Hivi mwanaume kununua vitenge ni kosa

Hivi mwanaume kununua vitenge ni kosa

ligera

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2014
Posts
2,646
Reaction score
1,173
Yupo kijana mmoja mtaani kwetu huku kijijini kwetu ambaye kila inapofika msimu wa mauzo wa mazao hununua vitenge vingi na kuweka ndani.watu wanachoshangaa ni kwamba kijana mwenyewe hajaoa vitenge vyote hivyo ni vya nini,umeibuka mzozo mkubwa kwamba huyu kijana anatembea na wake za watu imefikia hatua vijana wa hapa mtaani wanamtishia kumhamisha mtaa,wana jf tujadiliane
 
Kama anaenda kuuza kijiji jirani?

Acheni njaa vijana.

Mtamuhamisha akawe bilionea.
 
Umeshaona wake za watu wanavaa vitenge kwa wingi sana huko Kijijini kwenu?

Hapa unataka tujaadili nini sasa??
 
Halafu samahani, Kijiji chenu kina Mtaa?
 
Yupo kijana mmoja mtaani kwetu huku kijijini kwetu ambaye kila inapofika msimu wa mauzo wa mazao hununua vitenge vingi na kuweka ndani.watu wanachoshangaa ni kwamba kijana mwenyewe hajaoa vitenge vyote hivyo ni vya nini,umeibuka mzozo mkubwa kwamba huyu kijana anatembea na wake za watu imefikia hatua vijana wa hapa mtaani wanamtishia kumhamisha mtaa,wana jf tujadiliane

Sasa yeye kanunua vitenge halafu sisi tujadiliane nini,jinsi ya kwenda kumnyang'anya au?
 
he he he he, kwa kijijini hii inaweza kuwa ishu.
 
Umbea kazi! Sasa hao wake za watu anawagongea wapi mliposhindwa kufumania, hadi mfumanie matumizi ya vitenge? Ningekuwa mimi ningekuwa nanunua kitenge na pakiti 2 za condom
 
ha ha ha, huo ni uchokozi wa kiroho.

Afu unazifungua?

Umbea kazi! Sasa hao wake za watu anawagongea wapi mliposhindwa kufumania, hadi mfumanie matumizi ya vitenge? Ningekuwa mimi ningekuwa nanunua kitenge na pakiti 2 za condom
 
Kwa hiyo mtu kununua kitenge ni uzinzi????!!
Kama nyie hamtunzi wake zenu ye anajiandaa kumtunza wake!!!!!

Sasa jiandaeni baada ya kuoa na wake zenu kumuona mkewe "akishaini" ndio mtakaziwa kweli...watahamia airtel!!!!!!!

Muanze kutunza wake zenu au msubiri waje wayaone maisha katika mwanga bora....kuoa si kazi kazi kutunza mke! !!!!!!!
 
Umbea kazi! Sasa hao wake za watu anawagongea wapi mliposhindwa kufumania, hadi mfumanie matumizi ya vitenge? Ningekuwa mimi ningekuwa nanunua kitenge na pakiti 2 za condom


Hawana utaratibu wa ndomu huko ndio maana wanajua jamaa "anachoma mishkaki tu".
 
Anaandaa kwaajili ya mke atakayemuoa au anampa mama yake
 
Vijijini hata maji ya chupa ukinywa unatishia ndoa za watu
 
Back
Top Bottom