Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,477
- 30,130
Wananchi wote tumemsikia Rais Magufuli akimuagiza waziri wa Fedha, Dkt Philipo Mpango "achote" pesa kiasi cha shilingi bilioni mbili kwenye Hazina ya Taifa, ndani ya saa 24 na awaletee wakandarasi ili zikamilishe ujenzi wa Ikulu wa Chamwino na akaendelea kumpiga mkwara mzito waziri huyo kuwa ole wake asipozileta pesa hizo atakiona!
Swali langu ninaloliuliza, hivi njia hiyo ya kumuagiza waziri wa Fedha tena hadharani mbele ya macamera ya waandishi wa habari na kuendelea kumtisha kuwa ole wake asipotoa pesa hizo hazina ni sahihi kweli?
Ninavyojua mimi ni kuwa pesa zote za hazina ni mali ya Umma na siyo mali binafsi ya Rais na hakuna mtu yeyote mwenye uwezo wa kuagiza zitoke bali Bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania kwa mujibu wa Katiba ya nchi.
Ninavyojua Mimi ni kuwa Bunge halijaidhinisha pesa hizo zitoke kwa matumizi hayo ya ujenzi wa Ikulu
Hivi huyu Rais Magufuli anapata wapi kiburi cha kumwagiza waziri wa Fedha atoe hizo pesa ambazo hazijaizinishwa na Bunge la Jamhuri, ambalo linaendelea na vikao vyake hapo Dodoma?
Je, kwa kusikia wenyewe Rais Magufuli akimwagiza waziri wa Fedha "azichote" pesa hizo hazina, je ni pesa ngapi zinazotoka kwa aina hiyo ya kumwagiza waziri huyo wa Fedha?
Je, kwa "staili" hiyo ya Rais Magufuli ya kumwagiza waziri wa Fedha azitoe pesa hizo hazina tena akimtissha kuwa ole wake asipozitoa, je wananchi tutakuwa na "doubt" yoyote na ripoti ya CAG aliyepita, Profesa Assad, aliyeibua upotevu wa pesa za Umma, kwa kiasi cha shilingi trillion 1.5?