Narudia kusema tena Wenje hajawahi kusoma ST Augustine...wewe hunajua kama Wenje alikuwa mwalimu tu wa kawaida pale Mwanza Thaqafa Sec. Uzuri JF sio sehemu ya majungu wala porojo weka CV ya Wenje tuone lini alisoma hicho chuo.
acha kuongea kitu usichokijua wewe,wenje kamaliza saut 2007.mda wote unatumia masaburi kuargue
tusijaribu kupotosha ukweli hapa kwa mapenzi yenye upofu na hisia hisia tu.....
elimu ni muhimu sana kwenye uongozi na haswa wakati huu wa globalization na interdependence kwenye siasa na uchumi ndani ya mfumo wa kimataifa wa sasa. elimu kwanza ni maarifa, kujiamini na muhimu zaidi elimu ni nidhamu na nidhamu ni kitu muhimu kwenye uongozi
hatutegemei darasa la saba au a level guy akaja kua rais na kwisha akaenda nje ya nchi akitegemea wasaidizi tu kwenye kila kitu, huyu ataobekana hana authority na hapa unakosa sifa za uongozi moja kwa moja.
Psychologically watu wasio na elimu kubwa utaka kucover hii deficiency na dictatorial behaviors, useless populist tactics ili kuonekana relevant na utaka yes men wawazunguke kwenye kila idara.
phd wasiokua wazalendo wapo wengi na wenye uzalendo pia wapo wengi, ila darasa la 7, au form 4 wenye maarifa na uzoefu wa kuongoza taifa katia karne ya 21 siwaoni pamoja na kwamba wanaweza kua wazalendo kama mimi na wewe au hata zaidi yetu. uzalendo pekee yake hautoshi kukupa uongozi wa juu wa taifa haswa kwa hawa waliotajwa ambao wengi wao hawajaprove kwenye nafasi zao za uongozi kwa zaidi ya miaka 5.
JK ana Degree ya
uchumi, mbona nchi yetu uchumi upo chini? Naunga mkono kwamba elimu ni
muhimu sana katika karine hii ila elimu zetu za bongo, viongozi wengi
wali-forge vyeti, yaani hilo ndilo tatizo kubwa, na bado mpaka sasa
wanaendelea kuforge. NAWASILISHA
Kwahiyo hakuna fisadi wa Elimu katika hili jopo, kama walivyojaa katika chama jirani (Gambaz)Hawa ni baadhi ya wabunge wa kuchaguliwa wa CHADEMA. Elimu ni muhimu ndio maana nimeona ni vyema mkafahamu viwango vya elimu vya viongozi ambao kesho na kesho kutwa tunatarajia wawe wawakilishi wetu katika medani za kitaifa na kimataifa:
1) Godbless Jonathan Lema -- BBA, ST Augustine --- Amevuliwa ubunge kwa sasa, kesi inaendelea.
2) Antony Gervase Mbassa - - Adv diploma - KCMC
3) Prof Kulikoyela Kanalwanda Kahigi --- Phd
4) Freeman Aikaeli Mbowe Form six
5) Highness Samsoni Kiwia ---- Secondary education O level
6) Simon Peter Msigwa - -- O level, Degree bible college.
7) Yohana Israel Natse --- Diploma in Education, Masters in theology.
8) Halima James Mdee --- Degree, UDSM
9) Zitto Zuberi Kabwe --- Degree (economic) UDSM, Masters degree (MLB)
10) Silvester Mhoja Kasulumbay Primary, Certifcate from Monduli Teachers college
11) John Magale Shibuda --- O LEVEL
12) Joseph Osmund Mbilinyi --- Form IV
13) David Ernest Silinde --- Degree(BCOM), UDSM
14) Mustapha Boay Akunaay Degree in law, Open University
15) Meshack Jeremiah Opulukwa --- Not updated
16) Philemon Ndesamburo --- Advanced diploma in Shipping
17) Said Amour Afri --- Primary school
18) Vicent Kiboko Nyerere -- O level
19) Ezekia Dibogo Wenje --- Degree, St Augustine
20) Joseph Roman Selasini --- Degree, UDSM
21) Tundu Antiphas Mughwai Lissu ___ LLM Masters degree
22) John John Mnyika --- CV not updated
23) Salvatory Naluyaga Machemuli ___ Degree DIT
24) Joshua Samwel Nassari Not updated
CV ya 'DR' WILBROD SLAA HII HAPA:
Kuzaliwa, elimu ya msingi na sekondari
Dk. Slaa alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1948 katika Wilaya ya karatu. Alipata elimu ya msingi katika shule za Karatu na Kwermusi (Mbulu) kati ya mwaka 1958 na 1965. Alisoma elimu ya sekondari katika Shule za Dungunyi Seminari na Itega Seminari kati ya mwaka 1966 na 1971.
