Hivi ndivyo viwango vya elimu vya 'majembe' ya CHADEMA!

Hivi ndivyo viwango vya elimu vya 'majembe' ya CHADEMA!

Hawa ni baadhi ya wabunge wa kuchaguliwa wa CHADEMA. Elimu ni muhimu ndio maana nimeona ni vyema mkafahamu viwango vya elimu vya viongozi ambao kesho na kesho kutwa tunatarajia wawe wawakilishi wetu katika medani za kitaifa na kimataifa:

1) Godbless Jonathan Lema -- BBA, ST Augustine --- Amevuliwa ubunge kwa sasa, kesi inaendelea.
2) Antony Gervase Mbassa - - Adv diploma - KCMC
3) Prof Kulikoyela Kanalwanda Kahigi --- Phd
4) Freeman Aikaeli Mbowe – Form six
5) Highness Samsoni Kiwia ---- Secondary education – O level
6) Simon Peter Msigwa - -- O level, Degree bible college.
7) Yohana Israel Natse --- Diploma in Education, Masters in theology.
8) Halima James Mdee --- Degree, UDSM
9) Zitto Zuberi Kabwe --- Degree (economic) UDSM, Masters degree (MLB)
10) Silvester Mhoja Kasulumbay – Primary, Certifcate from Monduli Teachers college
11) John Magale Shibuda --- O LEVEL
12) Joseph Osmund Mbilinyi --- Form IV
13) David Ernest Silinde --- Degree(BCOM), UDSM
14) Mustapha Boay Akunaay – Degree in law, Open University
15) Meshack Jeremiah Opulukwa --- Not updated
16) Philemon Ndesamburo --- Advanced diploma in Shipping
17) Said Amour Afri --- Primary school
18) Vicent Kiboko Nyerere -- O level
19) Ezekia Dibogo Wenje --- Degree, St Augustine
20) Joseph Roman Selasini --- Degree, UDSM
21) Tundu Antiphas Mughwai Lissu ___ LLM – Masters degree
22) John John Mnyika --- CV not updated
23) Salvatory Naluyaga Machemuli ___ Degree – DIT
24) Joshua Samwel Nassari – Not updated

CV ya 'DR' WILBROD SLAA HII HAPA:
Kuzaliwa, elimu ya msingi na sekondari

Dk. Slaa alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1948 katika Wilaya ya karatu. Alipata elimu ya msingi katika shule za Karatu na Kwermusi (Mbulu) kati ya mwaka 1958 na 1965. Alisoma elimu ya sekondari katika Shule za Dung’unyi Seminari na Itega Seminari kati ya mwaka 1966 na 1971.

Mafanikio ya DK. Slaa kielimu na Kitaaluma

Dk. Slaa ana shahada na atashahada zifuatazo.
Sharada ya Uzamivu (PhD) katika Sheriaü ya kanisa kutoka Chuo kikuu cha St. Urban, Rome.
Stashahada ya Theolojiaü kutoka Kipalapala Seminari.
Stashahada ya falsafa kutoka Kiboshoü Seminari.
Stashahada ya Afya ya Macho kutoka Kituo cha Kimataifa chaü Macho.

Ni muhimu vyama kujipanga na kutokufanya mchezo na uongozi wa taifa. Sikujua mwaka ule Mbowe alipogombea urais, alipitishwa kwa vigezo gani? Uzoefu kazini au kitu gani hasa? Mtakaochangia mtatujuvya. Msitukane tu.

Kama mawaziri watatokana na wabunge, basi CHADEMA inaweza kuwa na wabunge ambao kielimu wanaweza kuwa kikwazo katika kutekeleza majukumu yao.

Indhari:
Chanzo cha taarifa hii ni kutoka kwenye web site ya bunge. Therefore, kama kuna kosa lolote unaweza kusahihisha. Si lengo kupotosha.

UJUMBE:
Tusidharau elimu wakati wa kuteua wagombea kuwakilisha watanzania.

WITO:
Tupeleke mapendekezo katika CRC ya kutaka mawaziri wasitokane na wabunge, kwa vile inaweza kuja kuwa tatizo kupata wabunge walio na sifa za kuongoza wizara.

Naomba ikiwezekana tuwekee na ya profes Maji marefu tafadhali
 
Hii ndio shida ya kujadili mambo ya msingi na watu wasiotaka kutumia bongo zao walizopewa na mwenyezi mungu. Badala yake wanafikiri mambo yatakwenda tu kwa kutumia vitabu vilivyotokana na bongo za wengine ambao wakati wanaandika hayo hawakua na vitabu.
 
