Hivi pesa inapatikana wapi?

Pm namba ya huyo jirani yako mkuu
 
Nacheka kama mazuri
 
Hivi unaelewa kwanza ninachokiongelea wewe kwenye mpira huwezi kutoboa Kwa huo umri we umekazana mtafutaji mara sijui nini wewe nenda Kabebe sembe
Hapo nimekutolea mfano wa umri

Miaka 30 ni mingi sana kuna baadhi ya madili huwezi fanya ndio maana nikasema umri unanitupa mkono nikiwa fukara hohehahe
 
Nimeenda migodini nimepiga veni na kanyero za kutosha sijapata pesa

Nimeingia porini kata miti na mbao sikupata pesa

Nimesoma hadi chuo pia olaa

Biashara ya uwakala, mitumba, viatu, viwanja, nyumba kote sijapata pesa

Oya pesa inapatina wapi mazee
Kosa lako ulikuwa unatumia nguvu bila mipango ndipo ulipokuwa unafeli.
Yaani wewe ulikuwa unafanya kitu kwa kukariri au kwa kusikia watu wengine kwamba mgodini kuna pesa sana kisha unakurupuka unaenda baadae unagundua hakuna hela.
Kumbe pesa iko mahali popote ulipo ukiweza kuchekecha ni kitu gani ni changamoto katika maeneo ulipo.
 
Sio kila mwenye Pesa ni pesa zingine ni za mashetani .
 
Kwahiyo kaacha biashara ya sembe
Zamani sana, ukimuona ana Bentley lake na wife anasukuma Range
Alipofanikiwa tu akanunua hizo biashara
Arudi tena adakwe wakati kaishafikia malengo

Wengine huwa wana tamaa mpaka washikwe, kila mara anasema hii ya mwisho
Anachezea hela zikiisha anarudi tena mwisho ananyongwa
 
Yaani kweli ata tapeli anakamatwa Kwa ajili ya tamaa tu
 
Kwenye kusaka pesa nguvu na akili vyote hutumika na lazima uingie kwenye bato uone kama kweli
 
Utatoboa kama ukituliza kichwa.
Wewe unaonekana ni aina ya watu wenye pupa au kwa lugha nyingine mihemko ukiwa mtu wa hivi kutoboa ni ngumu.
Kutoboa kunahitaji watu wenye creativity,focus,consistency sio kurukia mambo juu kwa juu.
Kwahiyo wanihakikishia baada ya miaka kumi mbele nitakuwa nimetoboa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…