Hivi ndivyo Lowassa alishiriki Richmond | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ndivyo Lowassa alishiriki Richmond

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Makaayamawe, Oct 26, 2009.

 1. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  [​IMG] Nyaraka zaonyesha kila hatua aliweka mikono yake
  [​IMG] Uthibitisho wa kuibeba Richmond watolewa peupe
  [​IMG] Kumbe ndiye aliipora Tanesco kazi ya kusaka mzabuni
  [​IMG] Wizara ya Nishari na Madini ilisubiri maamuzi yake .


  Na Mwandishi wetu
  26th October 2009


  [​IMG]

  Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

  Kilio cha Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa (pichani), bungeni kwamba alidhalilishwa sana kwa kuhusishwa na mkataba tata wa kampuni ya Richmond, si lolote wala chochote baada ya uchunguzi wa kina wa nyaraka uliofanywa na gazeti hili kubaini kwamba alihusika vilivyo katika mchakato mzima wa zabuni hiyo.

  Nyaraka kadhaa ambazo Nipashe imeziona, zimethibitisha si tu ushiriki wa Lowassa katika mchakato huo, bali alikuwa anatoa maelekezo ya nini kifanyike kwa kila hatua.

  Nyaraka hizo zinaonyesha kwamba Waziri wa Nishati na Madini wakati huo, Dk. Ibrahim Msabaha, alibakia kuwa kama karani tu wa kutekeleza maagizo ya Lowassa, kila hatua alikuwa anaamua Lowassa na kuifanya Wizara ya Nishati na Madini kutekeleza kile alichotaka kiongozi huyo aliyejiuzulu Februari mwaka jana huku akilalamika kwamba ameonewa kwa kuzushiwa mambo kuhusu kashfa ya Richmond.

  Akitii maagizo kutoka kwa Waziri Mkuu Lowassa, Dk. Msabaha, naye alimwandikia barua Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Athur Mwakapugi, Juni 21, 2006 akimwagiza atekeleze maagizo wa Waziri Mkuu ya kusaini mkataba na Richmond.

  Kwa kifupi barua hiyo inasomeka hivi
  …“Iagize Tanesco iingie mkataba na kampuni ya Richmond kwa ajili ya umeme wa kukodisha haraka iwezekanavyo. Nakuletea nakala ya kibali kilichotolewa kutoka ofisi ya Mhe. Waziri Mkuu kwa kumbukumbu za Wizara.”

  Kwa mujibu wa uchunguzi wetu, Katibu Mkuu huyo, wakati huo, Arthur Mwakapugi, baada ya kupata maelekezo toka kwa waziri wake, naye alitoa maagizo siku hiyo hiyo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco, Balozi Fulgence Kazaura, akimwagiza kuhakikisha shirika hilo linaingia mkataba na Richmond.

  Maelezo hayo ambayo aliyaandika kwa mkono yalisomeka kwa kifupi...
  “Andaa barua kwa Mwenyekiti wa Tanesco kumuagiza waingie mkataba na Richmond.”

  Taarifa zinaonyesha kuwa baada kampuni ya Richmond Development Company LLC kuingia mkataba na Tanesco Juni 23, 2006 na baada ya siku kusonga mbele bila kuwepo kwa dalili yoyote ya kupatikana kwa umeme wake katika kipindi cha siku 60 kama walivyosema wenyewe, maneno yalianza kuzagaa miongoni mwa wananchi, vyombo vya habari na hata baadhi ya wabunge, hivyo Lowassa akahisi kuwa kazi aliyokuwa ameisimamia kwa nguvu zote amechemsha na hivyo kutoa maelekezo mapya.

  Katika maelekezo hayo, Lowassa kwa barua yake kwenda kwa Waziri Msahaba alisema: “Kama unavyofahamu yapo maneno mengi sana yanasemwa kuhusu uwezo wa kampuni tajwa (yaani Richmond) kuagiza Gas Turbines kama alivyopewa mkataba na Tanesco baada ya kushinda zabuni. Yameandikiwa pia kwenye Gazeti la Thisday la jana (20.09.06).

  “Inawezekana hivi vikawa ni vita vya kibiashara. Lakini kwa sababu ya meneno hayo yanasemwa na watu wengi na tofauti ni vizuri UKAJIRIDHISHA kwamba kampuni hii itaweza kutekeleza kazi hiyo. Kama utaona shaka lolote ni vizuri kuwasiliana na Mwanasheria Mkuu mapema ili tuweze kuchukua hatua zinazopasa mara moja.”

