kwa kutokea hizo scandal ambazo zingine bado tunazifuatilia, hai-halalishi, lowasa kufanya alivyo fanya, na tena alivyo ........., ameanza kufanya madudu from day one, mkapa yeye madudu kafanya karibu ya second term , baada ya kuwadanganya watanzania kwa baadhi ya mazuri aliyo fanya, alhaji pia alifanya madudu second term, sasa wenzetu hawa, ili filimbi inalia kipute kianze , nao wanaanza na madudu. na zaidi ya hapo umeme ndio roho ya nchi, halafu mtu anasema we are right on time, katika ku-take off. etc etc
Pili ndugu yangu nikuulize sasa, kwa sababu watu hawa-heshimu hiyo due deligence ndio kuna halalisha uzuri wa EL. Sasa huo mshahara mnono, wa U-PM, na marupurupu mengine ni yanini. na pensheni ya kustaafu nayo unapewa, rejea warakawa mafao ya viongozi hasa hao wa juu ilikuwa ili wasiingie tamaa na ku-sign mikataba mibovu mibovu, infact hao akina mkapa ipo haja ya ku-reviewe pensheni zao ili kuona kama zinaendana na kazi waliotakiwa kuifanya.
Tatu uelewe hizo kesi zingine zinafuatiliwa , huwezi jua mwaka kesho tukawa na utawala tofauti, ambao utakuwa na uwezo wa kuzi shughulikia hizi tuhuma head on.
Nne ulipokuwa unasoma shule au tulipokuwa tuna soma shule kuna wengine walikuwa wanaiba mitihani, na kufanya juhudi tofauti ili wafaulu, lakini wewe ulikuwa hufanyi hivyo kwa sababu ya uadilifu wako na ulikuwa ukielewa kwamba muda utafika wata kwama, so to lowasa kama wenzie walikuwa wezi/ mafisadi haimanishi na yeye awe hivyo.
Nakuombea kwa Alah/ Mwenyezi Mungu/ Yehova/ God/Jah akupe nguvu na hekima zaidi ili utupe shule na waraka zako.
August,
Watu wengi humu kamwe hawatanielewa maana wameweka hisia zao (emotions) kwenye hili suala na hasa kuhusiana na Lowassa kiasi kwamba wanadhani namsafisha!
Suala la Richmond ni la Serikali nzima na Rais ambaye ndio msimamizi mkuu ndiye anayewajibika na si mwingine. Kwa kuwa Lowassa alifanya kazi hii kwa uzembe, ilimpasa Rais amfukuze kazi kama vile Nyerere alivyomuondoa Kawawa au Mwinyi alivyomuondoa Malecela.
Watu wanachokifumbia macho ni utamaduni mbovu na mfumo mbovu wa kiutawala na kiuongozi Tanzania!
Suala la kuingia mkataba mkubwa kama huu, halimhusu Waziri Mkuu pekee, ni mpaka Baraza la Mawaziri kwa kuwa tulikuwa kwenye crisis.
Ukisoma walichoandika Nipashe, unaona kuwa Waziri Mkuu alitaka upsates za kila kitu kila siku, which means alikiwakilisha kwa Rais wake kila siku.
Kuna watu ambao wanataka kuonyesha kuwa Kikwete hakuhusika, lakini nawaambia rejeeni interview ya Kikwete ya mwanzo mwa 2007 aliyofanya na NIpashe hao hao na uchangue alichokisema, ndipo utajua ni vipi mchakato mzima ulifanyika.
Lowassa alifanya makosa ya kiutendaji alipopewa jukumu la kuongoza mchalato huu wa kununua Umeme. Na hilo ndilo nililolisema awali kuwa ni makosa ya kiutendaji ambayo kila mtu anafanya.
Lakini watu wanafikiri aliiba, au kajitajirisha. Aliyetajirika na Richmond si Lowass ,bali ni Dowans na wote tunajua ni nani aliyeishikilia Dowans.
