jijiletublog
Member
- Jul 23, 2020
- 31
- 74
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amewashangaza Watanzania kuhoji uwezo wa Mungu katika uponyaji wa janga la corona nchini.
Kauli hiyo ya Lissu pia imeenda mbali zaidi alipowashangaa Waislamu na Wakristo kwenda kanisani na misikitini kuombea corona huku akiwaita ni wajinga.
Lissu ametoa kauli hizo tata zinazozidi kutoa tafakari ya afya yake ya akili akihojiwa na Radio Maisha ambapo amesema Mungu kwamba hawezi kuponya magonjwa na hana muda wa kuhangaika na wajinga.
“Kama alivyosema rais mwenyewe hii kitu dawa yake ni kwenda msikitini na makanisani kuomba Mungu, katika karne ya 21 rais anayesema ana PHD katika Kemia kuamini kwenye mambo kwamba unaweza kutibu ugonjwa kwa maombi ya Mungu,” amesema Lissu.
Mtangazaji wa kipindi hicho alimuuliza Lissu; “Kwa hiyo hujapendezwa kabisa kwa namna rais anavyoshughulika na hii ishu ya covid19 pale nchini?”
Lissu akajibu: “Mungu ana mambo mengi sana hana muda wa kuhangaika na wajinga.”
Kauli hii ya Lissu inaacha maswali kwamba je; ana dini? Kama kweli angekuwa na dini basi angekuwa na hofu ya Mungu.
Lissu anasahau kama ni Mungu amemponya na kumfikisha hapo alipo leo badala yake alianza kutukana watu kama vile haitoshi amehamia kwa muumba na watumishi wa wake.