Mbona mnapenda kupotosha umma Lema hajawahi kusoma ST AUGUSTINE UNIVERSITY wala Wenje naye hajawahi kusoma.
Cc to.. Ngongo,

Ritz wewe ndo utakuwa unajaribu kupotosha umma.Kwa mfano Wenje alianza kusoma Diploma ya ualimu Butimba na baadae akapata kazi Thaqaafa secondary kama mwalimu kisha akaenda HILLCREST secondary.Baada ya hapo akapata tenda za kijamii za kusafisha jiji tena barabara ya Rufiji.Kisha akaenda kusoma ST AUGUSTINE UNIVERSITY na ku-graduate ndipo Barclays bank baadae na wewe tafuta sasa
 
Last edited by a moderator:
naam shahada ni ushahidi ulionekana st augustine au hata harvard.Elimu ni kile unachotumia kilichobakizwa kwako ukishasahau uliyofundishwa ama kukariri!Swali ni iwapo wewe PhD uliyeleta mada na huyu MBOWE uliyemtuhumu kamaliza FORM 6 nani kweli ANA AKILI na kukubalika?Prof Sarungi alishindwa na Class 7 na wengineo.
Elimu za kukariri nazo deal?
 
Jamaa hiyo naomba 12 umebug men. Jamaa aliishia Form II men. Kama unaamini uwezo wa kuongoza hauhusiani na CV kwa nini useme uongo??!!!!!!!!
 
naam shahada ni ushahidi ulionekana st augustine au hata harvard.Elimu ni kile unachotumia kilichobakizwa kwako ukishasahau uliyofundishwa ama kukariri!Swali ni iwapo wewe PhD uliyeleta mada na huyu MBOWE uliyemtuhumu kamaliza FORM 6 nani kweli ANA AKILI na kukubalika?Prof Sarungi alishindwa na Class 7 na wengineo.
Elimu za kukariri nazo deal?

Unafikiri Mbowe alianza kukubalika lini kwa kumbu kumbu zako? Na ni kipi hasa kilimpa umaarufu? Yeyote anaweaza kujibu kama ukishindwa.
 
Watu kama akina Nape ndio wanaandika vitu vya kijinga kama hivi.
Kwanza kama elimu ndio kigezo cha kuwa kiongozi muadilifu, then kesho nachoma vyeti vyangu vyote! Degree zetu hazina maana kabisa!

choma leo
 
Sawa jembe hebu endelea kutujuza zaidi maana elimu kwa siasa ya sasa ni ya muhimu isije ikawa ya kina waziri nanihii anasema tanzania ni muungano wa zimbabwe na tanzania.
 
Sina uhakika kama CV ya Mbowe ipo sawa. Nadhani ana Masters kama sikosei. Wanaomfahamu kwa karibu wafuatilie.

Lakini kwa upande mwingine, elimu na utendaji ni vitu viwili tofauti kabisa. Tuna madokta na maprofessor wengi tu kwenye serikali ya CCM na bado hawajaweza kuleta mapinduzi yoyote yenye tija kwa taifa letu zaidi ya kulitia umaskini mkubwa usiomithilika. Nchi hii iliwahi kuwa na waziri mkuu mwenye elimu ya kawaida kabisa (Mzee Kawawa -RIP), na bado akaitumikia nchi kwa uaminifu mkubwa kuliko hao wenye PhD, Masters na vinginevyo.

Kwa mfano kwa elimu ya O-level mimi sioni kama ni shida kwa mtu kama huyo kuongoza nchi hata kama ingekuwa kwenye level ya urais. Kuna mtu anasema ingekuwaje kama Rais angekuwa hajasoma. Mimi namshangaa kwani Rais ndiyo amesoma kuliko Watanzania wengine wote? Mbona ana bachelor tu tena gentlemen na bado anawaongoza wenye PhD, post docs na Maprofessor? Idd Amin alikuwa na elimu gani na aliwaongoza waganda wenye elimu gani? Kule Njombe kaskazini sisi tuna mbunge Jah people hakuwahi kuingia darasani hata siku moja. lakini ndiyo mbunge wetu. Huwezi kumlinganisha hata na mbunge mmoja wa CHADEMA.