Mimi kusema kuwa Lowassa anatufaa, nimetoa sababu zangu za msingi, nikasema inabidi kuwa na sacrifice na compromise.
Ukisoma hii habari ya Nipashe, utaona kuwa kiuchapa kazi na ufuatiliaji, Lowassa was on top of his game! Na huyo ndiye Lowassa ninayempigia debe, uongozi wa namna hiyo wenye kufuatilia mambo.
Je Lowassa hana makosa? swali ni nani kati yetu hajafanya maamuzi mabovu au mabaya? Kawawa na vijiji vya ujamaa, Sokoine na Vita vya Ulanguzi, Malecela na G55 na OIC, na utitiri kibao.
KUna kitu tulimlaumu Mrema kuhusiana na kukataa kushiriki katika Collective Responsibility.
Suala la Richmond ni Collective Responsibility ya Serikali nzima, regardless ya nani alikuwa akiongoza task force. Kwenye task force alikuwepo Mwanasheria Mkuu, Katibu Mkuu Hazina na Katibu Mkuu NIshati. Hao ndio walikaa chini na kupitia makampuni yote yaliyoleta uzabuni kwa haraka haraka na ndio maana protocal za kawaida ziliachwa.
Je kazi hii ya kufanya uzabuni huu ilifanywa kwa kufuatia Sheria na Kanuni au tulikurupuka ili kujihami kutokana na hali ilivyokuwa mbaya?
Ikulu inatoa amri, wanaofuata wanatekeleza amri/agizo, ufinyu wa kufuata kuona kama tunaifanya kazi hii kwa kanuni unatokea, hujuma inafanyika kutokana na aliyepewa zabuni kuwa ni mbangaizji, mwishowe, mkataba unachukuliwa na yule aliyeutaka awali akapigwa panga na GNT kwa kuwa alihujumu kila kitu kwa makusudi ili aje aununue mkatana kwa bei nafuu.
Sasa kama aliyetuhujumu ni Shemeji ya Rais (inasemekana), alikuwa mweka fedha wa CCM na mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu, halafu tunakimbilia kushupalia kuwa aliytetuibia na kutuhujumu ni timu ya Serikali iliyofanya uzembe, iweje tuanze kusema timu ya Serikali imeiba?
FMES kasema Yona na Mramba walikiuka kitu, swali ni hili, Yona na Mramba walipofanya waliyoyafanya na kuyachapa katika Gazeti la Serikali, Wabunge, Baraza la Mawaziri, AG na watchdogs wengine wote walikuwa wapi kusema hili lirekebishwe?
Je kwenye suala la Richmond, TISS walikuwa wapi wasimshauri Rais directly kuwa hili ni bomu hata kama Lowassa alikwenda kichwa kichwa?
Kama mtasema Rais aliliacha makusudi Lowassa ajitie kitanzi, ambacho ni kitu cha kipuuzi na ni unafiki kuhusu Urafiki wao, je ile hasara ya nchi kukosa umeme wa kutosha ambayo ni kubwa kuliko hata mkataba mzima wa Richmond ni msalaba wa nani? (The actual cost of shortage of power duting this saga was more than the cost of the damn contract with Richmond!)
Okay lets say mkataba wa Buzwagi for that case. Karamagi kaenda London, kunahitajika mabadiliko kwenye mkataba, anayafanya bila kuwasiliana na AG. Yeye yupo hapo Churchil hotel na Rais. Anakuja anadai alifanya hivyo kwa kuwa ana mamlaka kwa mujibu wa Sheria. Kaingia mkataba wa miaka 25! Zitto katoa siri, kwanza Serikali nzima kwa kuwa wanafanya mambo kisiasa, wakatumia turufu ya kichama na kumshushua Zitto.
Mambo yalipoanza kudoda baada ya watu wa JF kubandika mkataba hadharani, Rais anaundia Tume!
Hivyo basi, all fingers will still point back to Head of State, regardless of outcome. It means he is reckless and negligent.