Lole Gwakisa
JF-Expert Member
- Nov 5, 2008
- 4,776
- 2,389
Mchungaji kweli una roho ngumu.
Rev Kishoka ndio kundi lile la wachungaji wa njia iendayo kuzimu, prohets of Doom,Vibwetere-wasikilize na uaangamia nao.
Mchungaji kweli una roho ngumu.
Mairo,
Je mnajua mchakato mzima wa uzabuni wa Serikali ulivyofanyika? Ukisoma hii taarifa, hakuna chochote kigeni ambacho ni cha kustaajabisha au usema kukiukwa kwa taratibu.
Suala la umeme ambalo lilileta Richmond lilitokana na kuhitajika kwa umeme wa dharura. Serikali kwa kupitia IMF/WB walikubaliana kuwa kwa kuwa hii ni emergency, zile protocal za ku-float tender kupitia zabuni na kadhalika ziachwe na kufanyike hiyo GNT.
Waziri Mkuu alipewa jukumu hili na Rasi na hakujichukulia uamuzi binafsi.
Kama mnakumbuka Kikwete alijitapa na kusema Richmond walipewa mkataba kutokana na kuwa na fees ndogo kuliko wengine, na ndipo tukahoji je mliangalia uwezo, lakini Serikali haikujibu.
Ukisoma hii habari, unaona ni mtiririko wa utekelezaji wa maamuzi ya Serikali na hakuna lolote lile.
Tena mbaya kuna TAHADHARI kijana wetu Eddo ametoa kuwa ikidhihirika yanayosemwa ni kweli, basi mkataba usitishwe na zaidi akasema itumike ile mbinu ya kutumia Letter of Credit kuwalipa hawa jamaa na si vingine!
Sasa kama mnajua L/C zinavyofanya kazi, mngejua kuwa Richmond walipaswa kuleta mitambo kwanza kabla ya kulipwa na kama wangeshindwa kuleta mitambo, wasingelipwa na mkataba ungekaa mguu pande!
Swali ni kwa nini Msabaha alikwenda kwa Meghji na Kikwete akiomba jama wapewe advance?
Ukisoma matendo ya Lowassa, hayana tofauti na ya Mramba au Yona ambao leo wanashitakiwa eti kwa uzembe ilhali kila walichokifanya kina Yona na Mramba kilikuwa na baraka za Serikali na kuchapwa kama agizo katika gazeti la Serikali.
Suala la kujiuliza tuhuma hizi za kusema alishiriki, je alishiriki kuhujumu au alishiriki kiutendaji kama alivyopewa jukumu hilo la kuhakikisha tunapata umeme wa haraka?
Mbona gazeti hili halichapi au kueleza jinsi Lowassa alivyokimbia Ikulu na kumwambia Rais wasitishe mkataba na Rais akakataa akasema anaogopa kesi London na tuendelee na mkataba ilhali ilishoaonekana kuwa Rochmond hawana uwezo?
kwanini alifikia kufanya kosa? (ndio akamueleza Mkulu) kwanini hakumshauri raisi toka mwanzo njia bora ya kufuatilia suala hili?Wana JF,
Tokana na maada hii inaonesha wazi kwamba Lowasa hana kosa na alijiuzulu ili kuepusha mengi na makubwa zaidi.
Alipogundua kosa alimpa mkulu taarifa ili mkataba usitishwe, lakini mkulu alikataa kwa kuogopa kesi. Nani wa kulaumiwa kati ya hawa wawili?.
Suala la kupatikana kwa umeme lilikuwa ni emmergency mpaka World bank na IMF waliona umuhimu huo na kukubaliana nalo ndiyo maana halikupata nafasi ya ku-flotishwa kwenye tenders kama ilivyo kawaida.
Alichofanya Lowasa ni kuona umeme unapatika kwa haraka na kwa gharama ndogo, ndiyo maana akawa anataka suala hilo liendeshwe haraka haraka. Yeye aliichagua Richmond kupewa kazi hiyo baada ya kupitia makabrasha mbali mbali mezani kwake yaliyoletwa na watendaji wake ambao ndiyo waliyoichagua na kuipendekeza Richmond kwa kigezo cha bei ndogo.
Kamati ya Mwakyembe kama ingelimuita Lowasa ili kupata maelezo kamili bila shaka wangeelewa kwanini Lowasa alifanya alichokifanya katika sakata zima la Richmond.