Tuache kupigia talumbeta mambo yasiyo na umhimu, tuangalie kwanza mambo ya msingi ambayo taifa letu kwa sasa linapungukiwa. Na tuangalie hawa watu pamoja na usomi wao mdogo wana mchango gani bungeni na katika mabadiliko ya kiuchumi na kijamii katika nchi yetu?
Kiongozi anapokuwa na Elimu ya kuridhisha inamsaidia kufikia malengo yake mazuri ya uongozi na utawala??. Je uongozi wa Amin idd ulikuwa bora? "fedha ya nchi inashuka thamani jibu ni kuchapisha noti za kutosha" Sema yote karne hii elimu ni muhimu sana. Ndio maana wazazi mnawapeleka wanenu shule waacheni wachunge ngombe.
 
Elimu ni mihimu sana,lakini tumeshuhudia viongozi wa bara la Africa wenye Elimu wanavyo shindwa kuendesha Inchi,ni vizuri ungeweka na CV za uhadilifu!
viongozi wa afrika wanatumika na mataifa beberu, sio kwamba hawajui. wanaweza sana kuongoza. na ndio maana kuna kitu kinaitwa "AFRICAN MANAGEMENT"
 
acha ujinga Ritz na kama kitu hujui ni bora ukae kimya kuliko kupiga propaganda za kike humu kwani kuna faida gani kudanganya mtu usimyemjua? Wenje ana Degree ya SAUT na kasome na wakina Moses Maachali na mpka muda huu mkosamali naye anasoma hapa SAUT degree ya sheria.
Degree ya SAUT ni ipi hiyo? somo gani hilo, nisaidie.
 
Tuashumu hatujui elimu ya JK na Mbowe alafu tuwape nafasi kufafanua mikakati ya kutukwamua na umaskini then uambiwe hawa mmoja wao ni form six utamchagua nani?
mikakati ya kujikwamua na umaskini kinadharia mbowe anaweza kivitendo no. Mie nasema hv: ukitaka kutokomeza umaskini fanya sana kazi.
 
Uongozi ni kipaji, wakati wa nyerere julius kambarage anakabidhiwa nchi, kwanza alikua kijana, na diploma ya ualimu tu, lakini alichofanyia nchi hakuna fisadi ataweza ata akipewa karne moja.
 
Vatican wanataka paddre wao arudi wamewekeza sana kumsomesha alichosomea hakifanyii kazi anapiga domo tu mbowe ana degree ya kupigisha disco pale bilicanas anaitwa dj beby
 
Ritz wewe ndo utakuwa unajaribu kupotosha umma.Kwa mfano Wenje alianza kusoma Diploma ya ualimu Butimba na baadae akapata kazi Thaqaafa secondary kama mwalimu kisha akaenda HILLCREST secondary.Baada ya hapo akapata tenda za kijamii za kusafisha jiji tena barabara ya Rufiji.Kisha akaenda kusoma ST AUGUSTINE UNIVERSITY na ku-graduate ndipo Barclays bank baadae na wewe tafuta sasa
nimepata jibu la kwa nn wenje mkorofi au mtukutu. Thaqaafa na hillcrest ni miongoni mwa shule zenye utovu wa nidhamu(wanafunzi) jjn mza. tena kapata tenda ya usafi mtaa wa rufiji aka uswazi, dah
 
Hawa ni baadhi ya wabunge wa kuchaguliwa wa CHADEMA. Elimu ni muhimu ndio maana nimeona ni vyema mkafahamu viwango vya elimu vya viongozi ambao kesho na kesho kutwa tunatarajia wawe wawakilishi wetu katika medani za kitaifa na kimataifa:

1) Godbless Jonathan Lema -- BBA, ST Augustine --- Amevuliwa ubunge kwa sasa, kesi inaendelea.
2) Antony Gervase Mbassa - - Adv diploma - KCMC
3) Prof Kulikoyela Kanalwanda Kahigi --- Phd
4) Freeman Aikaeli Mbowe – Form six
5) Highness Samsoni Kiwia ---- Secondary education – O level
6) Simon Peter Msigwa - -- O level, Degree bible college.
7) Yohana Israel Natse --- Diploma in Education, Masters in theology.
8) Halima James Mdee --- Degree, UDSM
9) Zitto Zuberi Kabwe --- Degree (economic) UDSM, Masters degree (MLB)
10) Silvester Mhoja Kasulumbay – Primary, Certifcate from Monduli Teachers college
11) John Magale Shibuda --- O LEVEL
12) Joseph Osmund Mbilinyi --- Form IV
13) David Ernest Silinde --- Degree(BCOM), UDSM
14) Mustapha Boay Akunaay – Degree in law, Open University
15) Meshack Jeremiah Opulukwa --- Not updated
16) Philemon Ndesamburo --- Advanced diploma in Shipping
17) Said Amour Afri --- Primary school
18) Vicent Kiboko Nyerere -- O level
19) Ezekia Dibogo Wenje --- Degree, St Augustine
20) Joseph Roman Selasini --- Degree, UDSM
21) Tundu Antiphas Mughwai Lissu ___ LLM – Masters degree
22) John John Mnyika --- CV not updated
23) Salvatory Naluyaga Machemuli ___ Degree – DIT
24) Joshua Samwel Nassari – Not updated

