Hivi Mengi ni Team Lowassa?


Mengi ni sawa na akina Gwajima kwani wanafuata upepo. Mengi alishawahi mponda sana Lowassa na kumpongeza sitta lakini kwa sasa lowassa kwake ni lulu. Gwajima na Mengi n walewale.
 
Last edited by a moderator:
Mengi anabeba tabia zote za watu wa kaskazini, awa watu wa huko lao moja wanajificha kwenye kivuli cha kukomboa watanzania. Safari hii wanataka kutega kote kote so mengi anajua upande wa ukawa hakuna kikwazo ngoma ipo ccm ndio maana anatoa support asimame fisadi lowassa.

Awa watu wa huko wanajifanya smart sana na wamejaliwa kipaji cha kushika watu maskio. Wenye akili kama mzee mchonga walifanikiwa kuwadhibiti.
 

Bila shaka ufahamu wako umetawaliwa na UKABILA tuu na si vinginevyo...pole sana ndugu hii nchi haikufai,ushauri wangu nenda kaungane na ndugu zako Burundi
 
Bila shaka ufahamu wako umetawaliwa na UKABILA tuu na si vinginevyo...pole sana ndugu hii nchi haikufai,ushauri wangu nenda kaungane na ndugu zako Burundi

Mimi nna uwezo wa kuona wewe usiloweza kuliona, pole sana kama nmekugusa. Ila wazalendo hawawezi kutazama nchi wanapewa hao jamaa. Aluta continua!
 

Laiti ungelikuwa mzalendo usingeliweza kuwagawa wenzako kwa kigezo cha maeneo wanayotokea...maskini wa fikra umejawa na hisia za UKABILA
 
Mengi ni sawa na akina Gwajima kwani wanafuata upepo. Mengi alishawahi mponda sana Lowassa na kumpongeza sitta lakini kwa sasa lowassa kwake ni lulu. Gwajima na Mengi n walewale.

Hao ni wafanyabiashara wanaangalia maslahi yao ya kibiashara.
 
Bila shaka ufahamu wako umetawaliwa na UKABILA tuu na si vinginevyo...pole sana ndugu hii nchi haikufai,ushauri wangu nenda kaungane na ndugu zako Burundi

Ni kweli ishu ya Mengi kumuunga mkono Lowasa imeegea zaidi ukanda.Watanzania wengi mu-wanafiki sana.Mnajifanya hamuutakı ukabila lakıni kumbe ndo mnaoishi.Mm sıku zote nasema, Mengi nı mnafikı na mfanyabiasha asiye na tija japo anapenda kujinasıbu km mtu aliyefanikiwa kıbiashara lakını hamna la maana.Afanyavyo biashara mara ni tofauti na Bakharesa na hata Dangote.
 
Kisukuma tunasema wajameni..huyu tajiri niliyekuwa namuona mzalendo hivi kimetokea nini jamani TAJIRI MZALENDO akabadilika hivi KWELI...Mwanzoni haya mambo niliona kama utani...eehee nilipokuja kuona picha kama hii nikapiga mstari TUMEPOTEZA mpiganaji SIJUI nini kilitokea..MAAMUZI YAKE ndiyo gharama yake. UVUMILIVU ni moja ya tunda la wenye SUBIRA.Binafsi nilijiaminisha huyu Mzee ni full Mzalendo weyiiiiii Yesu na Maria Kumbe si Team Mzalendo atii!!!Kumbe kuna nyuma ya pazia kwa wenye macho ya kuona mbali...safari nao wanapanga safu pakuche nao wataweka wao eti ni zamu yao...eheee kumbe haijalishi Mungu alisema nini kwenye UADILIFU ili mradi ndiye anae sikika sana kule kwenye CCM basi na kwa kuwa ni mwenzetu huku tutamfikisha kule nasi tuingiee.AHHAHHAHAAA basi siwangetafuta basi japo mzalendo wa kweli kweli...
.


Fisadi Papa Na Fisadi Nyangumi
Rostam Aziz Na Reginald Mengi

 
Kuna bwana mmoja mjanja mjanja sana na anapenda kutumia vyombo vyake vya matangazo ikiwa ni pamoja na TV,Radio na magazeti.

Ni mjanja sana wa kukimbilia media pindi anapobanwa kwa hoja.

Ni mnafiki kwelikweli na ametumia makundi ya kijamii yenye shida kujijengea umaarufu asiostahili.

Amejidai ni mwenye nguvu ya media yenye uwezo wa kuangusha serikali!

Amewalaghai hata chadema kwa kujidai kurusha mikutano yao.


Ni mlaghai mno na mjanja sana wa kufuata upepo.

Ninachomuhurumia ni kwamba mwaka huu amaingia pabaya(wrong turn)

Kosa la kujiunga na kambi ya kifisadi ni kosa atakalojutia maishani kwani kwa mara ya kwanza ATASHINDWA na hapo ndio itakuwa kikomo cha UNAFIKI wake.


Bado majuma kama mawili tu kitaeleweka.
 
Pasco bwana huyu utakuwa unamjua sana.
 
Last edited by a moderator:
We mwenyewe mnafiki maana ungekuwa si mnafiki ungemtaja tukamjuwa. Hapa tuna dare ku talk openly.
 

Wewe mwenyewe ni mnafiki toa kwanza boriti kwenye jicho lako ndipo uone kibanzi kilichomo kwenye jicho la mwenzio mchawi sio lazima ufumaniwe ukiwanga matendo yako tu yatakutia muhuri wa kuoneka wewe ni mchawi.
 
We mwenyewe mnafiki maana ungekuwa si mnafiki ungemtaja tukamjuwa. Hapa tuna dare ku talk openly.

Mnafiki anaelezwa na kujadiliwa kinafiki.
yaani hii ni mada ya kinafiki dhidi ya unafiki ili ajue kuna wanafiki zaidi yake.

Great thinkers only!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…