Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 57,216
- 128,978
Mkuu Mchambuzi kwa maoni yako kwenye hii lineup ya hawa panya, unaona kweli kuna panya yoyote mwenye uwezo wa kumfunga paka kengele? .Katiba ya JMT (1977) inamruhusu, na kanuni za chama chake zinamruhusu. Lakini ikitokea baadhi ya mawaziri wakajitenga kati ya sasa na 2020 kwa kuona kwamba hawaendani na kasi yake, hivyo kupisha wenye uwezo, watavurugana sana ndani ya chama chao, na sio kwa uchaguzi wa 2020 tu bali hata uchaguzi wa Mwenyekiti taifa baadae mwaka huu.
Nimenote hata wale watu wa Nyerere waliokuwa very vocal wakati wa JK kina Butiku, Kaduma, Kitine, Warioba and the like wameisha soma alama za nyakati na kujua saa hizi ni nyakati nyingine hivyo wamekaa chonjo saa mbaya.
Ila kuna kigogo mmoja tuliongea off the record akasema atamtafuta na kumkabili, haiwezekani wote tuendelee tuu kumchekea nyani, tutayavuna mabua ilhali shamba ni letu sote.
Paskali