Hivi ndivyo viwango vya elimu vya 'majembe' ya CHADEMA!

Hivi ndivyo viwango vya elimu vya 'majembe' ya CHADEMA!

Tuashumu hatujui elimu ya JK na Mbowe alafu tuwape nafasi kufafanua mikakati ya kutukwamua na umaskini then uambiwe hawa mmoja wao ni form six utamchagua nani?
 
Naomba tujiulize maswali,
>hawa ndio wanaoinyima serikali na chama tawala usingizi,wanaoingiza hiz taarifa za wabunge kwenye mtandao wa bunge ameajiriwa na nani kama si serikal inayoundwa na CCM?,watendaji wa chama tawala watashindwaje kuwachakachulia CV zao tu kwasababu wana nia yao ya kuchukua nchi.

>Tusiwe wepesi kuamini kila kitu,hivi mmoja kati ya hawa jamaa wakishindanishwa na rais kutoa speech iwe formal au informal it's obvious rais ataweweseka.

Ukifuatilia vizuri hawa jamaa wana uelewa na taaluma ya uongozi,elimu ya darasani inaweza isiapply popote katika uongozi wake kwahiyo these guys are superb!

Mkuu umenena.
 
Kwa maana hiyo elimu haina umuhimu? ya O'Level tu inatosha! Haina haja ya kuwa na Vyuo viingi, si ndo manake? sikubaliani na wewe!

Hujajibu hoja niliyoiweka hapa. Halafu sijui wewe ni wa wapi mkuu? Hivi Rais au waziri au mbunge ni nani hadi ahitaji sijui degree ya engineering, udaktari au ya ualimu? Urais ni taasisi! Rais anafanya maamuzi yake kwa kutumia wataalamu mbalimbali. Ikulu kuna wanasheria wenye PhD, kuna maingeneer, kuna wataalamu wa elimu na kila kada ambao wanamshauri Rais katika maeneo husika. Rais haendi kugonga vyuma Ikulu hadi atakiwe kuwa degree au PhD ya uhandisi, wala haendi kufundisha kule kiasi cha kumtaka awe na degree ya ualimu. Kusoma na kuandika na kiingereza kidogo vinatosha kabisa. Kinachohitajika ni busara zake tu za namna ya kuingoza nchi na uelewa mpana wa maisha na mambo yanayolihusu taifa lake.

Unanishangaza sana ndugu unaponambia eti hatuhitaji kuwa na vyuo vingi. Hivi vyuo vingi ni kwa ajili ya kutoa marais na wabunge wengi au kwaajili ya kuandaa wataalam wa idara mbalimbali? Tunahitaji wataalamu wa kila aina katika idara mbalimbali, lakini si lazima hao wawe marais. Si lazima sana kwamba rais awe ni mtaalam wa uchumi au uhandisi ndipo aweze kuongoza nchi. Mkapa alikuwa mwandishi wa habari, Nyerere alikuwa mwalimu, Kikwete ni mwanauchumi. Angalia tofauti zao za uongozi. Mwanauchumi ndo kavurunda kushinda wenzake wote. Sasa degree yake ya uchumi imelisaidiaje taifa? Think twice. Tunahitaji hekima zaidi kuliko shule za darasani.

Halafu mnaposimama hapa kujigamba juu ya elimu rejeeni upya bungeni na kuchunguza mijadala inayoendelea huko. Ni hao hao akina Msigwa mnaosema hawana elimu ndiyo wanaowakimbiza mchakamchaka akina professor magembe na vimeo vingine vya CCM kule bungeni. Ni hao hao akina Sugu na Wenje na Kiwia ndiyo wanaowatoa baro madokta na maprofessor wa CCM bungeni. Hawa watu hawana elimu ya darasani lakini wanaona mbali mara mia moja zaidi ya CCM.
 