Lowasa ameonewa, hakupewa nafasi ya kujieleza. Katika hili suala Lowasa hana kosa. Mwakyembe na kamati yake wanatakiwa kuwa wakweli na bila kuwa na woga wowote, watupe ukweli na undani wa tatizo hili.
Lowasa ni kiongozi shupavu, asiye na woga wala haya, mwenye msimamo madhubuti, mfuatiliaji mzuri na mwenye uwezo wa kupambanua masula kiundani.
Tanzania tunahitaji kutumia nguvu..
Nguvu na uwezo uliotumika kumtoa Nduli IDD amin DADAA ndio vitumike ktk kuwatoa hawa nyoka wenye sumu kali katika maendeleo ya watanzania.
...hakuna kati ya hao wawili anaye stahili lawama mkuu,ni SISI tulio wengi ndo wakujilaumu.Wana JF,
Tokana na maada hii inaonesha wazi kwamba Lowasa hana kosa na alijiuzulu ili kuepusha mengi na makubwa zaidi.
Alipogundua kosa alimpa mkulu taarifa ili mkataba usitishwe, lakini mkulu alikataa kwa kuogopa kesi. Nani wa kulaumiwa kati ya hawa wawili?.
Mkuu unatushangaza sana.World Bank na IMF ni nani hapa nchini?
Wenye nchi ndo thithi wenyewe, wasikilize hao jamaa at your own peril.
Mara kadhaa WB na IMF wamejulikana kuwa kichaka au a front for big multinational businesses.
Wanabadilika kama kinyonga hao,hawatakuja kumtetea sasa mzee EL.
EL Kujitetea or not, ukikamatwa na fundo la nyama mdomoni na ukalitema kabla ya kulimeza hakuondoi dhamira iliyokuwepo ya kuiba , mbaya zaidi kuiibia jamii ya Watanzania masikini waliokudhamini na kukuamini katika uongozi.
Mairo,
Je mnajua mchakato mzima wa uzabuni wa Serikali ulivyofanyika? Ukisoma hii taarifa, hakuna chochote kigeni ambacho ni cha kustaajabisha au usema kukiukwa kwa taratibu.
Suala la umeme ambalo lilileta Richmond lilitokana na kuhitajika kwa umeme wa dharura. Serikali kwa kupitia IMF/WB walikubaliana kuwa kwa kuwa hii ni emergency, zile protocal za ku-float tender kupitia zabuni na kadhalika ziachwe na kufanyike hiyo GNT.
Waziri Mkuu alipewa jukumu hili na Rasi na hakujichukulia uamuzi binafsi.
Kama mnakumbuka Kikwete alijitapa na kusema Richmond walipewa mkataba kutokana na kuwa na fees ndogo kuliko wengine, na ndipo tukahoji je mliangalia uwezo, lakini Serikali haikujibu.
Ukisoma hii habari, unaona ni mtiririko wa utekelezaji wa maamuzi ya Serikali na hakuna lolote lile.
Tena mbaya kuna TAHADHARI kijana wetu Eddo ametoa kuwa ikidhihirika yanayosemwa ni kweli, basi mkataba usitishwe na zaidi akasema itumike ile mbinu ya kutumia Letter of Credit kuwalipa hawa jamaa na si vingine!
Sasa kama mnajua L/C zinavyofanya kazi, mngejua kuwa Richmond walipaswa kuleta mitambo kwanza kabla ya kulipwa na kama wangeshindwa kuleta mitambo, wasingelipwa na mkataba ungekaa mguu pande!
Swali ni kwa nini Msabaha alikwenda kwa Meghji na Kikwete akiomba jama wapewe advance?
Ukisoma matendo ya Lowassa, hayana tofauti na ya Mramba au Yona ambao leo wanashitakiwa eti kwa uzembe ilhali kila walichokifanya kina Yona na Mramba kilikuwa na baraka za Serikali na kuchapwa kama agizo katika gazeti la Serikali.
Suala la kujiuliza tuhuma hizi za kusema alishiriki, je alishiriki kuhujumu au alishiriki kiutendaji kama alivyopewa jukumu hilo la kuhakikisha tunapata umeme wa haraka?
Mbona gazeti hili halichapi au kueleza jinsi Lowassa alivyokimbia Ikulu na kumwambia Rais wasitishe mkataba na Rais akakataa akasema anaogopa kesi London na tuendelee na mkataba ilhali ilishoaonekana kuwa Rochmond hawana uwezo?
