombo na ukumbi wa harusi bali kwa kua mda umeshafika na anahutaji kua na majukumu na mimi nikiwa kama mama napenda nione wajuku zangu wakati nna nguzu na zaidi kumuepusha na maradhi..........
 
Acha aoe tu! ila gangamala hata kwa mume wako kuwa akishaoa hakuna kukaa hapa yeye na mke wake. Tena ulitakiwa uite kikao cha familia mumeo, huyo kijana na wewe, ulikosea kumsikiliza wewe mwenyewe ai ungewahi kwa mumeo umwambie then uitishe kikao cha familia.
Mkuu tatizo sio pakukaa bado namuona nimdogo kwakuchukua majukumu yakuoa angekubali amalize chuo ndio aoe nna hakika asingetaka kuoa baada ya mda lakini ameshikilia aoe ndio aende chuo hapo ndio tunaposhindana....
 
Mkuu uko sahihi amesema kama hajamuoa huyu mwanamke haendi tena chuo na atahamia kwa huyo mwanamke,mie nimemsikiliza na sikumpigia kelele nimetaka kujua akili yake inamtuma vipi,na akili yake imeshaharibiwa hata chakula hali nyumbani anatoka asubuhi kurudi saa3 usiku,wakati alikua ananipeleka kazini nakunifata akitoka kunishisha anakwenda offisini kwa Babake anakwenda kumsaidia kazi kama utaamini mtoto wangu mpaka chakula alikua ananipikia ananiletea nile kazini,hatoki mpaka aniulize Mama doo u need anything? hatoki bila kuni hug na yani he was the best...
Lazima uelezwe ukweli, shida yako si kumwoniea huruma ni wivu wa kiMzazi (nadhani unanipata - red). Hili ni jambo la kawaida kwa wazazi wa kike. kama anampenda mtoto wa kiume hapendi awe mbali naye. Mumeo kusema mtoto akililia wembe mpe naye ni Wivu wa kuona kijana anapendwa (si kimwili) anachukua nafasi yake. Hivyo akioa basi mumeo atafaidi love yako 100%
 
Usikubali kabisa huu ujinga wa huyo mtoto mwambie kabisa hutaki kusikia halafu uone atafanya nini! hata wanao kwambia umkubalie wambie hukubaliani nao kabisa! Mwambie aendelee na masomo kwanza swala la kuoa hakuna na kama anang'ang'ania atafute pa kumpeleka huyo mkewe na usije kumsupport kwenye hilo jambo! We mwambie unachojua sasa hivi yeye anasoma full stop hayo mengine huyajui na hutoyajua kabisa na hutaki kusikia! Katika hili unatakiwa kuwa na msimamo mmoja..yani katoto kana miaka 21 kanataka kuoa Mungu wangu halafu mkewe kamlete kwao duuuu!
yani anataka aoe apeleke mwanamke kwao?kazi kweli kweli,
 
Lazima uelezwe ukweli, shida yako si kumwoniea huruma ni wivu wa kiMzazi (nadhani unanipata - red). Hili ni jambo la kawaida kwa wazazi wa kike. kama anampenda mtoto wa kiume hapendi awe mbali naye. Mumeo kusema mtoto akililia wembe mpe naye ni Wivu wa kuona kijana anapendwa (si kimwili) anachukua nafasi yake. Hivyo akioa basi mumeo atafaidi love yako 100%

Mkuu hujanielewa vizuri labda huyu sio mtoto wangu wa kumzaa ni mtoto wa marehemu Shemji yangu nimemchukua akiwa na miaka6 na sasa ana 21,ivi kweli kama ni kijana wangu nilombeba tumboni mwangu miezi 9 naweza kuka kimnya nikaona maisha yake yanaharibika mbele ya macho yangu? mie sio mama wakuona wivu wa kiasi hicho...
 
Ahsante kwa ushauri wako na ntajitahidi na ntazidi kumuomba Mungu kwa jinsi nilivya ambiwa huyo binti anakaa shamba
sasa sijui kapewa nini mpaka adabu zikamtoka na wamejua kua sitokubaliananalo....
Uchawi unahusika hapo dawa za asili,maombi,dua n.k. zinahitajika hapo
 
Vijana hudanganyana sana wawapo vyuoni.