Mkuu, inamaana wanaotakiwa kuwa na elimu ni CHADEMA tu hasa MBOWE kama ulivyo highlight kwenye thread yako?. Kama kweli wewe hauna mawazo mgando, tunaomba utuletee .cv .za watu wa CUF, TLP, UDP, CCM, CCK , ADC, CCJ, SAU , TPP, UPDP, NCCR, DP et cetera et cetera .
 
Uongozi na hekima haifundishi darasani ni kipaji watu wanachozaliwa navyo. Ndio maana mabilionea wengi sana hapa Duniani ni Ma drop out.

Tukirudi kwenye Ubunge, kwa kutumia katiba yetu ya sasa ibara ya 67 inasema hivi:

67.-(1) Subject to the provisions contained in this Article, any person
shall be qualified for election or appointment as a Member of Parliament if he -
(a) is a citizen of the United Republic who has attained the age of twenty-one years and who can read and write in Kiswahili or English; and
(b) is a member and a candidate proposed by a political party.

Kwa kutumia vigezo hivyo juu ni uwezo wa kuandika kiswahii au kingeereza ndio minimum requirement ya kugombea ubunge as far as Education is concerned.

Ni bora uwe na kiongozi wa darasa la saba Mzalendo kuliko kuwa na PHD where hata utendaji wako uko so poor.

Ninamifano zaidi ya 40 ya vijana viongozi tanzania ambao talents zao za uongozi zilianzia sekondari hata kabla wajamaliza eimu zao za vyuo vikuu. Kwa hiyo elimu ya chuo kikuuu is a Plus but is not the ultimate measure of Leadership quaity
 
  • Thanks
Reactions: ral
Mwanangu Mseven I am your father whether you like it or not. Sioni kosa langu hadi univue ubaba wenu. Najua. Huenda nimewagusa vibaya wapendwa wako kama siyo wewe. Baba yenu anapenda watoto walioelimika na si wababaishaji. Hamuwezi kuwakosoa CCM wakati nanyi mna tatizo hilo hilo. Siku zote baba yenu ni msemakweli bila kujali kama ukweli wake utapendwa au kuchukiwa.
 
Hivi ukiambiwa orodhesha majina ya wanafamilia yenu, utaanza na mamako au babako au mtoto , utaanza na lako au la mkeo au mtoto.

Itifaki lazima izingatiwe huwezi kumweka mwenyekiti wa chama namba nne wakati hauna vigezo vya kufanya hivyo, maana hauna mpangilio wa kuandika kwa aidha viwango vya elimu, umri n.k.
 
Hata kama ni sahihi, CDM inamajembe mengi yenye elimu nzuri kushinda hata wale wa Magamba. Wengi unaowasikia wanajitambulisha kama wana CDM humu JF wana shule nzuri sana na wengi wao utawasikia 2015.
 
Profesa Maji Marefu, Nursery School Ushotto
Lusinde Kudadadadeki, STD 1V Mtera Kata school
Kapt John Komba, Certificate of Nursery school, Mbinga. Diploma in Shot Klia, shot Klia..... Hima!, JWTZ; International certificate in Mgeniii, Mgeni huyu balaaaa..... TOT Taarab and Choir.

Sijui niendelee?

no justification here...uliowataja ni wapiga ramli tu hapa na pale wanatumika bila ya kua cream ya maamuzi ya CCM...waliotajwa na mleta mada ni cream ya CDM/yaani ndiyo CDM yenyewe na ni watu wenye maamuzi ya mwisho na ya juu.

jaribu kukomaa kiakili na kutofautisha ushabiki na kupoteza muda na hoja muhimu zinazohitaji majibu makini haswa katika muda ambao tunalalamika kuhusu uongozi mbovu na kushuka kwa elimu yetu hapa nchini
 
Huyo jamaa ni wa ajabu sana, baada ya kumuwekea link naona amekimbia

alitaka mwenyewe tena kwa ujasiri utadhani ameshaitembelea hyo website..!ogopa sana mtu anebisha kwa confidence kitu asichokifaham
Kwa uongo huo naconclude kwamba ritz=muongo namba moja jf ova
 
Hii ndiyo CV ya 'DR' WILBROD PETER SLAA:

Kuzaliwa, elimu ya msingi na sekondari

Alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1948 katika Wilaya ya karatu. Alipata elimu ya msingi katika shule za Karatu na Kwermusi (Mbulu) kati ya mwaka 1958 na 1965. Alisoma elimu ya sekondari katika Shule za Dung'unyi Seminari na Itega Seminari kati ya mwaka 1966 na 1971.

