Hivi vazi la taifa limekwenda wapi?

Hivi vazi la taifa limekwenda wapi?

Fungu lilitengwa na likatumika, mmiliki wa radio akachaguliwa kuwa mmoja wa majaji wa kutafuta vazi la taifa, halafu leo viongozi wanapigana vikumbo kubuniwa suti na sheria ngowi, hii nchi kazi kweli kweli.
 
Tupo kwenye MCHAKATO, Designer yupo kwenye hatua za mwisho za UCHAMBUZI yakinifu, hivyo tuvute subira
 
Ni kwa nini tu siadopt vazi la wasabato walilovaa extravaganza dsm
 
Habarin zenu wana jamii?

Wanajamii napenda kuuliza kuhusu mchakato wa vazi la taifa uliishia wapi? Maana miaka kadhaa nyuma tulitaarifiwa kuwa kunamchakato wa kuandaa vazi la taifa,cjui huu mchakato umeishia wapi!

Hakuna cha feedback za aina yeyote kuhusu vazi la taifa na kwa wale waliopewa tenda wamekula `buyu'!
 
Mkuu mtafute Haki/sheria Ngowi nafkri atakueleza siri ya Mchakto,maana jamaa walienda kuonana na kumwonyesha ma wax,na mabatiki Mkulu wa nchi.

Hizo nguo za Sheria ngowi huwa ni za kubana sana anapenda nguo nyembamba sana sasa tukimwachia abuni Vazi la Taifa kazi ipo hapooo....
 
Tupo kwenye MCHAKATO, Designer yupo kwenye hatua za mwisho za UCHAMBUZI yakinifu, hivyo tuvute subira

Jaribu kuwacheki Kesho au wiki ijayo au hata mwezi ujao maana mwaka Huu bajeti haitoshi, haya Ndiyo maneno ya wale waliopewa Dhamana, kwa mtindo huu maendeleo kuja Tz itakuwa ndoto.
 
swali gani sasa hilo? unauliza u serious bongo?jisheshimu bana
 
haha hela ilishaliwa wanangoja tusahau halafu waanzishe tena this country bhana
 
Niache kuvaa suti au t-shirt na jinzi eti muniletee hayo mavazi kama magauni...kazi kuiga iga toka kwa wanaigeria tu. Hilo vazi la taifa litawasaidia nini? Mnaacha kupigania utambulisho wa utaifa wenu kupitia nguvu ya uadilifu, shilingi na uchumi wenu mnakazana eti vazi la taifa.
Eti unamuona mtu jukwaani amepiga vazi la taifa la Tanzania anatumbuiza lakini muziki wake vionjo vyote vya ki naijeria au Congo.
Vazi la taifa si mchakati wa kubuniwa na kuratibiwa, if you dont have it know that you missed it ni vitu ambavyo huja automatic. Hivi kwa uelewa wako unadhani hata ukileta vazi hili utafanikiw kumvua mzanzibari ianzu yake? Au Mmasai Lubega yake? Sahau!!
 
Hili suala la vazi la taifa n usanii mtupu. Suala la vazi ni suala la utamaduni, na utamaduni hautafutwi unaweza kuigwa tu. Wamasai walitafuta wapi vazi lao? Wahehe je? Vipi wanigeria,, walitafuta? Mao alipowalazimisha wananchi wake kuvaa nguo za aina moja walivaa. Lakini alipokufa tu kila mtu akaanza kuvaa nguo anayotaka. Kwa nchi yetu yenye ilivyo huwezi kuwa na vazi la aina moja ukisema ni vazi la taifa. Kama mtu asipovaa atafanywaje? Tuache usanii.
 
Naombeni kufahamu kuhusu mchakato wa vazi la taifa umefikia wapi? Ni muda sasa mchakato upo kimya.
 
Lini ulisikia sirikhali imeanzisha jambo ikalifikisha mwisho?
 
Acha kukumbushana machumgu mkuu. Si unaona aliyeanzisha huu mchakato mwanzoni alikuwa anataka urais lakini sasa kaukimbia hata ubunge wa mjini na anataka kujaribu huko Manda amboko nasikia nao wameshamshtukia!
 
Back
Top Bottom