Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
TUsisahu kitu kimoja hapa...mwakyembe anasema kuna mambo walificha kulinda heshima ya serikali..wasiwasi wangu hili scandal ni la serikali nzima ya JK....mana kama kuna vitu vilifichwa kulinda heshima ya serikali, ni vitu gani hivyo wakati vilivyotolewa tu vilitosha waziri mkuu kujiuzulu? vingetolewa na hivyo vilivyofichwa? nadhani JK angejiuzulu...pole sana Lowasa, umetolewa kafala ilhali mlikuwa wengi hata na swaiba wako JK...we hukumbuki wakati wa mjadala mkali, JK alipotoka ziara ya marekani alithibitisha kukutana na wamiliki wa kampuni ya RICHMOND, lakini baadae akina mwakyembe wanasema Richmond ni kampuni hewa!..., Mbona Kamati ya Mwakyembe haikumuhoji Rais kujua hao aliokutana nao Marekani na kuzungumza nao ni akina nani?...Pole sana EL......mlikuwa wengi, lakini ilikuwa zamu yako.
Kinachonishangaza ni hiki cha Wabunge na kamati za Bunge kudai kuwa wanafanya mambo mengine kwa kuinusuru Serikali au kulinda heshima ya Serikali.
Sasa najiuliza, wao kama mhimili wa Tatu wa Serikali kwa mujibu wa Katiba, inakuwaje wnaonea haya makosa ya Serikali kwa gharama za jasho na kodi za Mwananchi wa Tanzania?
Leo hii wanapigana vikumbo Bungeni kuilaumu Serikali kuwanyanyasa na kuwakosea heshima kwa kuhojiwa na TAKUKURU, lakini wao ni wepesi kuionea huruma Serikali Kuu na kuilindia heshima!
Huu ni unafiki na mbaya zaidi ni undumilakuwili ambako kunafikia kulifanya Bunge letu lionekane kama ni wapiga mhuri kwa matakwa ya Serikali Kuu na Chama kinachotawala na zaidi ni kuwa Bunge letu bado halijawa huru na kua na uwezo wa kuidhibiti Serikali.
Nikisema kuwa Wapiganaji wanapigania nini au kuhoji kelele za kung'ang'ania koo moja na simfumo mzima mbovui wa kiutendaji, naambiwa sina akili au nikae kimya!
Ndio maana leo hii Pinda na Sitta wanatishana, ndio maana mwaka jana na juzi Lowassa na Sitta walitishana na ni kutokana na Bunge kushindwa kuwajibika na kujilinda kwa kutumia Katiba kwa kuogopa mkao wa Kikao cha Chama.
Leo hii isingekuwa Wahisani kuhoji kilichotokea Dodoma wakati wa kikao cha mwishi cha NEC ambacho kilimsulubisha Sitta, Serikali na CCM wasingetoa kauli za kujisahihisha au kusema Spika wa Bunge (ambaye Kikatiba ni mhimili mkuu na mtu mwenye hadhi yake) hakuwekwa kwenye kikaango na kudiriki kuwasuta Wabunge wake wenyewe kwa kushindwa kulizungumzia suala la taratibu za Kibunge ndani ya Bunge.
Hata hili suala la posho za Wabunge kwenye vikao au wao kuwa ni wajumbe wa bodi na kupata posho mara mbili ni mtego ambap Wabunge wenyewe wamejiwekea na wanaanza kunaswa kama Paya.
Ikiwa Spika anadiriki kudai eti kupewa Posho ya ziada ni Utamaduni wa Kitanzania na hivyo kuihalalisha na ukikimbuka zile kauli zake za kusema Wananchi wakihongwa na Mafisadi wapokee hongo, je unadhani Spika na Bunge wana heshima gani tena au uwezo gani kuidhibiti Serikali?
Kwa nini Mwakyembe aseme waliilindia Heshima Serikali lakini wakamkaba koo Waziri Mkuu? je Waziri Mkuu si Serikali na Kiongozi Mkuu wa Serikali Bungeni?