  Aidha, Lowassa akijua kwamba kuna jambo linazidi kuumuka juu ya Richmond, katika barua hiyo ya Septemba 21, 2006 alijipa moyo akisema: “Kwa upande mwingine kwa kuwa malipo yake ni kwa L/C hawezi kupata nafasi ya ‘kuturusha’. Ila unachoweza kufanya ni kuweka utaratibu wa kumfuatilia kwa karibu ili kuhakikisha kwamba analeta ‘turbines’ hizo zenye kiwango na kwa wakati. Napenda kupata taarifa za ufuatiliaji wa suala hili kila siku; bila kukosa.”

  Ushiriki wa Lowassa haukuishia kwenye barua hiyo aliyoandika na kuisaini mwenyewe Septemba 21, 2006 tu; bali
  ushiriki wake mwingine unaonekana katika waraka wa Waziri Msabaha, aliyegeuzwa karani katika mchakato mzima huo, kwenda kwa Mwenyekiti wa bodi ya Tanesco, Balozi Flugence Kazaura.

  Dk. Msabaha anamtaarifu Balozi Kazaura kuwa suala la kushughulikia mashine za umeme wa kukodi limekwisha kushughulikiwa na Waziri Mkuu Lowassa.

  Katika barua hiyo ambayo pia Nipashe ilifanikiwa kuiona ya Aprili 12, 2006 inasema ifuatavyo:

  “Nadhani hatukuelewana vizuri. Suala la kushughulikia gas turbines za kukodisha lilishashughulikiwa na Mhe. Waziri Mkuu, ambaye aliunda Kamati ya wataalam watatu – KM- Hazina, KM Nishati na AG. Nia ni kuliondoa suala zima kwenye mikono ya Menejimenti ya Tanesco ambayo imeshindwa kulishughulikia kwa ufanisi.”

  Kwa barua hiyo, si tu kwamba Dk. Msahaba aliweka wazi msimamo wa Lowassa katika suala zima la ukodishaji wa mitambo hiyo, bali pia alionyesha jinsi ilikuwa imekubalika kuwaweka pembeni Tanesco ambao walikuwa ni wataalam wa mitambo hiyo kuliko mtu mwingine yeyote kwenye masuala ya uzalishaji umeme.

  “Waache Kamati iliyoteuliwa kufanya kazi hiyo kwa kushirikiana na BODI yako na wataalam wa Tanesco kwa kadri watakavyoona inafaa.
  Pasiwe tena na picha kama vile Menejimenti ya Tanesco imerejeshewa kazi hiyo, maana huko kutakuwa ni kukiuka maagizo ya Mhe. Waziri Mkuu,” kwa kauli hiyo ni dhahiri Lowassa alikuwa ndiye anayejua mwelekeo wa kile alichokuwa anakitaka.

  Mikono ya Lowassa katika sakata la Richmond haipo tu kwenye kumwagiza Dk. Msabaha na Kamati ya Makatibu pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, lakini pia inaonekana jinsi alivyobariki mapendekezo ya Timu ya Majadilino ya Serikali (GNT) iliyojadiliana na Richmond.

  Kwa mujibu wa barua nyingine ya Waziri Msabaha ambayo pia Nipashe imefanikiwa kuiona ya Juni 17, 2006 siku sita tu kabla ya mkataba wa Richmond kusainiwa, inaonyesha alivyoelezwa hatua kwa hatua za majadiliano baina ya GNT na Richamond na jinsi utekelezaji wa mkataba utakavyokuwa.

  Katika barua hiyo, Lowassa alielezwa gharama za kuleta mitambo hiyo na mpangilio mzima wa kuileta kwa awamu tatu, kwa kuonyesha alivyokuwa amelipa suala hilo kipaumbele, Juni 21, 2006 Lowassa kupitia kwa Katibu wake, aliyetambulika kama B. Olekuyan, alimtaarifu Katibu wa Waziri wa Nishati na Madini majibu ya bosi wake.

  Majibu yalisema ifuatavyo: “Mheshimwa Waziri Mkuu amekubali mapandekezo na ushauri wa Mheshimiwa Waziri. Tafadhali mjulishe.”


