Hivi vijana wengine mnaharakisha nini kuoa?

Vijana wamekuwa mambulula kiasi inati huruma mm napita maana nimesha yaona siku mbili ndoa hakuna utaniambia
 
Yani mkuu nimeongea na wazazi wa hayu Binti hii asubuhi nakawambia kijana wangu bado mdogo anasoma shule bora tusubiri amalize huweai amini maneno alosema mzazi wa huyu binti,eeeh mdogo eeh mbona anavyokuja akimparamia anajua aichomeke wapi,mtoto kwako unakowalea kama mayai baba mzima kila unalo mwambia eti subiri nikamweleze Mama sasa kwa taarifa yako namsubiri kwa hamu hapa atakupa salam zangu,mie sikujua hata nimwambieje akakata cm..

jiandae kulipa mahali ya kuanzia m 1.5
 
Mkuu sio mdogo wangu ni mtoto wa shemeji yangu nimemchukua tangu anamiaka 6 sasa ana21 nimemsomesha nje sasa alikuja likizo ndio akakutana na hicho kituko amekolea,nimemuita Dad,babu yao wa kwa baba na bibi yao wa kwa mama ..watakuja jioni...
Usije kukubali kabisa hili swala kabisa hata kama ukibaki pekee mwenye msimamo huo! Usikubali kabisa na uwambie unakataa kwa kuwa unaona huyu kijana hajaweza kujitegemea kwa hiyo hauko tayari kuruhusu aoe..usikubali kabisa
 
Anatakiwa asikubali kabisa hili jambo na aking'ang'ania atafute pa kwenda na mkewe sio hapo kwake na ikiwezekana aitishe kikao kabisa na amueleze mbele ya ndugu zake kuwa hakubaliani na hilo jambo kabisa na hatokubali.

Mamy unasikia bora uonekane mbaya leo lakini unajenga
 
Vijana wamekuwa mambulula kiasi inati huruma mm napita maana nimesha yaona siku mbili ndoa hakuna utaniambia
Yani mie hata kufikiria sitaki kua ataoa sasaivi,nashindwa kuelewa ile ndoto alokua nayo ikowapi? mapenzi alokua anasema mama hakuna aneweza kuchukua nafasi yako na wewe ndio utanichagulia mimi mke unaemtaka wewe sababau sina chakukulipa Mom,leo hii amebadilika kupita maelezo....
 
​sawa una huruma ya mama lakini amekuwa mbishi sasa unamfanyeje mwache aende majuto ni mjukuu

Huyo mjukuu akuletee ulee tena never nikufute kinyesi nije nifute na mwanao pia hapana hakuna kupewa wembe
 
Yani na Wish angekua anajua kiasi gani anataka kuharibu maisha yake na nikimuliza umekutana na huyu binti wapi anasema shamba alikua anatembea na mtoto mgongoni all by herself she really tourched my heart,nilibaki namuangalia tuu...
Kuna jambo linaendelea si bure! Kijana amesha haribiwa ubungo kabisa na kinacho fata yawezekana hata chuo asirudi huyu lets wait.
 
Usije kukubali kabisa hili swala kabisa hata kama ukibaki pekee mwenye msimamo huo! Usikubali kabisa na uwambie unakataa kwa kuwa unaona huyu kijana hajaweza kujitegemea kwa hiyo hauko tayari kuruhusu aoe..usikubali kabisa
Ahsante sana kwakusimama na mimi japo najua kua hao wanaokija watasema mtoto akililia wembe mpe mimi simpi wembe ntampa kitabu asome na inshallah hata kama nimekufa atajua kama Mama amenipa elimu...
 
Amekua mbishi wala siamini kama ndio yeye ...........

Ishu yako ngumu lakini rahisi mkubalie lakini mpe masharti akiweza utamruhusu aoe mwambie alishe familia yenu kwa wiki 3 bila nyinyi kutoa hata shilingi akiweza basi yupo tayari kuoa akishindwa basi asubiri mda bado.
 
Yani na Wish angekua anajua kiasi gani anataka kuharibu maisha yake na nikimuliza umekutana na huyu binti wapi anasema shamba alikua anatembea na mtoto mgongoni all by herself she really tourched my heart,nilibaki namuangalia tuu...

Ha ha ha ha anaigiza tamthilia ha ha mwambie hapa ni bongo alafu aache maigizo hata ajala starehe za ujana anataka starehe za ubaba na umama he he he miss mie
 
Huyo mjukuu akuletee ulee tena never nikufute kinyesi nije nifute na mwanao pia hapana hakuna kupewa wembe
Unajua watu wanakimbia kusema mtoto akililia wembe mpe..wanasahau hili neno halifai kila sehemu! Akimkubalia kuoa huyu mtoto hakika atajuta kwanini alimkubalia maana atabeba mzigo mkubwa kuliko atakapo mkatalia! Katika hili anatakiwa awe namsimamo tuuu hakuna kuoa kama anataka kuoa atafute pakumpeleka mkewe na ajue jinsi ya kumlisha.

Akafinya mchezo huyu kijana hata shule inaweza kuwa mwisho wake maana naona ni wazi kuna kitu anafanyiwa kutoka kwa upande wa msicha..hakika hii ni zaidi ya uke...asije kukubali huu ujinga kabisa. Hakika kati ya story za jf hii imeniacha mdomo wazi kabisa.
 
