Hivi Magufuli atagombea tena?

Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,898
11,745
Nakumbuka wakati wa kampeni alivyopata shida kujinadi, ikafika mahali mzee wa watu akaanza kupiga push ups, akaongea kila lugha ili raia wamuelewe haikutosha akaacha na chama chake akaanza kukiponda na kusema wao ndio wameifikisha hii nchi hapa.

Maswali pekee ambalo najiuliza mpaka sasa huyu mtu atagombea tena? Hakumbuki yaliyompata kipindi kile, hivi atawaeleza nini watanzania wamuelewe au ndio anasubiri 2019 awasaulishe, atarudi Kagera kuomba kura? Kule simiyu ataenda? Watumishi wa umma atawaomba kura? Wanafunzi wa vyuo vikuu je?, wahitimu wa vyuo vikuu atawambia nini? Atajiteteaje kuhusu Tanzania ya viwanda, nakumbuka alisema serikali yake ni viwanda hivyo viwanda vimefika vingapi? Au ndio vile anavyozindua vilivyo anza kufanya kazi kipindi cha Kikwete.

Vijijini huko atawaeleza nini kuhusu milioni 50 alizoahidi, ataenda huko kweli kuomba kura zao. Wafanyabiashara ambao wamefunga biashara zao kutokana na hali mbaya kiuchumi atawaambia nini? Kuna msemo unasema "usitukane mambo kabla hujavuka mto" nakumbuka Mhe alianza kwa mbwembwe na dhihaka nyingi kwa watangulizi wake, nadhani hivi sasa anajionea.
 
Katiba ya JMT (1977) inamruhusu, na kanuni za chama chake zinamruhusu. Lakini ikitokea baadhi ya mawaziri wakajitenga kati ya sasa na 2020 kwa kuona kwamba hawaendani na kasi yake, hivyo kupisha wenye uwezo, watavurugana sana ndani ya chama chao, na sio kwa uchaguzi wa 2020 tu bali hata uchaguzi wa Mwenyekiti taifa baadae mwaka huu.
 
Katiba ya JMT (1977) inamruhusu, na kanuni za chama chake zinamruhusu. Lakini ikitokea baadhi ya mawaziri wakajitenga kati ya sasa na 2020 kwa kuona kwamba hawaendani na kasi yake, hivyo kupisha wenye uwezo, watavurugana sana ndani ya chama chao, na sio uchaguzi wa 2020 tu bali hata uchaguzi wa Mwenyekiti taifa baadae mwaka huu.
Waziri gani wa kujitenga pale, wote ni wakufyata.
 
Nakumbuka wakati wa kampeni alivyopata shida kujinadi, ikafika mahali mzee wa watu akaanza kupiga push ups, akaongea kila lugha ili raia wamuelewe haikutosha akaacha na chama chake akaanza kukiponda na kusema wao ndio wameifikisha hii nchi hapa.

Maswali pekee ambalo najiuliza mpaka sasa huyu mtu atagombea tena? Hakumbuki yaliyompata kipindi kile, hivi atawaeleza nini watanzania wamuelewe au ndio anasubiri 2019 awasaulishe, atarudi Kagera kuomba kura? Kule simiyu ataenda? Watumishi wa umma atawaomba kura? Wanafunzi wa vyuo vikuu je?, wahitimu wa vyuo vikuu atawambia nini? Atajiteteaje kuhusu Tanzania ya viwanda, nakumbuka alisema serikali yake ni viwanda hivyo viwanda vimefika vingapi? Au ndio vile anavyozindua vilivyo anza kufanya kazi kipindi cha Kikwete.

Vijijini huko atawaeleza nini kuhusu milioni 50 alizoahidi, ataenda huko kweli kuomba kura zao. Wafanyabiashara ambao wamefunga biashara zao kutokana na hali mbaya kiuchumi atawaambia nini? Kuna msemo unasema "usitukane mambo kabla hujavuka mto" nakumbuka Mhe alianza kwa mbwembwe na dhihaka nyingi kwa watangulizi wake, nadhani hivi sasa anajionea.
Tume ya uchaguzi ni ile ile pia January yupo ni mwendo wa uchakachuaji kama kawaida.
 
Wenye upeo wa kuona mbali wameshaachana na hizi kelele,wameshagundua ni kelele tu,CCM ni ile ile,tume ya uchaguzi ni ile ile na imefanyiwa marekebisho msiyopenda kusikia zaidi,katiba ni ile ile,kwa kukukumbusha 2020 hakuna UKAWA kwa wenye kuelewa wameshaelewa,CDM kama watamuweka tena yule waliyemnadi ni FISADI PAPA tena,basi CCM ushindi ni wa saa 5 asubuhi,yule jamaa hatakaa aachiwe kikombe kwa namna yoyote aingie IKULU,haitakaa itokee.Ndio maana ya ule usemi wa afe beki afe kipa.
 
Ushindi saa tano? Kama 2015 hali ilikuwa vile unadhani 2020 patatosha? Ima ccm ikubali kuanguka au wafanye ya Gambia. Watu wana hasira nanyi sana.
 
Mkuu unaongea kama huwajui watanzania vizuri,CDM ni taasisi,ila CCM ni taasisi kubwa zaidi,ikifika 2019 mambo yatasetiwa na wataalam,mzunguko utakuwepo wa pesa,na bahasha kibao na watu watasahau yote,tatizo mnaangalia ya mwaka mmoja tu,mnaanza kutoa tathmini ya 2020,mwaka jana mlipigwa mkwara wa maandamano,kila mtu kimya,sijaona hata wa kukohoa,mmepiga kelele kwenye magazeti na TV sasa hivi yameanza kukaa kimya pia,mpaka 2018 tutakuwa tumeshaanza kuwa kama China yenye chama kimoja,watu wa propaganda zitakuwa hazilipi tena,sana sana itabakia JF kama nayo itapona misukosuko iliyopo,hapo ndo utaelewa ninachojaribu kumaanisha.2020 hakuna hata hayo mafuriko ya kutengeneza,mambo yatakuwa yamebadilika sana,watu watakuwa wameshaacha mazoea ya kupiga domo,itakuwa ni kila mtu bize na familia yake na tumbo lake.Jaribu kuangalia hili suala kwa mapana,sio kwa ushabiki au upenzi wa chama fulani.
 
Waungwana wanasema tunatakiwa tusamehe lakini tusisahau.
 
Mafuriko yalianza kutengenezwa tangu enzi za Lyatonga Mrema tena Mbabe mwenyewe Nyerere alikuwepo hai sembuse 2020 ndio unafikiri mafuriko yataisha?
 
MIAKA 20 AU MUGABE STYLE. ..MAY HE REIGN. ..MAY HE SHINE ALL OVER THE WORLD. ...
 
Acha hizo wewe usitukane "mambo" ndiyo kitu gani? Kwa taarifa yako ni kwamba atagombea na ushindi uko palepale. Hapa kazi tu
 
Back
Top Bottom