Hivi mwanaume anaacha au anaachwa? Mwanaume kweli unaanzaje kulia kwa kuachwa?

2019

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
2,982
4,457
Kwanza kabisa tuwasikitikie vijana wote wanaodai ni wanaume huku wakilia kuachwa.

Inavyojulikana mwanaume haachwi bali anaacha au wanaachana na mke wake. Kwanini mwanaume hawezi kuachwa? Kwa sababu yeye ndio kichwa cha familia, uliwahi kuona tela likiacha kichwa nyuma? Hapana.

Tafsiri ya vijana wanaodai ni wanaume wanaolia lia kudai kuachwa maana yake yeye ndio alikuwa tegemezi, yani mkewe ndio alikuwa analisha familia, analipa kodi. N.K hapo lazma ulie kwa sababu huna option ingine sababu hujiwezi.

Mwanaume wa kweli hawezi kulia kama mkewe ataondoka nyumbani bali atasonga mbele sababu wanawake wenye shida ya kuolewa ni wengi kuliko wanaume wanaotaka kuoa. Sa unaanzaje kulia, kulalamika? Sokoni kuna mikato yote, kuna aina zote, umekosa kabisa? Ni aibu kwa vijana.

1624269083248.png
 
Kwanza kabisa tuwasikitikie vijana wote wanaodai ni wanaume huku wakilia kuachwa.

wanaotaka kuoa. Sa unaanzaje kulia, kulalamika? Sokoni kuna mikato yote,kuna aina zote,umekosa kabisa? Ni aibu kwa vijana.
Mwanaume haachwi, ila inauma sana unapogundua kuwa mpenzi wako ana mpenzi mwingine, halafu mbaya zaidi wewe uwe decent sana unakuja kugundua kuwa muhuni anakula kichwa, unaumia sana, ukivuta picha ile mikunjo unayomkunja halafu unagundua muhuni naye yumo humo!!!

Ukitafuta majibu huyapati, ndiyo umeachwa hivyo, ukijaribu kumrudisha unaweza lakini kuvumilia maumivu ni ngumu sana, bora uhumie mpaka umalizike na uhanze upya.
 
Mwanaume haachwi, hata kama mwanamke anakuzidi uwezo na cheo, ukiwa vizuri kiakili na ukitembea na chaki, atarudi mwenyewe tu.

Mimi mara yangu ya kwanza kufumaniwa (Red Handed) na demu wangu nlikua na miaka 16, mpaka nafika miaka 19 nlifumaniwa zaidi ya mara 8 au 9. Mademu zangu mpaka nafika umri wa miaka 22 ilibidi wanizoee na wazoeane tu. Sometime mpaka walikua wanapigiana simu "Hivi huyu jamaa umemuona leo, yupo huko? Sim yake toka juzi hapatikani"

Nikisikia mwanaume mwenye age zaidi ya 21, anaumizwa au analialia kisa mapenzi huwa namshangaa sana, yani nakua kama naangalia movie ya kichina bila subtitles.

Ila nikiona mwanaume anakosa usingizi kwasababu ya biashara au mchongo wa hela umekwenda vibaya, namheshimu sana mpambanaji.
 
Mwanaume wa kweli hawezi kulia kama mkewe ataondoka nyumbani bali atasonga mbele sababu wanawake wenye shida ya kuolewa ni wengi kuliko wanaume wanaotaka kuoa. Sa unaanzaje kulia, kulalamika? Sokoni kuna mikato yote,kuna aina zote,umekosa kabisa? Ni aibu kwa vijana.
Omba sana, sali sana yasikukute! Ukishabalehe kwenye ndoa, huwazii wewe, unawawazia future ya Wanao! Unaweza kuhusu kesho ya Watoto wako, mahusiano yanapovunjika wanaoumia ni watoto na sio nyie!

Uwe unawaza mbali kidogo. Inauma, inafikirisha na inatatiza siku wanao wakikuuliza "Baba, kwanini ulimuacha Mama?"
 
Kuacha Ni Kile kitendo cha mmoja Wenu kuvunja bakubaliano yenu muliyojiwekea.

Hivyo yule anaesitisha mahusiano Hayo anahesabika kama Ameacha, na yule Ambae hakuwa tayari mahusiano hayo yavunjike Yeye Anahesabiwa kama Ameachwa Bila kujari muhusika ni mwanamke au mwanaume.

Ndio maana hata kwenye mpira mchezaji akivunja mkataba na timu yake (KUIACHA) moja kwa moja mchezaji huyo itabidi alipe gharama za kimkataba kwa timu husika.

Timu nayo ikimvunjia mkataba mchezaji inabidi imlipe mchezaji huyo haki zake zote kwavile wao ndio wamemuacha.
 
Kumbuka mwanamke hana uwezo wa kuamua aolewe lini,lakini mwanaume unaweza kuamua naona kesho na ikawezekana. Sa kidume unakubalije kuendeshwa kama gari bovu
 
Mwanaume haachwi, hata kama mwanamke anakuzidi uwezo na cheo, ukiwa vizuri kiakili na ukitembea na chaki, atarudi mwenyewe tu.

Mimi mara yangu ya kwanza kufumaniwa (Red Handed) na demu wangu nlikua na miaka 16, mpaka nafika miaka 19 nlifumaniwa zaidi ya mara 8 au 9. Mademu zangu mpaka nafika umri wa miaka 22 ilibidi wanizoee na wazoeane tu. Sometime mpaka walikua wanapigiana simu "Hivi huyu jamaa umemuona leo, yupo huko? Sim yake toka juzi hapatikani"

Nikisikia mwanaume mwenye age zaidi ya 21, anaumizwa au analialia kisa mapenzi huwa namshangaa sana, yani nakua kama naangalia movie ya kichina bila subtitles.

Ila nikiona mwanaume anakosa usingizi kwasababu ya biashara au mchongo wa hela umekwenda vibaya, namheshimu sana mpambanaji.
great thinker lazma uwe hot cake
 
Kumbuka mwanamke hana uwezo wa kuamua aolewe lini,lakini mwanaume unaweza kuamua naona kesho na ikawezekana. Sa kidume unakubalije kuendeshwa kama gari bovu
Issue ya kuoa/kuolewa ni point nyingine hata haina uhusiano na mada husika.
 
Back
Top Bottom