Hivi ndivyo viwango vya elimu vya 'majembe' ya CHADEMA!

Hivi ndivyo viwango vya elimu vya 'majembe' ya CHADEMA!

Uongozi ni uwezo na siyo elimu wala umri na vipato. Wako wapi PhD holders ambao leo hii wanashuhudia wanyama wakiamishwa kwenda nchi za kiliberali pasina kushauri lolote?... Degree ni afya.
Ufike wakati sasa tutoe wito kuwachagua viongozi wenye vision na mission na siyo waliosoma Harvad wakaja kutumaliza. think twice ndugu............... Jongea Mtanzania
 
Nionavyo mimi, siku hizi kuna kuudhulia na kusoma inagwa mwisho wa siku wote wanatoka na vyeti kama wahitimu. Kwa mfano anayenunua mitihani au kufanyiwa mtihani akapata degree na yule anayefanya mtihani kwa kujitegemea, wote hawa kwenye mahafali wanavaa majoo na kushangilia kumaliza chuo.

Ukweli unakuja kubainika huku kwenye utendaji hasa wanapokuwa wanafanya kazi kwenye taasisi za serikali zisizozingatia uwajibikaji, ndio maana ukienda ofisi fulani unakosa huduma au kwanza utoe kitu kidogo, na hata ukitoa kitu kidogo bado upati huduma stahiki kwakuwa anayekuhudumia ana degree lakini hana ujuzi unaotokana na degree yake!
 
Nchi huwa inategea wazalendo. atu wanaoipenda nchi yao kwa dhati KABISA ndio wawe viongozi. Hao waliopo wenye vyeti vya MGAWO na vya KUNUNUA, wamefanya nini? Mbali na kuonyesha UTAALAMU wao wa KUUZA chi?
 
zitto zuberi kabwe au Tzzk 2015 ana phd
Halima james mdee ana masters ya sheria kaipatia south africa.
Lema std seven.

mbowe form four certificate.
 
Uongozi ni uwezo na siyo elimu wala umri na vipato. Wako wapi PhD holders ambao leo hii wanashuhudia wanyama wakiamishwa kwenda nchi za kiliberali pasina kushauri lolote?... Degree ni afya.
Ufike wakati sasa tutoe wito kuwachagua viongozi wenye vision na mission na siyo waliosoma Harvad wakaja kutumaliza. think twice ndugu............... Jongea Mtanzania

Uliwezaje kupima vision ya Mbowe na Slaa walipojiunga na CHADEMA wakati ule?
 
Nchi huwa inategea wazalendo. atu wanaoipenda nchi yao kwa dhati KABISA ndio wawe viongozi. Hao waliopo wenye vyeti vya MGAWO na vya KUNUNUA, wamefanya nini? Mbali na kuonyesha UTAALAMU wao wa KUUZA chi?
Kijana kuwa na heshima, una maana hao wenye vyeti hapo juu walinunua? Interesting, leo magwanda mnaonesha your true colours and your way of thinking. Na hii ni kutokana na kupingana na facts! Haya endelea....
 
Ok Bring on... SUGU Vs MUHONGWA, Nani unafikiri anaweza kuweka mikataba feki hadharani kwa maslahi ya Taifa letu? Jibu kampe mkeo, mumeo, basha lako, kimada wako na hata mwajiri wako aliekuajiri hapa mtandaoni...
 
Hakuna lolote wewe? Mbona Rais mwinyi alikuwa na diploma tu lakini aliongoza vizuri/ Cha msingi nikuwa na viongozi safi lakini elimu kubwa sana si ya lazima. Chenge na usomi wake si kauwa TRC?
Chalii angu usifananishe Tanzania na Marekani hata siku moja. Bora ungefananisha Tanzania na Burundi, Malawi. Zambia.
 
Elimu n ki2 cha msingi sana ukiangalia hawa wabunge wa chadem n zaid ya asilimia 74 hawana elimu inayofaa, anayetaka kulingansha na ccm anacha bse watu kama hao ccm inao zaid ya miahamsn bungen so. Elim inamata.

hivi ni bora kuwa na watu wenye elimu ya kati alaf wana msaada kwa taifa au ni bora kuwa na watu wenye elimu kubwa alaf nchi inaendelea kuwa masikini na hawana msaada wowote!

