Hivi Rais Magufuli kumuagiza Waziri wa Fedha atoe pesa shilingi bilioni mbili toka Hazina ni sahihi?

Katika ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, ibara ya 135(2) ninainukuu kama ifuatavyi "Fedha ambazo hazitawekwa kwenye mfuko Mkuu wa Hazina ya serikali ni zile zote ambazo zimetajwa na sheria kwamba zitumike kwa shughuli maalum" mwisho wa kunukuu

Sasa swali tunalojiuliza hivi pesa za ujenzi wa Makao makuu ya Chamwino hazijawekwa kwenye fungu hilo la Mfuko mkuu wa hazina ya serikali??
Kama kwenye Bajeti kuu hawakutenga wala kuidhinisha ujenzi wa Ikulu maana yake haipo mfuko mkuu lakini bado itakua hazina. Hakuna katiba iliyovunjwa chief.
 
Haya maagizo ni wazi ndiyo yananunua madege yasio na faida na kujenga zile njia za kuvukia ng'ombe kule chattle zenye mpaka mataa ya kuongezea magari.
JAYJAY
Absolutely true

Ni ukweli usiopingika kuwa Rais huyu ameamua kuisigina Katiba ya nchi waziwazi kabisa na hivyo kuzigeuza pesa zetu za Umna kama pesa zake binafsi!
 
Ninavyojua Mimi ni kuwa Bunge halijaidhinisha pesa hizo zitoke kwa matumizi hayo ya ujenzi ya Ikulu.
Tatizo bajeti ya serikali mnaisusia hamuisomi kutwa kushinda mitandaoni. Huwezi kutoa pesa ya serikali kama unakwenda kutoa pesa yako deci. Kuna mifumo, ambayo ni rahisi tu, waziri yeye ni kumuamuru paymaster general apeleke kwenye akaunti ya Jkt
 
Awamu ya 5 Prezzo yupo juu ya katiba.

Kama alimuagiza Mkuu Ndugai asilipe mishahara upinzani wakati ni "Miamala" miwili tofauti ndio ashindwe kumuagiza Waziri kutoa Mpunga wakati ni "Muamala" mmoja?
 
Kama pesa ya umma inatumika kujenga jengo la umma na sio nyumba yake binafsi tatizo lipo wapi?,na nikueleze tu kwa roho hiyo mbaya ya kumchukia Magufuli kuna hatari ya uzee wako kuwa mchawi mkubwa na ngazi ya familia na mtaa itakutenga.
 
Mystery,

Kashfa ya matumizi mabaya ya fedha za Serikali kwa awamu ya 5 itakuwa ni mbaya kuliko ESCROW na EPA za awamu ya 3 na ya 4.

Pesa ya umma inapigwa vibaya sana kupitia miradi ya UJENZI ambayo makampuni yanayo jenga yana mtandao unaohusisha viongozi wakubwa.

Najuwa Dr Philip Mpango ni msafi na ni professional mwenye integrity ya juu sana. Namshauri asiogope KUTUMBULIWA kwa ajili ya kuogopa vitisho vya Jiwe kwa kuwa miaka 5 ijayo Jiwe akiwa nje, basi yanayowakuta akina Kitilya na akina Rugemalira yatamkuta na Jiwe hata kuwapo kumtetea.

Nina log off
 
Mystery,

Sasa zimetolewa kwa kukumilisha miradi ya maendeleo na kwa umma na sio binafsi, ingekua kuwa katoa kwa maslahi yake sawa, acha uchizi.
 
Mystery,

Kuna mambo mengine hayataka urasimu, sasa mpaka bunge lipitishe hiyo miradi na wakandari wanapata wapi pesa za kuwalipa vibarua za kujikumumi wao, ndiyo maana hapo awali maendeleo yalichelewa sana kwa fikra kama hizi na mawazo kama yako.
 
Fedha zilizomo katika mfuko maalum wowote wa serikali, ukiachilia mbali Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali, hazitatolewa kutoka mfuko huo kwa ajili ya matumizi ila mpaka matumizi hayo yawe yameidhinishwa na sheria.
Hizo sheria zilipitagwa na wakti.
 
Back
Top Bottom