  Kwa kasi ya ajabu, siku hiyo hiyo, Dk. Msabaha akiwa anafanyia kazi majibu ya Lowassa, alimwagiza Katibu Mkuu wake, Arthur Mwakapugi, hatua za kuchukua juu mkataba wa Richmond.

  “Serikali imekubali mapandekezo ya Wizara kuwa Tanesco iagizwe kuingia mkataba wa kuleta Gas Turbines za kukodisha za jumla ya MW 105.6 na kampuni ya Richmond kwa mtiririko uliopendekezwa katika makubaliano kati ya Kampuni ya Richmond ya Marekani na GNT,” ilisema barua hiyo na kuongeza kuwa:
  “Iagize Tanesco iingie mkataba na kampuni hiyo kwa ajili ya umeme wa kukodisha haraka iwezekanavyo. Nakuletea kibali kilichotolewa kutoka kwa Ofisi ya Mhe. Waziri Mkuu kwa kumbukumbu za Wizara.”

  Mwakapugi naye kwa kasi kama ya Waziri Msabaha, siku hiyo hiyo, aliagiza Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco aagize Tanesco waingie mkataba na Richmond. Mkataba ambao kwa mujibu wa kumbukumbu za Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mchakato wa mkataba wa Richmond, ulisainiwa usiku kwa haraka hizo hizo siku mbili baadaye.


  Mikono ya Lowassa pia ilionekana kwenye mkataba wa Richmond kama waraka wa ndani wa Waziri Msabaha kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara akieleza kuwa Waziri Mkuu ameamrisha Richmond wapewe dili nyingine ya kuzalisha megawati 40 za umeme.

  Waraka huo wa Julai 13, 2006 baada ya kusainiwa kwa mkataba wa Richmond na Tanesco, unasema:
  “Nimezungumza tena na Mheshimiwa Waziri Mkuu leo juu ya bei ya mitambo ya Aggreko. Msimamo ni uleule niliokueleza awali na ameagiza tuulize Richmond kama anaweza kutoa 40 MW kwa bei isiyozidi ile ile ya 4.99 cents per kwh na kama tunaweza kuipata basi achukuliwe Richmond.”

  Kwa maelekezo ya Lowassa, Msabaha katika barua hiyo kwa Katibu Mkuu alisema:
  “Nimempigia simu Mohamed Gire wa kampuni ya Richmond juu ya upatikanaji wa hizo MW 40. Gire amekubali kuwa anaweza kutoa MW 40 za ziada ifikapo Septemba na kwa bei hiyo ya USD cents 4.99 @ kwh. Amesema hatahitaji majadiliano mapya. Inatosha kama ataandikiwa barua tu ya nyongeza MW 40.”

  Kwa mtiririko mzima wa kusakwa kwa Richmond, hakuna hata hatua moja ambayo Lowassa anaweza kudai hakuhusika katika mchakato mzima, na kama vile Dk. Msabaha alikuwa anajua kitakachotokea wakati wote alionyesha kwamba alikuwa akifanyia kazi maelekezo ya bosi wake, yaani Lowassa.

  Kuna habari kwamba wakati Serikali itakapowasilisha ripoti ya utekelezaji wa maazimo ya Bunge juu ya Richmond, hoja ya kutaka kusafishwa kwa Lowassa itaibuka ikilenga kuionyesha kwamba alionewa na Kamati Teule ya Bunge ya kuchunguza mchakato wa mkataba wa Richmond na Tanesco.


  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Lowassa sasa aende mahakamani kama NIPASHE wanamzushia.
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280

  Mkuu Makaa ya mawe heshima mbele.

  Lowasa si mjinga kiasi hicho mkuu wangu hawezi kwenda mahakamani kwasababu anajua huko ataumbuka zaidi.

  Makaa ya mawe kwani wewe ulikuwa hujui Lowasa alishiriki kila hatua ya kuibeba Richard Monduli ?.Hii kitu kila mtu anajua Naare alipiga dili kwa faida yake & Co.
   
 4. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kila kitu bongo kinawezekana!
   
 5. kilema

  kilema Member

  #5
  Oct 26, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Inachekesha halafu inauma. Suala la Umeme gumu labda twende kwa mganga kupata pafect information. Inanishangaza juzi rais alitoa agizo mitambo ya IPTL iwashwe hata iki haijaisha tayari mafuta ya kuiendesha yamekwisha wasili! du kasi ya ajabu! mambo serikali ingefanya kazi kwa kasi hivi Tanzania tunngekuwa Mbali lakini hmm PPRA imefuatwa? yasije yakaanza tena ya Richmond.
   
