Hivi maisha bila kuvaa nguo ingekuwaje?

Hivi maisha bila kuvaa nguo ingekuwaje?

Hapana mi sipendi kuchoka kwahivyo fikra zangu ni nyepesi nyepesi sana.

Sitaki kuteseka.

Fikra zako ziko deep…. hii issues ni dipuuu (kwa sauti ya Da Mange)
Issue ni deep iko ndaniii
Anyways nachojua wanaume wangechekesha sana 😂🤦🏻‍♀️
Ile mikia yao na gorori vinapiga pa pa pa pa 🤣🤣🤣🤣🙌
 
Una miaka mingapi mamaa?
mtu mzima wa makamo😁
Ingekuwa poa tu wala isingekuwa ajabu kutembea uchi. Miaka ya hivi karibuni si mbali sana hapo 1980s watu walikuwa wanatembea uchi wa mnyama na haikushangaza. Unakuta binti mkubwa tu hajavaa nguo chuchu saa sita zimesimama, tako hilo!, kijana wa kiume hajavaa nguo mkia umening'inia na hakuna matamanio ya kubakana. Wazee ilikuwa ni kawaida kuona mitulinga imening'nia chini huku juu kavaa mgolole/shuka anatembea hana wasiwasi. Fasheni za kuvaa nguo zikaanza na baadae chupi zikaja mtu anavaa nguo huku ndani kavaa chupi. Zikaja anda na chupi kwa wanawake baadaye taiti, mwanamke anavaa chupi na taiti kwa pamoja huku nje kavaa nguo nyingine ni ngumu kuona uchi wake. Wazee nao wakaanza kuvaa chupi ndani na nje wanavaa kaptula/suruali mikia ikaacha kuonekana. Sasa hivi ni ngumu hata kuona chupi ya mwanamke alijisahau kukaa ukaona mapaja yake. Ni fasheni tu ya kufunika mwili ili uchi usionekane na kujikinga na baridi
Aiseee kumbe ilikua hivyo sawa
 
Kwani hujawahi kuona kichaa mtu mzima anatembea uchi wa mnyama hajavaa nguo, jamii haimshangai, tena mkia unaonekana wazi hasa vichaa wa kiume! Kichaa wa kike ni nadra sana kuonekana akiwa uchi wa mnyama ila wa kiume imezoeleka na hakuna anayejali kumvika nguo. Kuna mzee mmoja ni kichaa mwaka wa kumi sasa namuona havai nguo anarandaranda tu mtaani kwake watu wamezoea kumtazama wanaona ni kawaida tu, mpaka watoto humtazama na kuona mkia wake. Enzi zetu ilikuwa ni mwiko kabisa kuona na kutazama uchu wa mtu yeyote hata kama ni kichaa, unafumba macho apite/upite usione uchi ule
Kwanini hakamatwi na akavalishwa nguo 🤔
 
Suala la kubaki uchi limebaki kwa watu wawili tu, mke na mume wake chumbani kwao huko ndani. Watoto wadogo bado hawajitambui na hawajui kuwa uchi ni faragha haipaswi kuonwa na mtu mwingine, havioni aibu kutokuvaa nguo kuficha uchi. Suala la kubaki uchi si la kawaida na halijazoeleka
Kwakweli kukaa uchi ni chumbani tu
 
Nimetoka kuoga wakati napaka Lotion nilikua mbele ya kioo gafla nikajiona kwenye kio nikiwa mtupu

Hapo hapo nikajiuliza hivi ingekuaje kama tungekua tunatembea utupu bila nguo hivi maisha yangekuaje?

Nikajiuliza pia hivi ni nani alipata wazo la kuvaa nguo

Aliwaza nini ?
Ni baridi kali ilimsukuma?
Au jua kali kupita kiasi?
Au aibu ?
Kama ni aibu alijuaje hii ni aibu ?

Maana kwa viumbe hai nadhani mwanadamu ndio anavaa nguo

Mada yangu naigawanya sehemu mbili wewe mdau utajibu upande unaopenda
👇

Mtazamo wa kidini

Kwa mujibu wa Biblia, baada ya Adamu na Hawa kula tunda walilokatazwa, wakafumbuliwa macho wote wawili, wakajua kuwa wako uchi wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo (Mwanzo 3:7)

Baadaye Adamu akasema:

Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha (Mwanzo 3:10)

Hapo tunaona Adamu alikua akiishi mtupu na hakuwahi kugundua kua alikua mtupu alikua kawaida

Baada ya kula hilo tunda ndio akagundua kua yupo uchi yeye na Hawa

Swali la kujiuliza kama Adam aligundua kua yupo uchi baada ya kula tunda

Hii ina maana mwanzo hakujua chochote na alikua akiishi mtupu

Je huko kwenye bustani ya Edeni hakukua na baridi?
Kama lilikuepo mbona hakusikia?
Je hakukua na jua kali ?
Kama lilikuepo mbona hakulisikia?

Au kulikua na mazingira rafika kwa kuishi mtupu?

Je, simulizi hili linaonyesha kwamba desturi ya kujisitiri ilianza hapo, au ni fundisho la kiroho kuhusu dhamiri ya mwanadamu?


Mtazamo wa kifalsafa 👇

JE , nguo ni matokeo ya akili ya mwanadamu kutafuta ulinzi dhidi ya baridi, jua na mazingira, au ni makubaliano ya kijamii kuhusu staha na utambulisho?

Leo utasikia mtu wa kwanza kugundua simu ni fulani

Aliegungua radio ni fulani

Hivi ni nani wa kwanza aligundua kwamba watu wavae nguo badala ya kutembea watupu?

Kama tungekuwa kama wanyama wengine wasiovaa nguo, je, maadili na maisha ya jamii yangekuwaje?

Yaani tuwe kama ng'ombe , Mbuzi ,
Au wanyama wa mwituni

Yaani tungekua tunapeta naked ingekuaje😅🙌

ShesRise_1 ✋️
Tungedinyana kama kuku!
 
Back
Top Bottom