Dk. Slaa ana shahada na atashahada zifuatazo.
Sharada ya Uzamivu (PhD) katika Sheriaü ya kanisa kutoka Chuo kikuu cha St. Urban, Rome.
Stashahada ya Theolojiaü kutoka Kipalapala Seminari.
Stashahada ya falsafa kutoka Kiboshoü Seminari.
Stashahada ya Afya ya Macho kutoka Kituo cha Kimataifa chaü Macho.

Huyu ndiye mnayepambanishwa na Kikwete! Sasa hivi mnampanisha na ZITTO katika urais!

CHADEMA ILIANZA KAMA NGO YA WATU KUTAFUTIA HELA. MNAHITAJI KUIBADILISHA KUWA CHAMA AMBACHO KITAKUJAKUSHIKA HATAMU ZA UONGOZI WA TAIFA HILI. Msifanye mchezo jamani, taifa mtaliangamiza.

Kweli CCM ni tatizo lakini CDM utakuwa msiba mkuu. Slaa anafaa kumrithi Kardinali pengi ili kanisa liende mbele sio uongozi wa taifa hili. Elimu yake ni haba sana kumpa urais. Ni mtazamo tu lakini, msitukane, jibuni kwa hoja.
 
aiseeeeeee babaangu umefika muda kila m2 aweke cv yake

mkuu rombo
premary education; mengwe premary
sec education : makalema
diploma : kilimanjaro
agriculture
kazi : bwana shamba
mkowa wa rombo

sina digree wala master

na wewe weka yako ni si kuangalia ya mwezako
anza ritz
 
Uongozi na hekima haifundishi darasani ni kipaji watu wanachozaliwa navyo. Ndio maana mabilionea wengi sana hapa Duniani ni Ma drop out.

Tukirudi kwenye Ubunge, kwa kutumia katiba yetu ya sasa ibara ya 67 inasema hivi:

67.-(1) Subject to the provisions contained in this Article, any person
shall be qualified for election or appointment as a Member of Parliament if he -
(a) is a citizen of the United Republic who has attained the age of twenty-one years and who can read and write in Kiswahili or English; and
(b) is a member and a candidate proposed by a political party.

Kwa kutumia vigezo hivyo juu ni uwezo wa kuandika kiswahii au kingeereza ndio minimum requirement ya kugombea ubunge as far as Education is concerned.

Ni bora uwe na kiongozi wa darasa la saba Mzalendo kuliko kuwa na PHD where hata utendaji wako uko so poor.

Ninamifano zaidi ya 40 ya vijana viongozi tanzania ambao talents zao za uongozi zilianzia sekondari hata kabla wajamaliza eimu zao za vyuo vikuu. Kwa hiyo elimu ya chuo kikuuu is a Plus but is not the ultimate measure of Leadership quaity

tusijaribu kupotosha ukweli hapa kwa mapenzi yenye upofu na hisia hisia tu.....

elimu ni muhimu sana kwenye uongozi na haswa wakati huu wa globalization na interdependence kwenye siasa na uchumi ndani ya mfumo wa kimataifa wa sasa. elimu kwanza ni maarifa, kujiamini na muhimu zaidi elimu ni nidhamu na nidhamu ni kitu muhimu kwenye uongozi

hatutegemei darasa la saba au a level guy akaja kua rais na kwisha akaenda nje ya nchi akitegemea wasaidizi tu kwenye kila kitu, huyu ataobekana hana authority na hapa unakosa sifa za uongozi moja kwa moja.