 6. W

  WildCard JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Nipashe wamenusa taarifa ya serikali Bungeni wiki hii nini?
   
 7. M

  Magezi JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hivi lowasa, chenge, JK, mkapa, n.k. wana damu kama yetu au?? Nafikiri wao hawata kufa eti??
   
 8. D

  Deo JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 1,191
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kazi njema sana
   
 9. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2009
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Siongei kitu mimi mtoto wa mchungaji ninachosubiri tu ni maombi ya nchi watu woote wanaohusika katika suala hili wale hukumu kwani nimesoma na kuelewa ushiriki wa mkuu mwanzo mwisho mmmhhhh!!! thithemi kitu god amshukie kama Dit.. Asante mkuu
   
 10. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mkuu makaa ya mawe kazi nzuri. Tusibiri ripoti itakavyopokelewa na kufanyiwa kazi; I am sure EL atasafishwa. Miafrika ndiyo tulivyo tu.
   
 11. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Kwa wanaJF waliofuatilia issue hii toka mwanzo, the question is not whether he was involved or not, the question is whether legali steps will be taken against him and others who were involved. Current power outages are reminder that we still have left overs to deal with before going any further.
  Kama tutaendelea na ujinga ule ule wa kusema hatuwezi kuwashughulikia tutaendelea kuprove ujinga. Bunge na kama yake wameplay a role, bahati mbaya wao sio polisi na mahakama, lket us see what the executive branch of government says.
   
 12. M

  Mundu JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2009
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Hii IPTL nayo ni dili la wakubwa tu, tusubiri... mana kila kitu nacho kinakwenda kwa kasi ya ajabu!

  wa tz tumekuwa na kugeuzwa mtaji sasa na wa tz wenzetu hawa tuliowapa uwezo wa kutuongoza! Sijui nyaraka za Ngeleja kwenda IPTL nazo zinasomekaje!!?
   
 13. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Mhh siasa tamu bwana halafu jamaa bado anataka kugombea urahisi naye anakambi ndani ya CCM, hatari!
  ataendaje mahakamani kwani amesahau ile ya jengo la vijana la CCM makao makuu alivyokimbia. na mpaka leo hajaongea lolote na akashindwa kumpeleka kubenea mahakamani!!
   
 14. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mkuu Mgongo heshima mbele,
  Ni kweli kabisa akienda mahakamani ataumbuka. Swali ni kuwa je atakaa kimya baada ya kuwekwa wazi kiasi hiki na Mengi? Maana ingawa tulikuwa tunajua juu ya ushiriki wake, hajawahi kuropokewa hadharani na magazeti.

  Akikaa kimya atakuwa amekubali ushiriki, akijitosa kujitetea atakuwa amejipalia makaa, kazi kwake.
   
 15. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #15
  Oct 26, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Inawezekana wamezinusa. Lakini umemsikia na SAS naye kaipiga kijembe sirikali ya JK juu ya Richmonduli?
   
 16. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #16
  Oct 26, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,165
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
   
 17. M

  Mundu JF-Expert Member

  #17
  Oct 26, 2009
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Makaayamawe,

  Mengi hausiki na hiyo habari. Yeye ni mmiliki tu wa kile chombo na si mhariri na wala mwandishi wa habari.
   
 18. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #18
  Oct 26, 2009
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Tujiandae, kesha kwenda hija kujitakasa. Anautaka urais kwa udi na uvumba
   
 19. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #19
  Oct 26, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wakina Mwakyembe katika ripoti yao kwenye Bunge hawakumtuhumu moja kwa moja EL bali walisema kutokana na mambo yalivyoenda wanamwachia Waziri Mkuu ajifikirie katika suala zima. EL aljua kwamba Mwakyembe na timu yake waliona mengi na ili kuepuka aibu akajifikiria na kesho yake akabwaga manyanga! Jitihada za kumsafisha EL upya ndio sasa zinaibua ushaidi mpya dhidi yake. Tutasikia mengi. Stay tuned.
   
 20. Mairo

  Mairo Member

  #20
  Oct 26, 2009
  Joined: Jun 4, 2009
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu Rev Upo? I would like to read your comments on this!
   
Loading...