Je una kubali hao wasomi mia hamsini unao wasema kutoka sisimweli ndio wame tufikisha hapa tulipo?
 
Dokta Kikwete na Dokta Deodorus Kamala wamepatia wapi vyeti vyao vya udokta? Pia kuna Dokta Salha Batilda Buriani yule wa daraja mbili Arusha aliyegombea ubunge akaangukia pua na sasa ni balozi wa Tz huko Kenya na pia aliwahi kuwa naibu waziri katika wizara mbalimbali ikiwamo ya mazingira. Ni weupi kama machicha ya nazi, wamebaki kushindana kujipachika elimu wasizokuwa nazo tu. Nasubiri jibu ili niendelee kufumua mabomu. Usidhani nimemsahau Dokta Shukuru Kawambwa, huyu ni aibu tupu kwa taifa.
 
Hawa ni baadhi ya wabunge wa kuchaguliwa wa CHADEMA. Elimu ni muhimu ndio maana nimeona ni vyema mkafahamu viwango vya elimu vya viongozi ambao kesho na kesho kutwa tunatarajia wawe wawakilishi wetu katika medani za kitaifa na kimataifa:

1) Godbless Jonathan Lema -- BBA, ST Augustine --- Amevuliwa ubunge kwa sasa, kesi inaendelea.
2) Antony Gervase Mbassa - - Adv diploma - KCMC
3) Prof Kulikoyela Kanalwanda Kahigi --- Phd
4) Freeman Aikaeli Mbowe – Form six
5) Highness Samsoni Kiwia ---- Secondary education – O level
6) Simon Peter Msigwa - -- O level, Degree bible college.
7) Yohana Israel Natse --- Diploma in Education, Masters in theology.
8) Halima James Mdee --- Degree, UDSM
9) Zitto Zuberi Kabwe --- Degree (economic) UDSM, Masters degree (MLB)
10) Silvester Mhoja Kasulumbay – Primary, Certifcate from Monduli Teachers college
11) John Magale Shibuda --- O LEVEL
12) Joseph Osmund Mbilinyi --- Form IV
13) David Ernest Silinde --- Degree(BCOM), UDSM
14) Mustapha Boay Akunaay – Degree in law, Open University
15) Meshack Jeremiah Opulukwa --- Not updated
16) Philemon Ndesamburo --- Advanced diploma in Shipping
17) Said Amour Afri --- Primary school
18) Vicent Kiboko Nyerere -- O level
19) Ezekia Dibogo Wenje --- Degree, St Augustine
20) Joseph Roman Selasini --- Degree, UDSM
21) Tundu Antiphas Mughwai Lissu ___ LLM – Masters degree
22) John John Mnyika --- CV not updated
23) Salvatory Naluyaga Machemuli ___ Degree – DIT
24) Joshua Samwel Nassari – Not updated

CV ya 'DR' WILBROD SLAA HII HAPA:
Kuzaliwa, elimu ya msingi na sekondari

Dk. Slaa alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1948 katika Wilaya ya karatu. Alipata elimu ya msingi katika shule za Karatu na Kwermusi (Mbulu) kati ya mwaka 1958 na 1965. Alisoma elimu ya sekondari katika Shule za Dung’unyi Seminari na Itega Seminari kati ya mwaka 1966 na 1971.

Mafanikio ya DK. Slaa kielimu na Kitaaluma

Dk. Slaa ana shahada na atashahada zifuatazo.
Sharada ya Uzamivu (PhD) katika Sheriaü ya kanisa kutoka Chuo kikuu cha St. Urban, Rome.
Stashahada ya Theolojiaü kutoka Kipalapala Seminari.
Stashahada ya falsafa kutoka Kiboshoü Seminari.
Stashahada ya Afya ya Macho kutoka Kituo cha Kimataifa chaü Macho.

