Hivi Lissu ana dini kweli?

Huyo siyo Lissu na sio sauti yake
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amewashangaza Watanzania kuhoji uwezo wa Mungu katika uponyaji wa janga la corona nchini.

Kauli hiyo ya Lissu pia imeenda mbali zaidi alipowashangaa Waislamu na Wakristo kwenda kanisani na misikitini kuombea corona huku akiwaita ni wajinga.

Lissu ametoa kauli hizo tata zinazozidi kutoa tafakari ya afya yake ya akili akihojiwa na Radio Maisha ambapo amesema Mungu kwamba hawezi kuponya magonjwa na hana muda wa kuhangaika na wajinga.

“Kama alivyosema rais mwenyewe hii kitu dawa yake ni kwenda msikitini na makanisani kuomba Mungu, katika karne ya 21 rais anayesema ana PHD katika Kemia kuamini kwenye mambo kwamba unaweza kutibu ugonjwa kwa maombi ya Mungu,” amesema Lissu.

Mtangazaji wa kipindi hicho alimuuliza Lissu; “Kwa hiyo hujapendezwa kabisa kwa namna rais anavyoshughulika na hii ishu ya covid19 pale nchini?”
Lissu akajibu: “Mungu ana mambo mengi sana hana muda wa kuhangaika na wajinga.”

Kauli hii ya Lissu inaacha maswali kwamba je; ana dini? Kama kweli angekuwa na dini basi angekuwa na hofu ya Mungu.

Lissu anasahau kama ni Mungu amemponya na kumfikisha hapo alipo leo badala yake alianza kutukana watu kama vile haitoshi amehamia kwa muumba na watumishi wa wake.

View attachment 1611348
 
Sijasema hivyo.

Mafundisho yetu ni sala na kazi. Tukiumwa tunaenda hospitali huku tukiamini kuwa Mungu ndiye anayeponya wao madaktari wanatibu tu, pia ni Mungu aliyebariki na kuwezesha dawa na maarifa ya kitabibu kugunduliwa.
Hapa tupo wote. Huu ndio ukweli.

Wakati gonjwa la corona lilivotikisa sawa tuliomba safi kabisa. Tahadhari nayo mfano kuvaa mask ni jambo la muhimu ma doctor walishauri. Sema imefikia kipindi ukivaa mask mkulu akiwepo kwenye huo mkutano unaonekana kituko.

Lazima mtu mwenye akili akubali kua Corona si gonjwa la kiafrika. Magonjwa yako maeneo kwa maeneo. Mfano tropical countries yellow fever au malaria.

Kwa muktadhaa huu huu tukubaliane corona sio kwa waafrika. Km ni kweli very few.

Kusema tumeomba na korona ikatoweka ni ujinga. Ni kama mzungu wa England aseme malaria England hamna coz Mungu wetu tulimuomba akatusikiliza. Nyie waafrika Mungu hakuwasikiliza upande wa malaria.

Kwa maana nyingine hem tuitishe kuomba na kufunga mwezi mzima malaria iishe Tanzanian kama kweli kuomba tu ugonjwa unaondoka.

Maana yake nn, ni kua hili gonjwa halijafanyiwa research ya kutosha. Hivyo wataalam wangepata fursa hiyo huenda wangetupa majibu sahihi why not Africa.

Achana na wakenya sijui lockdown hiyo ilikua geresha watu wapige pesa.

Magufuli nnachomkubali ni ule uthubutu wake wa kujaribu njia ya kwamba kwa sisi huu sio ugonjwa wetu pigeni kazi. This Magufuli guy I'm telling you was gambling. And his gambling paid big time. Yaani ikatokea kwamba ku gamble kwake ikawa kwanza ugonjwa sio wetu, kitu ambacho amewapiga bao wana science.

Kama huu ugonjwa ulikua ni wa kwetu mbona tungeokotana vibudu.

Tusitaniane ugonjwa haujaondolewa kwa kuomba. Ni kua hautuhusu kutoka na labda geographical location yetu.
 
Tangu Lisu aweke nguvu katika kuwapambania wapenzi wa jinsia mmoja nikajua Lisu anashida kichwani Ila sikutegemea kwamba anaweza kukufuru kwa kiwango hicho.
Ccm ndio imeandika hadi barua kwenye balozi
 
Hapa tupo wote. Huu ndio ukweli.
Wakati gonjwa la corona lilivotikisa sawa tuliomba safi kabisa. Tahadhari nayo mfano kuvaa mask ni jambo la muhimu ma doctor walishauri. Sema imefikia kipindi ukivaa mask mkulu akiwepo kwenye huo mkutano unaonekana kituko.