Ukiwa hujui taratibu za manunuzi na due deligence utajibu kama ulivyo jibu, lakini ukiwa unajua utapingana na majibu ya lowasa.Mchungaji
Nakubaliana na reasoning yako.. logically ni sahihi kabisa kwa kuchangia zaidi labda tujibu maswali yafuatayo, sio kwa kumsafisha EL Lakini tu kuhakikisha haki inatendeka.
Nipashe wanaonyesha kusisitiza kuwa ofisi ya waziri mkuu ilihusika kila hatua: Hii sio ajabu kwa sababu ya unyeti wa suala lenyewe yani nchi iko gizani ni wazi ungetegemea waziri mkuu afuatilie kwa karibu, kama alivyosema mwenyewe kwenye barua anataka repoti kila siku bila kukosa- Hapo hana kosa kufuatiliwa kwa karibu ni wajibu wa Waziri mkuu na pia ni utekelezaji wa maagizo ya Rais kuhakikisha umeme unapatikana. Sasa angefuatilia nani kama sio Waziri mkuu.
Kukiukwa kwa taratibu za tenda: Hili pia lilisababishwa na unyeti wa suala lenyewe na sio lazima iwe ni ufisadi. na kubwa hapa ni kwamba IMF/Worl bank walijua,yaani haikuwa siri kuwa watafast track issue nzima ili umeme uje mapema.
Barua za Waziri mkuu: Waziri mkuu katika barua inayotajwa na nipashe anasema wazi Waziri Msabaha afuatilie na kama kuna mashaka basi atoe taarifa ili hatua zichukuliwe mara moja (nahisi ni pamoja na kuvunja mkataba ikibidi). kama ni kweli JK alikataa kwa kuogopa kesi kama mchungaji anavyosema mimi sijui, lakini hapa kwa barua ile ya kwenda kwa Msabaha kutoka kwa Waziri mkuu , naomba nimclear Lowasa kwa nini aliweka wazi kama kuna utata apewe taarifa hatua zichukuliwe.
Kwa kusema ukweli barua hizi zinamsafisha zaidi Lowasa kuliko kumkandamiza.Inawezekana Lowasa aliwaamini Richmond na wakamtapeli. Kwa hiyo Richmond ametapeli serikali , sasa kama kuibiwa ndio tumeibiwa wote sisi na Lowasa.. kwa hiyo tunaweza kumhukumu LA kwa uzembe wa kutapeliwa na Richmond , kwa kuwaamini Richmond lakini si kwa UFISADI,aliposema anajiuzulu kwa makosa ya kiutendaji nakubaliana nae, kwamba angekuwa makini zaidi asingewaamini RICHMOND kiasi kile.. na uzuri aliposhtuka kwamba sasa hawa jamaa ni wahuni aligeuka na akataka wachukuliwe hatua. katika suala hili kwa kusema ukweli .. ni haraka ndio iliponza.. na kama waswahili wasemavyo Hararka haraka haina baraka. Umakini ulikosekana.
Hatua zilizochukuliwa: Richmond wameshtakiwa mahakamani, na kama Gire sio mmiliki cha msingi abanwe ataje wamiliki .. vinginevyo jamani itakuwa ni kumwonea Waziri mkuu mstaaafu .. bila ushahidi.. tuweke jazba pembeni na tureason logically bila jazba.
Kosa la Lowasa katika sakata hili: kwa maoni yangu Lowasa alikosea kureact kwa jazba mara baada ya Mwakyembe kusoma report. Kuzira uwaziri mkuu haukuwa uamuzi kwa busara. Angeweza kuelezea ilivyokuwa akaleta na barua alizoandika na kueleza kwa nini aliamua kulivalia njuga suala hili kama alivyokuwa akifanya kwa masuala mengine na kwamba ile ni staili yake ya utendaji na kwamba waheshimiwa wabunge wasiwe na shaka ya yeye kuhusika kwa karibu kwani alikuwa akitekeleza majukumu ya kikazi kama alivyoagizwa na Raisi, kisha angeliachia bunge liamue. Alikosea kuleta jaza na kujiweka kwenye Victim position na yeye kuanza kublame na kucomplain... badala ya kuweka facts mezani na kuacha wabunge wachambue. Ninaamini bunge lingegawanyika na labda kumsamehe au kumwajibisha kwa uzembe na kisha kuigiza serikali imkamate mmiliki wa Richmond achukule hatua kwa kutapeli .. Lowasa angekuwa bado Waziri mkuu hadi leo ... Hasira hasara.. naomba tujadili kwa hoja tafadhali bila jazba.. kwani ukiwa na jazba uwezo wa kureason vitu unapungua na unaanza kuapply logical falacies kibao.. mwenye ushahidi na mwazo tofauti tuendelee kujadili....Na kwa taarifa mimi sio fisadi wala mwanamtandao ni mchambuzi tu wa mambo.. manake watu wengine wanaweza kuja na majibu mafupi na kusema .. ahah wale wale mafisadi hao ... mmmmmh hapana leta hoja mezani.. nawakilisha.
