Hivi tbc wanamdanganya nani?

Hivi tbc wanamdanganya nani?

Habari za tbc huwa zimechakachuliwa kama mkanda wa video waliotoa polisi kuhusu vurugu za arusha
 
Ndg. Wapendwa jana katika tarifa ya habari ya saa mbili usiku TBC walitangaza kuwa kiwango cha kufaulu matokeo kidato cha nne "chapanda" ikilinganishwa na mwaka uliotangulia. Hata Thread iliyokuwa ikipita chini ya luninga ilisoma hivyo. Tofauti na TBC, TV nyingine zilisema kiwango kimeshuka! hata magazeti ya leo yanathibitisha hilo!.

Swali, TBC walilenga kumdanganya nani? kwa malengo/makusudi/ gani? na manufaa ya nani? Chombo cha Umma kinapiga siasa hata katika maswala ya msingi kweli! Kunahaja ya kuwa na taasisi ya umma potofu kama hii?

Wazee wa kuchakachua!
 
Didia, Hivi huoni unjaza tu server za watubila sababu?, threads nyingine bwana!! umeona ukweli unao taka kweneye TV stations zingine na Magazeti then what else do you need? next time just tune to your best TV/Radio/News paper period!

yaani huwezi hata kufanya maamuzi ya nyumbani kwako hadi utafute ushauri humu?

sio lazima ujibu ulichojibu kaka, kila mtu ana haki ya kuelezea kile anachojisikia, ili mradi hajamkashifu mtu, na ndio maana ya forum, kama unaona post sio useful kwako basi pita tu sio lazima uchangie
 
System ya nchi hii ni uchakachuaji kila eneo:
  1. Wanachakachua mafuta
  2. Wamechakachua matokeo ya rais na wabunge
  3. Wamechakachua tukio la mauaji Arusha na jina la Mkennya waliyemuua
  4. Wamechakachua maamuzi ya CC juu ya Dowans na sasa wanamsingizia Chiligati kuwa hiyo ni kauli yake si ya CCM
  5. Sasa wanachakachua matokeo ya form IV....... sijui kwa faida ya nani?
 
Ndg. Wapendwa jana katika tarifa ya habari ya saa mbili usiku TBC walitangaza kuwa kiwango cha kufaulu matokeo kidato cha nne "chapanda" ikilinganishwa na mwaka uliotangulia. Hata Thread iliyokuwa ikipita chini ya luninga ilisoma hivyo. Tofauti na TBC, TV nyingine zilisema kiwango kimeshuka! hata magazeti ya leo yanathibitisha hilo!.

Swali, TBC walilenga kumdanganya nani? kwa malengo/makusudi/ gani? na manufaa ya nani? Chombo cha Umma kinapiga siasa hata katika maswala ya msingi kweli! Kunahaja ya kuwa na taasisi ya umma potofu kama hii?

Nakubaliana nawe kuwa hakuna haja ya kuwa na taasisi feki kama tbc ambayo inakula kodi ya wananchi. Hiki chombo tokea uchaguzi mkuu 2010 kimekuwa hopeless kabisa. Quality ya programs inashuka siku hata siku. Siku hizi kabla ya taarifa ya saa mbili usiku utaona mara mitambo imegoma mara muda unapita bila sababu yeyote ya msingi na hata kuomba radhi.

Kibaya zaidi ni kwamba tbc kwa sasa haina mkurugenzi (kuna kaimu tu) basi kuna kila juhudi za watu kujipendekeza kwa watawala ili wafikiriwe ktk nafasi hiyo. Hivyo watu wanajitahidi sana waonekane wanaipenda sana serikali ya Kikwete mfano ni hicho kitendo cha taarifa ya matokeao ya kidato cha nne kuonyesha kuwa kiwango cha ufaulu kimepanda!! Shameless people.
 
hata mimi sajawaelewa hata kidogo kwa walichofanya,naona imegeuzwa chombo cha propaganda,lakini wanachofanya TBC ni kuchakachua ueledi wa fani yao na si kingine,na ndio mana wakamtoa TIDO.:sick:
 
Hivi ninyi watu wa TBC mnayasoma haya? ama mkifika ktk Thread kama hizi huwa mnafimba machooooo?
badilikeni bwana na hayo ndio matunda ya kumtoa tildo kwa mambo yenu ya siasa

mapinduziiiiii daimaaaaa
 
hyo inaitwa TBCCM na hata habari zao ni za ki ccm.... ukisema uangaze ukweli na uhakika wana ku TIDO............... BE AWARE na hyo tv stataion kwani itakupoteza.....
 
Nakubaliana nawe kuwa hakuna haja ya kuwa na taasisi feki kama tbc ambayo inakula kodi ya wananchi. Hiki chombo tokea uchaguzi mkuu 2010 kimekuwa hopeless kabisa. Quality ya programs inashuka siku hata siku. Siku hizi kabla ya taarifa ya saa mbili usiku utaona mara mitambo imegoma mara muda unapita bila sababu yeyote ya msingi na hata kuomba radhi.

Kibaya zaidi ni kwamba tbc kwa sasa haina mkurugenzi (kuna kaimu tu) basi kuna kila juhudi za watu kujipendekeza kwa watawala ili wafikiriwe ktk nafasi hiyo. Hivyo watu wanajitahidi sana waonekane wanaipenda sana serikali ya Kikwete mfano ni hicho kitendo cha taarifa ya matokeao ya kidato cha nne kuonyesha kuwa kiwango cha ufaulu kimepanda!! Shameless people.


Mkuu nimekusoma.
 
hii tv nayo iko km comedy tu siku hizi.tangu aondoke Tiddo wameanza kurudi kule walikotoka badala ya kusonga mbele
 
Back
Top Bottom