Kuna jambo linaendelea si bure! Kijana amesha haribiwa ubungo kabisa na kinacho fata yawezekana hata chuo asirudi huyu lets wait.
Mkuu uko sahihi amesema kama hajamuoa huyu mwanamke haendi tena chuo na atahamia kwa huyo mwanamke,mie nimemsikiliza na sikumpigia kelele nimetaka kujua akili yake inamtuma vipi,na akili yake imeshaharibiwa hata chakula hali nyumbani anatoka asubuhi kurudi saa3 usiku,wakati alikua ananipeleka kazini nakunifata akitoka kunishisha anakwenda offisini kwa Babake anakwenda kumsaidia kazi kama utaamini mtoto wangu mpaka chakula alikua ananipikia ananiletea nile kazini,hatoki mpaka aniulize Mama doo u need anything? hatoki bila kuni hug na yani he was the best...
 
Yani mkuu nimeongea na wazazi wa hayu Binti hii asubuhi nakawambia kijana wangu bado mdogo anasoma shule bora tusubiri amalize huweai amini maneno alosema mzazi wa huyu binti,eeeh mdogo eeh mbona anavyokuja akimparamia anajua aichomeke wapi,mtoto kwako unakowalea kama mayai baba mzima kila unalo mwambia eti subiri nikamweleze Mama sasa kwa taarifa yako namsubiri kwa hamu hapa atakupa salam zangu,mie sikujua hata nimwambieje akakata cm..

Heheheee washamtengeneza, chezea visiwani? katengenezwa na ukoo mzima...

Mama amka usiku piga rakaa 2 muombe Munguu, halafu mshauri asali istikhara Allah atafanya maajabu yake...ila hapo pagumu, mzazi anajibu hivyoo?
 
Ha ha ha ha anaigiza tamthilia ha ha mwambie hapa ni bongo alafu aache maigizo hata ajala starehe za ujana anataka starehe za ubaba na umama he he he miss mie
shosti ameyavaa mapenzi vibaya na huyo mtoto wa shamba kajua kua huyu mtoto nimpindue vipi,na anavyo elekea huyu mtoto anapewa mpaka aseme mwenyewe basi......
 
Kuna jambo linaendelea si bure! Kijana amesha haribiwa ubungo kabisa na kinacho fata yawezekana hata chuo asirudi huyu lets wait.

Chezea watu, na ile location watu wanapenda ndoa hatari....na hivyo chakula anakula huko hukoo, duh...wa kuombewa dua tuuu huyu.
 
Unajua watu wanakimbia kusema mtoto akililia wembe mpe..wanasahau hili neno halifai kila sehemu! Akimkubalia kuoa huyu mtoto hakika atajuta kwanini alimkubalia maana atabeba mzigo mkubwa kuliko atakapo mkatalia! Katika hili anatakiwa awe namsimamo tuuu hakuna kuoa kama anataka kuoa atafute pakumpeleka mkewe na ajue jinsi ya kumlisha.

Akafinya mchezo huyu kijana hata shule inaweza kuwa mwisho wake maana naona ni wazi kuna kitu anafanyiwa kutoka kwa upande wa msicha..hakika hii ni zaidi ya uke...asije kukubali huu ujinga kabisa. Hakika kati ya story za jf hii imeniacha mdomo wazi kabisa.

Kweli kabisa kijana anapoelekea ni bora kupinga hadi mwisho ndiyo wanakimbilia kujiua ni bora afe kuliko kuleta mzigo nyumbani yani huyo dogo anashida yeye kapewa msaada ajaweza kusimama anataka kuleta mtu mwingine apewe msaada ningekuwa mimi huyo mama ningemjibu dry yamuume kuwa ndiyo mama yako angekubali mi siyo mama yako sasa ukiweza kusimama mwenyewe ukaplay nafasi ya mama na baba bila kutegemea popote ongeza mtu la sivyo subiri ni huo mkia unamsumbua unahamu ya kuchapa
 
Heheheee washamtengeneza, chezea visiwani? katengenezwa na ukoo mzima...

Mama amka usiku piga rakaa 2 muombe Munguu, halafu mshauri asali istikhara Allah atafanya maajabu yake...ila hapo pagumu, mzazi anajibu hivyoo?
Mkuu sikufichi sijalala hata kidogo tangu jana mpaka sasa,inshallah ntafanya hivyo na pia namsubiri Dad aje nimsikilize nini tufanye yani nikizubaa mtoto namkosa,naona ananitoka kwenye himaya yangu hivi hivi ......
na angalau yule mzazi wa binti angesema basi njoo tujadili ananijibu pumba ndio nimerowa nimajiiiiiiii...
 
Ahsante sana kwakusimama na mimi japo najua kua hao wanaokija watasema mtoto akililia wembe mpe mimi simpi wembe ntampa kitabu asome na inshallah hata kama nimekufa atajua kama Mama amenipa elimu...
Usikubali kabisa huu ujinga wa huyo mtoto mwambie kabisa hutaki kusikia halafu uone atafanya nini! hata wanao kwambia umkubalie wambie hukubaliani nao kabisa! Mwambie aendelee na masomo kwanza swala la kuoa hakuna na kama anang'ang'ania atafute pa kumpeleka huyo mkewe na usije kumsupport kwenye hilo jambo! We mwambie unachojua sasa hivi yeye anasoma full stop hayo mengine huyajui na hutoyajua kabisa na hutaki kusikia! Katika hili unatakiwa kuwa na msimamo mmoja..yani katoto kana miaka 21 kanataka kuoa Mungu wangu halafu mkewe kamlete kwao duuuu!
 
Back
Top Bottom