Ni muhimu vyama kujipanga na kutokufanya mchezo na uongozi wa taifa. Sikujua mwaka ule Mbowe alipogombea urais, alipitishwa kwa vigezo gani? Uzoefu kazini au kitu gani hasa? Mtakaochangia mtatujuvya. Msitukane tu.

Kama mawaziri watatokana na wabunge, basi CHADEMA inaweza kuwa na wabunge ambao kielimu wanaweza kuwa kikwazo katika kutekeleza majukumu yao.

Indhari:
Chanzo cha taarifa hii ni kutoka kwenye web site ya bunge. Therefore, kama kuna kosa lolote unaweza kusahihisha. Si lengo kupotosha.

UJUMBE:
Tusidharau elimu wakati wa kuteua wagombea kuwakilisha watanzania.

WITO:
Tupeleke mapendekezo katika CRC ya kutaka mawaziri wasitokane na wabunge, kwa vile inaweza kuja kuwa tatizo kupata wabunge walio na sifa za kuongoza wizara.

mkuu you brighten my day. sikutarajia kama chadema kuna vilaza kwa kiasi hiki. du! sina hamu kabisa.
 
Bayana elimu ni kitu kipana saana co kama unavyozan kwamba elimu hupatikana darasani tu laa c kweli.... Kama wewe ni mfatiliaje wa mambo ya teknolojia hapa dunian bas nazan utakuwa unamjua Steve Jobbs, Jobbs ni mtu aliye leta mapinduz ya teknolojia hapa dunian, kwanza ni co founder wa apple, ndio designer na mwanzishi wa matumizi ya mouse kwenye computer, vile vile ndiye aliyeleta mapinduz ya smart phone, mwanzilishi wa tablets kama ipad, na mwasisi wa digital music device kama ipod na ndio apple walioleta revolutionary user interface and gui chini ya Steve Jobbs. Lakin Steve Jobbs alikuwa hana elimu chuoni hata kidogo lakin ndio mtu aliyetela mabadiliki makubwa kwenye teknolojia. Sasa kuwa na diploma, degree, masters au PhD c kitu kama sio mzalendo jaman wanaccm
 
Mwandishi mzuri anatafiti toka source ambayo ni ya kuaminika zaidi ya moja na kufikia hitimisho, vinginevyo utakua hujatenda haki! next time give yourself time to research from more than one credible sources.
 
I have no doubt with the source that I have used. Kama una updates zozote ni nyongeza tu na unaweza kuziweka hapo watu wakaziangalia.
 
Bayana elimu ni kitu kipana saana co kama unavyozan kwamba elimu hupatikana darasani tu laa c kweli.... Kama wewe ni mfatiliaje wa mambo ya teknolojia hapa dunian bas nazan utakuwa unamjua Steve Jobbs, Jobbs ni mtu aliye leta mapinduz ya teknolojia hapa dunian, kwanza ni co founder wa apple, ndio designer na mwanzishi wa matumizi ya mouse kwenye computer, vile vile ndiye aliyeleta mapinduz ya smart phone, mwanzilishi wa tablets kama ipad, na mwasisi wa digital music device kama ipod na ndio apple walioleta revolutionary user interface and gui chini ya Steve Jobbs. Lakin Steve Jobbs alikuwa hana elimu chuoni hata kidogo lakin ndio mtu aliyetela mabadiliki makubwa kwenye teknolojia. Sasa kuwa na diploma, degree, masters au PhD c kitu kama sio mzalendo jaman wanaccm

Humjui Stev Jobs vizuri itakuwa ulisimuliwa tu. Hebu pata desa la Steve hapa ujue zaidi acha kudanganya umma.