Psychologically watu wasio na elimu kubwa utaka kucover hii deficiency na dictatorial behaviors, useless populist tactics ili kuonekana relevant na utaka yes men wawazunguke kwenye kila idara.

phd wasiokua wazalendo wapo wengi na wenye uzalendo pia wapo wengi, ila darasa la 7, au form 4 wenye maarifa na uzoefu wa kuongoza taifa katia karne ya 21 siwaoni pamoja na kwamba wanaweza kua wazalendo kama mimi na wewe au hata zaidi yetu. uzalendo pekee yake hautoshi kukupa uongozi wa juu wa taifa haswa kwa hawa waliotajwa ambao wengi wao hawajaprove kwenye nafasi zao za uongozi kwa zaidi ya miaka 5.
 
Hii ndiyo CV ya 'DR' WILBROD PETER SLAA:

Kuzaliwa, elimu ya msingi na sekondari

Alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1948 katika Wilaya ya karatu. Alipata elimu ya msingi katika shule za Karatu na Kwermusi (Mbulu) kati ya mwaka 1958 na 1965. Alisoma elimu ya sekondari katika Shule za Dung’unyi Seminari na Itega Seminari kati ya mwaka 1966 na 1971.

Dk. Slaa ana shahada na atashahada zifuatazo.
Sharada ya Uzamivu (PhD) katika Sheriaü ya kanisa kutoka Chuo kikuu cha St. Urban, Rome.
Stashahada ya Theolojiaü kutoka Kipalapala Seminari.
Stashahada ya falsafa kutoka Kiboshoü Seminari.
Stashahada ya Afya ya Macho kutoka Kituo cha Kimataifa chaü Macho.

Huyu ndiye mnayepambanishwa na Kikwete! Sasa hivi mnampanisha na ZITTO katika urais!

CHADEMA ILIANZA KAMA NGO YA WATU KUTAFUTIA HELA. MNAHITAJI KUIBADILISHA KUWA CHAMA AMBACHO KITAKUJAKUSHIKA HATAMU ZA UONGOZI WA TAIFA HILI. Msifanye mchezo jamani, taifa mtaliangamiza.

Kweli CCM ni tatizo lakini CDM utakuwa msiba mkuu. Slaa anafaa kumrithi Kardinali pengi ili kanisa liende mbele sio uongozi wa taifa hili. Elimu yake ni haba sana kumpa urais. Ni mtazamo tu lakini, msitukane, jibuni kwa hoja.
Naona mkuu sasa umeamua kuingia katika mkombozi pekee aliyebaki, PROPAGANDA ZA UDINI.
 
Mkuu, inamaana wanaotakiwa kuwa na elimu ni CHADEMA tu hasa MBOWE kama ulivyo highlight kwenye thread yako?. Kama kweli wewe hauna mawazo mgando, tunaomba utuletee .cv .za watu wa CUF, TLP, UDP, CCM, CCK , ADC, CCJ, SAU , TPP, UPDP, NCCR, DP et cetera et cetera .

Tunaangalia chama ambacho ni kikubwa kwa sasa. Hivyo vingine vitakuja baadaye wakati ukifika. Tafsiri ya mawazo mgando au yaliyoyeyuka nakuachia wewe. Cha msingi CDM ijitafakari upya. La sivyo tutakuwa tunafanya mzaha na taifa hili.
 
Wamesoma wapi. tujue inawezekana wamepotosha bunge
 
Naona mkuu sasa umeamua kuingia katika mkombozi pekee aliyebaki, PROPAGANDA ZA UDINI.

Vijembe vipo kwenye siasa! Nimetumia vijembe vya watani wenu CCM Kipotezee hicho kipengele, gusa hivyo vingine kama una ubavu tukuone!
 
Back
Top Bottom