Aliyeandika makala hii akitegemea itaonesha ubaya wa EL kushiriki mchakato wa Rdc amechemsha. Makala inaonesha EL akiwa on top of his game. Ndiyo tatizo la kupigana vita wasiyojua adui ni nani. Oh well.
Lole wa Gwakisa,
Serikali ilibidi iombe pesa kwa wahisani kuhusiana na suala hili la umeme wa dharura. Pesa ambazo tulisamehewa kulipia madeni na IMF/WB ndio tulizoruhusiwa kuzitumia kuingia mkataba huu.
Kwa upande mmoja, kwa kuwa hiyo psa ilishapangiwa matumizi, kilichofanyika Serikalini ni kile cha mazoea cha kutokujali tena alimradi fedha hii si yetu ni ya mhisani.
IMF/WB walisema badala ya sisi kulipa riba na mkopo, hiyo pesa tuipeleke kwenye umeme wa dharura!
Sasa kama unadai IMF/WB ni nani, mbona huulizi kuhusu zile sera za ERP, Ubinafsishaji na nyingine nyingi ambazo IMF/WB na donor countries wameilazimisha Serikali yetu ifuate wanachotaka?
Je unafikiri Mkapa kutamba sisi kusamehewa madeni Paris Club ili kuwa ni kutokana na Good Governance au kuongezeka uzalishaji? Jibu ni nope, nil, zilch big no na hapana.
Jibu la sisi kusamehewa madeni na Paris Club wakati wa Mkapa ni kuuzwa kwa NMB, Sheria mpya ya madini 1998, kubinafsishwa holela kwa mashirika na kuuzwa kwa bei chee huku tukitii amri za wakubwa.
Kama tulikuwa na ujasiri na uzalendo wa kukataa kushinikizwa na IMF/WB kama tulivyofanya wakati wa IPTL, tusingeuza basi hayo mashirika yetu ambayo mengine yalikuwa hayana matatizo yeyote!
Mkuu wangu kila siku unakuja na mambo jambo..Mairo,
Je mnajua mchakato mzima wa uzabuni wa Serikali ulivyofanyika? Ukisoma hii taarifa, hakuna chochote kigeni ambacho ni cha kustaajabisha au usema kukiukwa kwa taratibu.
Suala la umeme ambalo lilileta Richmond lilitokana na kuhitajika kwa umeme wa dharura. Serikali kwa kupitia IMF/WB walikubaliana kuwa kwa kuwa hii ni emergency, zile protocal za ku-float tender kupitia zabuni na kadhalika ziachwe na kufanyike hiyo GNT.
Waziri Mkuu alipewa jukumu hili na Rasi na hakujichukulia uamuzi binafsi.
Kama mnakumbuka Kikwete alijitapa na kusema Richmond walipewa mkataba kutokana na kuwa na fees ndogo kuliko wengine, na ndipo tukahoji je mliangalia uwezo, lakini Serikali haikujibu.
Ukisoma hii habari, unaona ni mtiririko wa utekelezaji wa maamuzi ya Serikali na hakuna lolote lile.
Tena mbaya kuna TAHADHARI kijana wetu Eddo ametoa kuwa ikidhihirika yanayosemwa ni kweli, basi mkataba usitishwe na zaidi akasema itumike ile mbinu ya kutumia Letter of Credit kuwalipa hawa jamaa na si vingine!
Sasa kama mnajua L/C zinavyofanya kazi, mngejua kuwa Richmond walipaswa kuleta mitambo kwanza kabla ya kulipwa na kama wangeshindwa kuleta mitambo, wasingelipwa na mkataba ungekaa mguu pande!
Swali ni kwa nini Msabaha alikwenda kwa Meghji na Kikwete akiomba jama wapewe advance?