Short Bio | all about Steve Jobs.com

Sasa unamfananisha Steve Jobs na nani kwenye chama chako, Mbowe au Slaa? Kwa lipi lenye uwiano?
 
mkuu you brighten my day. sikutarajia kama chadema kuna vilaza kwa kiasi hiki. du! sina hamu kabisa.
Bofya kwenye like hapo uwaoneshe magwanda nguvu ya umma!!:smiling:
 
Jamani tusitetee ujinga kwa vile wanaoguswa tunawashabikia. Mambo ya elimu haipatikani darasani US iliongozwa na marais wasio na diploma yamepitwa na wakati. Elimu ni muhimu tutake tusitake. Hivi nani yuko tayari kwa mfano kuongozwa na rais asiyejua kusoma na kuandika katika karne ya 21? Sasa mnatetea nini hapa? Angekuwa ameandikwa Salma Kikwete kama kihiyo hapa kila mmoja angehanikiza kumtaka asome. Mie nadhani wabunge wa CDM ambao Resumes zao haziko safi wanapaswa kwenda shule. Bila kusoma watapitwa na wakati. Mfano Mbowe aliwahi kuwa admitted Hull University. Je ni kwanini hakumaliza masomo yake? Alifeli, alikuwa na udhuru?
Point of correction, to all contributors!!!! Tanzania hatuna elimu (am stand to be corrected), tuna mfumo tunaouita elimu wa kujifunza kusoma na kuandika kiingereza thats all, ndio maana kiujuzi ( I mean technical know how) hakuna tofauti kubwa kati ya form four, form six, graduate, masters holder na PHD kwa category ileile ya specialization. Wanachotofautiana ni namna tu ya kuitafsiri kutokana na ukomavu wa lugha ya kiingereza. Najua kwa majority sintoeleweka, but kwa wenye fikra pevu wanaweza kuthink critically na kuelewa ninachomaanisha. Mfano rahisi tu, tuna watu watatu wa fani moja (Fundi wa magari wa mtaani std VII, mhitimu wa VETA mechanical technician, Graduate wa mechanical Engineering), wote kwa pamoja wapelekewe gari bovu la aina moja, (wa kwanza atatumia uzoefu na kubahatisha bahatisha kutafuta tatizo, wa pili atatumia technical practice, wa tatu atatumia translation skills), kama hiyo model ya gari hakuna kati yao aliyewahi kukutana nayo kabla, hakuna atakayekuwa na ufumbuzi wa tatizo. Hii ina maana elimu tunayopokea, ni ya utambuzi tu na si ujuzi. Kama tungepata elimu ya ujuzi, Leo hii so called bingwa wa electronics, PHD. Mwandosya angekuwa na kitu cha kujivunia katika mwendelezo wa electronics nchini, na si kuagiza tu technology toka nje. Leo hii far east wako juu sana sababu wanafundisha elimu ya ujuzi, na si kujua sana lugha za kigeni. Lugha ni muhimu sana kwa mawasiliano, lakini je tunawapa elimu ya ujuzi watu wetu?????? Ama tumebaki kuwa taifa la Loliondo????

Kwa mtazamo wangu, tofauti za viwango vya madarasa walivyonavyo viongozi wetu si kigezo cha ufanisi wao bali, dhamira, muono na utashi wa kila mmoja katika kutafuta mbinu za kutatua shida mbalimbali za kijamii kwa kushirikiana na wanaowaongoza.
 
Ok Bring on... SUGU Vs MUHONGWA, Nani unafikiri anaweza kuweka mikataba feki hadharani kwa maslahi ya Taifa letu? Jibu kampe mkeo, mumeo, basha lako, kimada wako na hata mwajiri wako aliekuajiri hapa mtandaoni...

nyie ndo viumbe mnaoiharibia cdm inaonekana ni chama cha wahuni!!! Hivi huwezi kukomenti bila kutukana?hivi unaona ujanja ni kutangaza mikataba hadharani kama matangazo ya vifo?labda me naishi dunia nyingine nielimishe,japo kunijuza nchi moja tu ambayo inatangazaga mikataba yake hadharani na kuichapisha magazetini kama ilivyo?hizo justifikesheni mnazotumia kuwatetea hao wasomi wa cdm zinatoa taswira ya namna mnavyofikiri/uwezo wenu wa kufikiri.
 
Kwa nnavyofahamu Mbowe ana degree ya uchumi ya Udsm, na alikwenda hull university uingereza kwa ajili ya kusomea masters
 
Back
Top Bottom