CV ya 'DR' WILBROD SLAA HII HAPA:
Kuzaliwa, elimu ya msingi na sekondari

Dk. Slaa alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1948 katika Wilaya ya karatu. Alipata elimu ya msingi katika shule za Karatu na Kwermusi (Mbulu) kati ya mwaka 1958 na 1965. Alisoma elimu ya sekondari katika Shule za Dung’unyi Seminari na Itega Seminari kati ya mwaka 1966 na 1971.

Mafanikio ya DK. Slaa kielimu na Kitaaluma

Dk. Slaa ana shahada na atashahada zifuatazo.
Sharada ya Uzamivu (PhD) katika Sheriaü ya kanisa kutoka Chuo kikuu cha St. Urban, Rome.
Stashahada ya Theolojiaü kutoka Kipalapala Seminari.
Stashahada ya falsafa kutoka Kiboshoü Seminari.
Stashahada ya Afya ya Macho kutoka Kituo cha Kimataifa chaü Macho.

Ni muhimu vyama kujipanga na kutokufanya mchezo na uongozi wa taifa. Sikujua mwaka ule Mbowe alipogombea urais, alipitishwa kwa vigezo gani? Uzoefu kazini au kitu gani hasa? Mtakaochangia mtatujuvya. Msitukane tu.

Kama mawaziri watatokana na wabunge, basi CHADEMA inaweza kuwa na wabunge ambao kielimu wanaweza kuwa kikwazo katika kutekeleza majukumu yao.

Indhari:
Chanzo cha taarifa hii ni kutoka kwenye web site ya bunge. Therefore, kama kuna kosa lolote unaweza kusahihisha. Si lengo kupotosha.

UJUMBE:
Tusidharau elimu wakati wa kuteua wagombea kuwakilisha watanzania.

WITO:
Tupeleke mapendekezo katika CRC ya kutaka mawaziri wasitokane na wabunge, kwa vile inaweza kuja kuwa tatizo kupata wabunge walio na sifa za kuongoza wizara.

this is only you can do?
 
Nijuavyo elimu haipatikani darasani tu, kuna wasomi waliobobea lakini ni bure kabisa. Kuna michango na mawazo ambayo hutolewa na wenye shahada za elimu Bungeni hadi nashangaa.
Juzi juzi alipokamatwa Sheikh Ponda, msomi mmoja mbobevu na mwanasiasa, alinishangaza sana kwa maoni aliyoyatoa.

Sasa kama wabunge ni hoi kiasi hicho, unategemea mawaziri watafanyaje kazi hata kama hawatatokana na wabunge.

Hivi nyie mnaelewa maana ya Bunge na Kazi zake? Basi ni rahisi kuwa waziri kuliko mbunge maana hapo ndio mambo yote yanaanzia, mawaziri ni watekelezaji tu ya yale ya kutoka bungeni. Pengine ufikirie kitu kidogo tu, BAJETI. Waziri hawezi kuendelea na bajeti bila idhini ya Bunge.

Nilifurahi sana wakati mtaalamu Ibrahim wa Zanzibaa akiwaeleza kamati ya wawakilishi juu ya mjadala wa Muungano, pale walipolalamika kuwa Dodoma wameongoza vipengele vingi visivyokuwepo kwenye muungano. Alipowajulisha kuwa baraza la wawakilishi lilichaguwa wajumbe kati ya wawakilishi kujadili mambo hayo na hatimaye wakakubaliana na kuwaonyesha sahihi zao, hawakuwa na la kujibu. Ushauri wake wasipeleke wawakilishi mbumbu mbu Dodoma, kwani watachokipitisha huku kitakuwa halali na kitachobaki ni utekelezaji tu.

Hivyo kuweni macho na wabunge. Mbumbumbu OUT!
 
Back
Top Bottom