Ukisoma matendo ya Lowassa, hayana tofauti na ya Mramba au Yona ambao leo wanashitakiwa eti kwa uzembe ilhali kila walichokifanya kina Yona na Mramba kilikuwa na baraka za Serikali na kuchapwa kama agizo katika gazeti la Serikali.
Suala la kujiuliza tuhuma hizi za kusema alishiriki, je alishiriki kuhujumu au alishiriki kiutendaji kama alivyopewa jukumu hilo la kuhakikisha tunapata umeme wa haraka?
Mbona gazeti hili halichapi au kueleza jinsi Lowassa alivyokimbia Ikulu na kumwambia Rais wasitishe mkataba na Rais akakataa akasema anaogopa kesi London na tuendelee na mkataba ilhali ilishoaonekana kuwa Rochmond hawana uwezo?
Mairo,
Je mnajua mchakato mzima wa uzabuni wa Serikali ulivyofanyika? Ukisoma hii taarifa, hakuna chochote kigeni ambacho ni cha kustaajabisha au usema kukiukwa kwa taratibu.
Suala la umeme ambalo lilileta Richmond lilitokana na kuhitajika kwa umeme wa dharura. Serikali kwa kupitia IMF/WB walikubaliana kuwa kwa kuwa hii ni emergency, zile protocal za ku-float tender kupitia zabuni na kadhalika ziachwe na kufanyike hiyo GNT.
Waziri Mkuu alipewa jukumu hili na Rasi na hakujichukulia uamuzi binafsi.
Kama mnakumbuka Kikwete alijitapa na kusema Richmond walipewa mkataba kutokana na kuwa na fees ndogo kuliko wengine, na ndipo tukahoji je mliangalia uwezo, lakini Serikali haikujibu.
Ukisoma hii habari, unaona ni mtiririko wa utekelezaji wa maamuzi ya Serikali na hakuna lolote lile.
Tena mbaya kuna TAHADHARI kijana wetu Eddo ametoa kuwa ikidhihirika yanayosemwa ni kweli, basi mkataba usitishwe na zaidi akasema itumike ile mbinu ya kutumia Letter of Credit kuwalipa hawa jamaa na si vingine!
Sasa kama mnajua L/C zinavyofanya kazi, mngejua kuwa Richmond walipaswa kuleta mitambo kwanza kabla ya kulipwa na kama wangeshindwa kuleta mitambo, wasingelipwa na mkataba ungekaa mguu pande!
Swali ni kwa nini Msabaha alikwenda kwa Meghji na Kikwete akiomba jama wapewe advance?
Ukisoma matendo ya Lowassa, hayana tofauti na ya Mramba au Yona ambao leo wanashitakiwa eti kwa uzembe ilhali kila walichokifanya kina Yona na Mramba kilikuwa na baraka za Serikali na kuchapwa kama agizo katika gazeti la Serikali.
Suala la kujiuliza tuhuma hizi za kusema alishiriki, je alishiriki kuhujumu au alishiriki kiutendaji kama alivyopewa jukumu hilo la kuhakikisha tunapata umeme wa haraka?
Mbona gazeti hili halichapi au kueleza jinsi Lowassa alivyokimbia Ikulu na kumwambia Rais wasitishe mkataba na Rais akakataa akasema anaogopa kesi London na tuendelee na mkataba ilhali ilishoaonekana kuwa Rochmond hawana uwezo?
Sidhani kama Lowasa atakuwa na Uso wa kukimbilia Ikulu, Lowasa ni la kuvunda halisikii Udi wala Ubani.Rev.Kishoka heshima mbele,
Ninaona hoja ya msingi hapa ambayo Mh.EL ataitumia kujisafisha.unless kama ni yeye aliyetoa maagizo ya maandishi kwa Mh.Msabaha kufukuzia advance Hazina tofauti na maelekezo yake mwenyewe ya awali ya kufungua Letter of Credit (LC).
Mpaka kwenye hatua ya kuagiza ifunguliwe LC naona Mh.Lowassa alikuwa sahihi sana,na kwa mazingira ya dharura ilikuwa ni sahihi kuwanyang'anya kazi TANESCO waliokuwa wanasuasua kufanya maamuzi.
Mhh! Nahisi EL ataponyoka kwenye hili la Richmond na hapo ndipo mbio zake za ikulu zitakapochukua kasi ya ajabu.Na hapo ndipo akina yakhe waliokuwa wanampiga vita watakapotafuta nchi ya kwenda kujificha.
Let's wait and see,sinema hii itakavyomalizikia. Je,Starring EL atauawa?