Lazima mtu mwenye akili akubali kua Corona si gonjwa la kiafrika. Magonjwa yako maeneo kwa maeneo. Mfano tropical countries yellow fever au malaria.
Kwa muktadhaa huu huu tukubaliane corona sio kwa waafrika. Km ni kweli very few.

Kusema tumeomba na korona ikatoweka ni ujinga. Ni kama mzungu wa England aseme malaria England hamna coz Mungu wetu tulimuomba akatusikiliza. Nyie waafrika Mungu hakuwasikiliza upande wa malaria.
Kwa maana nyingine hem tuitishe kuomba na kufunga mwezi mzima malaria iishe Tanzanian kama kweli kuomba tu ugonjwa unaondoka.

Maana yake nn, ni kua hili gonjwa halijafanyiwa research ya kutosha. Hivyo wataalam wangepata fursa hiyo huenda wangetupa majibu sahihi why not Africa.
Achana na wakenya sijui lockdown hiyo ilikua geresha watu wapige pesa.

Magufuli nnachomkubali ni ule uthubutu wake wa kujaribu njia ya kwamba kwa sisi huu sio ugonjwa wetu pigeni kazi. This magufuli guy I'm telling you was gambling. And his gambling paid big time. Yaani ikatokea kwamba ku gamble kwake ikawa kwanza ugonjwa sio wetu, kitu ambacho amewapiga bao wana science.
Kama huu ugonjwa ulikua ni wa kwetu mbona tungeokotana vibudu.
Tusitaniane ugonjwa haujaondolewa kwa kuomba. Ni kua hautuhusu kutoka na labda geographical location yetu.
Vyovyote utakavyoamini lakini wote kuanzia Lissu, Zitto, wafuasi wao na watanzania kwa ujumla tunakiri aidha hadharani au kimya kimya kuwa corona haipo Tanzania na mwenye kustahili credit ni Rais Magufuli kwa namna alivyotuongoza kuushinda ugonjwa huu. Kama angefuata ushauri na kelele za kina Zitto na Mbowe, bunge la bajeti lisingefanyika, uchaguzi mkuu leo hii tusingekuwa tunaufanya.

Kenya wanahangaika na huu ugonjwa hadi sasa.

Hongera sana Magufuli kwa uongozi wako thabiti. Kura zote tumpe Msgufuli na CCM ili atufanyie makubwa zaidi.
 
Yes yuko sahihi kabisa
Kilichotumika ni uponywaji wa kisaikologia

Mungu huyu huyu awauwe Mpaka taifa ambalo alilitamka kwenye kitabu chake kuwa ni taifa teule Israel kwa Korona then Tanzania iachwe?

Mpaka Ibada ya hija maca ilisitishwa because ya korona
Wao walimlilia Mungu kama sisi tulivyofanya?

Kama ni msomaji wa biblia utakuwa unajua kuwa hao taifa teule mara nyingi walipomkosea aliwaadhibu vikali.

Approach ya mwanzo gonjwa lilipokuwa linaingia ndiyo ina matter, wao na nchi zingine walichagua kupambana wenyewe sisi tulichagua kumtegemea Mungu na matokeo unayaona dunia nzima.
 
Magufuli ni mkristo ,Mkatoliki kanisani anaenda kufanya ni nini na damu za watu aliso mwaga?
Kwa ushahidi upi ulionao kuwa Magufuli alimwaga damu Kama sio propaganda tu za mitandaoni?

Hivi Chadema hamjifunzi kwa Mch.Peter Msigwa alimwaga tuhuma kibao kwa Kinana alipopelekwa mahakamani akashindwa kutoa ushahidi, ikabidi aombe radhi kwa vyombo vya habari. Mtu Kama wewe ukipelekwa mahakamani utaanza kulialia tu. Acheni propaganda za kuchafua viongozi wa nchi.
 
Wao walimlilia Mungu kama sisi tulivyofanya?

Kama ni msomaji wa biblia utakuwa unajua kuwa hao taifa teule mara nyingi walipomkosea aliwaadhibu vikali.

Approach ya mwanzo gonjwa lilipokuwa linaingia ndiyo ina matter, wao na nchi zingine walichagua kupambana wenyewe sisi tulichagua kumtegemea Mungu na matokeo unayaona dunia nzima.

Acha ukilaza ndugu yangu
Kovid ipo, kuwa Makini
 
Ninapigwa butwaa na watu wanaojinadi kumuombea Lissu kwa Mungu kwamba ndiye awe chaguo la Watanzania.

