Mkuu Rev Upo? I would like to read your comments on this!
Mairo,
Je mnajua mchakato mzima wa uzabuni wa Serikali ulivyofanyika? Ukisoma hii taarifa, hakuna chochote kigeni ambacho ni cha kustaajabisha au usema kukiukwa kwa taratibu.
Suala la umeme ambalo lilileta Richmond lilitokana na kuhitajika kwa umeme wa dharura. Serikali kwa kupitia IMF/WB walikubaliana kuwa kwa kuwa hii ni emergency, zile protocal za ku-float tender kupitia zabuni na kadhalika ziachwe na kufanyike hiyo GNT.
Waziri Mkuu alipewa jukumu hili na Rasi na hakujichukulia uamuzi binafsi.
Kama mnakumbuka Kikwete alijitapa na kusema Richmond walipewa mkataba kutokana na kuwa na fees ndogo kuliko wengine, na ndipo tukahoji je mliangalia uwezo, lakini Serikali haikujibu.
Ukisoma hii habari, unaona ni mtiririko wa utekelezaji wa maamuzi ya Serikali na hakuna lolote lile.
Tena mbaya kuna TAHADHARI kijana wetu Eddo ametoa kuwa ikidhihirika yanayosemwa ni kweli, basi mkataba usitishwe na zaidi akasema itumike ile mbinu ya kutumia Letter of Credit kuwalipa hawa jamaa na si vingine!
Sasa kama mnajua L/C zinavyofanya kazi, mngejua kuwa Richmond walipaswa kuleta mitambo kwanza kabla ya kulipwa na kama wangeshindwa kuleta mitambo, wasingelipwa na mkataba ungekaa mguu pande!
Swali ni kwa nini Msabaha alikwenda kwa Meghji na Kikwete akiomba jama wapewe advance?
Ukisoma matendo ya Lowassa, hayana tofauti na ya Mramba au Yona ambao leo wanashitakiwa eti kwa uzembe ilhali kila walichokifanya kina Yona na Mramba kilikuwa na baraka za Serikali na kuchapwa kama agizo katika gazeti la Serikali.
Suala la kujiuliza tuhuma hizi za kusema alishiriki, je alishiriki kuhujumu au alishiriki kiutendaji kama alivyopewa jukumu hilo la kuhakikisha tunapata umeme wa haraka?
Mbona gazeti hili halichapi au kueleza jinsi Lowassa alivyokimbia Ikulu na kumwambia Rais wasitishe mkataba na Rais akakataa akasema anaogopa kesi London na tuendelee na mkataba ilhali ilishoaonekana kuwa Rochmond hawana uwezo?