Mafanikio ya DK. Slaa kielimu na Kitaaluma
Dk. Slaa ana shahada na atashahada zifuatazo.
Sharada ya Uzamivu (PhD) katika Sheriaü ya kanisa kutoka Chuo kikuu cha St. Urban, Rome.
Stashahada ya Theolojiaü kutoka Kipalapala Seminari.
Stashahada ya falsafa kutoka Kiboshoü Seminari.
Stashahada ya Afya ya Macho kutoka Kituo cha Kimataifa chaü Macho.
Ni muhimu vyama kujipanga na kutokufanya mchezo na uongozi wa taifa. Sikujua mwaka ule Mbowe alipogombea urais, alipitishwa kwa vigezo gani? Uzoefu kazini au kitu gani hasa? Mtakaochangia mtatujuvya. Msitukane tu.
Kama mawaziri watatokana na wabunge, basi CHADEMA inaweza kuwa na wabunge ambao kielimu wanaweza kuwa kikwazo katika kutekeleza majukumu yao.
Indhari:
Chanzo cha taarifa hii ni kutoka kwenye web site ya bunge. Therefore, kama kuna kosa lolote unaweza kusahihisha. Si lengo kupotosha.
UJUMBE:
Tusidharau elimu wakati wa kuteua wagombea kuwakilisha watanzania.
WITO:
Tupeleke mapendekezo katika CRC ya kutaka mawaziri wasitokane na wabunge, kwa vile inaweza kuja kuwa tatizo kupata wabunge walio na sifa za kuongoza wizara.
Bayana Nawe unataka kuwa katika lile genge la watumwa humu jamvini siyo??
Acha kudanganya umma.
Mleta mada weka CV yako kwanza halafu utuambie umelifanyia nini taifa hili mpaka sasa hivi.
kisha weka CV za hao magamba wako unaodhani wana elimu kubwa na kila mmoja wao elezea amelifanyia nini taifa hili.
CV kubwa hazina maana kwetu kama unachojivunia ni kuwa fisadi na kulifanya taifa lako kuwa masikini
babu huyo mngoni umempaisha sana, hapo kwenye red ni koogwe bana sio ushoto, ushoto ni half london kule ati, wasomi wengi ndo maana hata nyumba alokuwa anaishi mkoloni edward twinning ipo kuleProfesa Maji Marefu, Nursery School Ushotto
Lusinde Kudadadadeki, STD 1V Mtera Kata school
Kapt John Komba, Certificate of Nursery school, Mbinga. Diploma in Shot Klia, shot Klia..... Hima!, JWTZ; International certificate in Mgeniii, Mgeni huyu balaaaa..... TOT Taarab and Choir.
Sijui niendelee?
Leo imeguswa CHADEMA kuhusu elimu naona ngonjera zimekuwa nyiingi! Angetajwa mwengine kama alivyoguswa yule waziri aliyesema TZ ni muungano wa Unguja na Msubmbiji! Ungeona humu magwanda jinsi walivyomshambulia kutaka kuonesha umuhimu wa elimu.
Au ndio maana mnavaa magwanda hata wakati wa kiangazi kwa kushindwa kujua hata utabiri wa hali ya hewa?
Inshort chama kina hitaji reforms.
Mkumbuke ule msemo usemao ''ELIMU YA MJINGA NI MAJUNGU''
Musa alipowaongoza wana wa islael alikuwa na na elimu gani?.Yesu alikuwa na Elimu gani? kawawa JE? Mrema? SOKOINE?.Tunachokitaka Watanzania ni BUSARA.kama uongozi ungekuwa Ni Elimu basi Rais wa nchi hii angekuwa DR Slaa ama PRO LIPUMBA.Kwani wanamzidi Kikwete.Je Maji Marefu na Mbunge wa nyanghwale wana Elimu gani?