Lakini kama course yake ni mtaani most wanted,mwacheni!!
 
Wacha wamto!mb!ee fa!la!huyo wakilala kwenye madeka yao akili zinaisha nakuona mambo simple
 
sisi wa kristo tunaamini kuna funzo Mungu alikusudia kuwapa wana wa israel pale alipokuwa akiwatoa katika nchi ya misri utumwani kuelekea kaanani nchi ya ahadi. kwa jiografia ya eneo lile ingewachukua takribani wiki moja kufika kaanan lakini walitumia miaka 40. mungu alitaka kuwafunza alitaka kuwaondea moyo wa kibuli. Ndivyo ilivyo safari ya maisha yetu kuna wakati sehemu ya kufikia kwa mwaka tunatumia miaka na miaka sio kwasababu Mungu hapendi lakini kuna vitu ambavyo anahitaji tusiwe navyo kuna makosa tunafanya hata kama ukisamehewa makovu huwa hayafutiki. ukweli ni kwamba sio kila tulalolitaraji katika maisha yetu litaenda kama tulivyo tegemea na hapa wengi ndo huwa tunakosea. watoto wanamuogopa mume wako wanamjua wanakujua umewalea katika malezi ya kubebwa sana mzazi wa kiafrika mtoto huwezi kuwa na ujasiri huo. mimi ni mtoto am 2 yrs above you son but trust me unaonekanaa mama angu mdogo uko too democratic mtoto ni mtoto tu wewe ndo umemlea akionyesha hiyo tabia kuna somewhere na wewe ulikosea katika kuwalea i feel so sorry kijana wa 21 yrs kuwaza kuleta mwanamke Nyumbani it is shameful na usimchukue kaa mtoto nowdays watu wanawahi kubalee watu wanawahi kufa sikuhizi watu wanakuwa mapema ukikuta 21 yrs old ana save na kuwa na hata 2m hana kiwanja hana kibiashara there you have raise question. am sorry mumy kusema kuwa watu kama wewe ni muhimu kuwepo duniani sababu watu wenye moyo kama wako wasingekuwepo hakik wajinga na wapumbavu wangepat shida kuishi dunia hii lakini kwakuwa watu kama wewe mpo Mungu anawapa pumzi wana survive kupitia migongo yenu na maisha yanakuwa fairly balanced equation loss=gain. ila usiumie sababu watu kama hao lazima wawepo ili werevu wa survive hatuwezi wote tuwe matajiri nani atamtumikia mwenzie. Mgonjwa akiumwa doctor hashangiliii hadharani ila kimoyo moyo amepata kula yake. Angalia usije ukawa una struggle na curse za wazazi wao
 
mwambieni ajitegemee kwanza yy kama yy
thn akioa aende akaishi na mke wake
asijeoa ukaletewa mkwe hapo kwako!!
 
Mume wangu ni mtu mzuri sana ila kwenye tatizo anakua na Hasira sana ndio mana anasema mwache afanye yakishamkuta atajua,yani namuomba mungu anipe umri niwalee hawa watoto lakini nikifunga jicho wamepotea,sababu hata mdogo wake alipotaka kuoa wakaja kumwambia akasema kama anataka kuacha shule sababau ya mume sawa,mie nilibaki mdomo wazi........

Heee pambana
 
Sikujua Kama dunianii kuna watu wema Kama wewe.babangu alifariki nikiwa na miaka mitatu.mama akamfuata miaka Saba iliyofuatia.at the age of ten ilibidi niishi na ndugu ambao walinichukia Sana.nashukuru mungu sa hivi najitegemea.sikupata malezi mema.nashangaa huyu kijana pamoja na kufanyia yote hayo anakudharau...nadhani itabidi ukate usaidizi wako kwa mda ili aamke kutoka huo usingizi Wa ujinga
 
Back
Top Bottom