Ikumbukwe kipindi cha CORONA akihojiwa na mtangazaji wa BBC, Lissu alisema kitendo cha Magufuli ambaye nii mbobezi kwenye kemia kumtegemea Mungu kuwa atatuokoa na janga la Covid ni ujinga mkubwa.

Tena akaendelea kusema kuwa katika karne hii ya 21 kumtegemea Mungu kwamba ataweza kutuepusha na zahama la Covid ni upuuzi.

Sasa najiuliza Askofu Bagonza na akina Ponda wanamtaja Mungu yupi pale wanapomuombea Lissu?

Hata wewe unayesoma uzi huu jiulize, ni Mungu yupi ambaye anatembea na Lissu huku akimkufuru na kuwadhihaki wanaomtegemea?

Lissu akapimwe akili
 
Upo hapa kuhalalisha mwanadamu kupigwa risasi bila kosa?

Yaani upo hapa kufurahia Lissu kupigwa risasi?

Fvck you big time!
Akili yako bado ndogo sana kuelewa mambo mapana kama haya.
Ni wewe ndiyo unaona hakuna kosa ila wenye kumpga ndiyo wanajua kosa alilofanya.

Pia hata aliyepigwa anajua kosa alilofanya hadi akapigwa maana alishawahi kukiri hadharani kuwa kwanini yeye alipigwa risasi.
Ila kwa sababu uelewa wako ni mdogo utaendelea kuuuliza maswali ya kipuuzi.
 
Vyovyote utakavyoamini lakini wote kuanzia Lissu, Zitto, wafuasi wao na watanzania kwa ujumla tunakiri aidha hadharani au kimya kimya kuwa corona haipo Tanzania na mwenye kustahili credit ni Rais Magufuli kwa namna alivyotuongoza kuushinda ugonjwa huu. Kama angefuata ushauri na kelele za kina Zitto na Mbowe, bunge la bajeti lisingefanyika, uchaguzi mkuu leo hii tusingekuwa tunaufanya.

Kenya wanahangaika na huu ugonjwa hadi sasa.

Hongera sana Magufuli kwa uongozi wako thabiti. Kura zote tumpe Msgufuli na CCM ili atufanyie makubwa zaidi.
Hakuna sehemu ya dunia uchaguzi umeahirishwa sababu ya korona. Marekani inaongoza kwa korona lkn uchaguzi kama kawa.

Kenya hamna korona. Ni usanii tu unafanyika kula pesa za WHO.
Hoja zako zingine ziko kwenye post yangu uliocopy.
 
KURA ZA UBUNGE NA URAISI ZITASAFIRISHWA KWENDA KUHESABIWA JIMBONI, HAZITAHESABIWA KWENYE VITUO VYA KUPIGIA KURA

KURA ZA UDIWANI ZITASAFIRISHWA KWENDA KUHESABIWA MAKAO MAKUU YA KATA (KATANI)

WAPINZANI HAMPATI KITU.

KUWENI MAKINI
Kwani sisi hatukujui katani, hatukujui wilayani, kwa akili ndogo tu ulipaswa ujue kuwa wilayani asilimia kubwa ndiko Kuna mizizi ya upinzani, wakienda huko Ndio zoezi la wizi litakuwa gumu zaidi, na Kama hujui kura haziibwi wilayani, wanapachika hi ukohuko kwenye vituo vya uchochoroni
 
Hata uwe na IMANI inayohamisha milima...lakini kama huna UPENDO, imani yako ni kazi bure.

Kitendo cha kutaka kumuua lissu ni kukosa upendo.
 
Hakuna sehemu ya dunia uchaguzi umeahirishwa sababu ya korona. Marekani inaongoza kwa korona lkn uchaguzi kama kawa.

Kenya hamna korona. Ni usanii tu unafanyika kula pesa za WHO.
Hoja zako zingine ziko kwenye post yangu uliocopy.
Marekani kura wanapigaje? Hujasikia kura za mapema zimepigwa tena kwa posta?

Kwa katiba ya Kenya si rahisi kudanganya kuwa kuna corona wakati haipo. Kenya ipo.
 
Tangu Lisu aweke nguvu katika kuwapambania wapenzi wa jinsia mmoja nikajua Lisu anashida kichwani Ila sikutegemea kwamba anaweza kukufuru kwa kiwango hicho.
Hebu tuoneshe clip moja aliyowapambania mashoga.

Je serikali yako inasemaje kuhusu hayo unayomshingizia lissu.View attachment 1611891
IMG_20201018_161556.jpg
View attachment 1611892
 
Back
Top Bottom