Hivi kweli kuna Mtanzania mwenye akili zake timamu anaweza kuichagua tena CCM, kwa Lipi?

Ukiwa na Ubongo timamu uliobeba akili timamu zinazofanya kazi kwa utimamu wake, akili timilifu, HUWEZI KUISHABIKIA CCM.
Mkuu Allen Kilewella , kwanza naheshumu mawazo yako hata kama sukubaliani na wewe.

Pili hata mimi kule nyuma, pia niliwahi kuwaza kama ulivyowaza wewe, lakini baada ya kufanya research ya kutosha kwenye siasa zetu,
nikajikuta kwa Tanzania, hakuna vyama, kuna chama kimoja tuu ambacho ndicho chama kweli cha siasa ambacho ni the one and only CCM!, na kuna vikundi na magenge posing kama vyama ,Je, mtu kujiunga CCM ni ujinga? Je, wana CCM ni wajinga? Je, watanzania wanaoichagua CCM, kila uchao ni wajinga? Its not fair

Hivyo usipo ichagua CCM, utachagua nini?!. Do Tanzanian have a choice to choose from?
P
 
Mkuu umeandika vizuri, Mie nimejiunga Chadema 2019 na ndo mwaka nikajiunga jf, hasa baada ya kuona kila aliekua ccm anaonekana ndo mwenye nchi, nilisema hapana ngoja niwe chadema ukweli Sina stress, ccm ni janga la taifa, wahuni Sana hawa
Ubarikiwe sana
 
Sio wewe tu walikuwepo akina Lizabon, Imhotep na John sasa hivi wana furaha.

Kuwa ccm nikujitafutia laana hata kama unaona kwa sasa unatusua lakini huko mbele itavuna ulichopanda
 
Hata mimi kule nyuma, pia niliwahi kuwaza kama wewe, nikajikuta kwa Tanzania, chama kweli cha siasa ni kimoja tuu, the one and only CCM!, hivyo usipo ichagua CCM, utachagua nini?!. Do Tanzanian have a choice to choose from?
P
Ndio chama ulichopata kura moja kati ya kura 1000?
Ingawa kwenye maisha tunashauriwa tusikate tamaa ile wewe Mzee umepitiliz viwango.

Shukuru Mungu ni mtoto wa system ungekuwa kituko🤣🤣
 
Ndio chama ulichopata kura moja kati ya kura 1000?
Unaposhindana na kushindwa, unajitathmini umeshindwaje. Hivyo kuna kushindwa na kushindwa, ukishindwa ukajitathmini umeshindwa kihalali na waliokuzidi sifa, unakubali kushindwa na kushirikiana na washindi, ndivyo ilivyokuwa Kawe, tulikuwa wagombea 176, anatakiwa mmoja, nikashindwa kihalali kabisa na kujitokeza humu jf kuwaomba msinibeze Uchaguzi 2020 - Wana JF, nipeni Pole. Msinicheke wala msinibeze; nimegombea ubunge Kawe kupitia CCM nimeambulia kura 1. Ama kweli CCM ina wenyewe!
Hivyo nakuomba na wewe usinibeze!.

Hujabezwa umeelezwa fact kuwa ulipata kura 1/1000. Naushkuru maana kwasystem yenu yamagoli yamkono hatahiyo moja (yakwako) ungeikosa!!!
Si unawasimangaga alafu ghafla ukawashobokea pindi ya uchaguzi kisa kabila ukajua utabebwa hahahhhaaaa... Hawashindwi kukuwekea hata negative wale ndugu njaa(mayala) mzee wa pppppprz sjui
 
Hujabezwa umeelezwa fact kuwa ulipata kura 1/1000.
Its true nilipata kura moja, kuendelea kusema sema kuhusu mimi kupata kura moja ni kunisimanga. Uchaguzi 2020 - Wana JF, nipeni Pole. Msinicheke wala msinibeze; nimegombea ubunge Kawe kupitia CCM nimeambulia kura 1. Ama kweli CCM ina wenyewe! niliwaomba humu msinibeze wala msinisimange kwa hiyo kura moja!.
Si unawasimangaga alafu ghafla ukawashobokea pindi ya uchaguzi kisa kabila ukajua utabebwa hahahhhaaaa... Hawashindwi kukuwekea hata negative wale ndugu
Mimi huwa sisimangi wala sishoboki, ukiona nimesema jambo ujue ni la kweli.
P
 
Usinijibu kiholela like you are talking to CHADEMA F6 Div 0 mwenyekiti wenu, answer me with deep thinking, acha ujinga i said, CCM usiizoea kijinga jinga hivyo, nakwambia ukweli, uwe na adabu na CCM, acha ujinga for last time.
Na mimi nasisitiza...ukiwa na akili timamu huwezi kuishabikia CCM, full stop. Eti deep thinking! Deep thinking na UCCM ni kama mwanga na giza.

Adui mkubwa wa taifa hili ni CCM na hadi siku Watanzania watakapozinduka na kulielewa hilo, taifa la Tanzania halitafanikiwa lolote chini ya hilo genge, CCM.

Vitisho havisaidii kitu, vitisho havitakuondoa kwenye tope la ujinga na vitisho vinazidi tu kukuanika tu usivyo na akili na kwa CCM hiyo ni sifa ya kutwaa uongozi!
 
Japokuwa uzi wa mtoa hoja uko kiukakasi, majibu yako haya na hiyo "like" ya Pascal mnampa "points" nyingi mtoa mada.

Mlipaswa kujibu kwa kuthibitisha kinyume cha mtoa hoja, sasa ona maneno haya uliyoandika, mmmh! anaweza kuwa yuko sawa kupitia kwako.
 
Nikajikuta kwa Tanzania, hakuna vyama, kuna chama kimoja tuu ambacho ndicho chama kweli cha siasa ambacho ni the one and only CCM!, na kuna vikundi na magenge posing kama vyama

Hivyo usipo ichagua CCM, utachagua nini?!. Do Tanzanian have a choice to choose from?
P
Kwanza ndugu yangu Pasco nikushukuru kwa kuchangia, lakini lazima kila wakati usitake mitizamo yako iwe ndiyo Kweli (Facts) hata kama wewe unaona ni ukweli (The truth).

CCM siyo fumbo la imani kiasi kwamba watanzania wasio wana CCM hawaoni jinsi kinavyoendesha siasa zake za ndani na nje ya chama hicho. Kusema kwamba vyama vingine nje ya CCM ni magenge yaliyopozi kama vyama vya siasa, ni kujikosea heshima wewe mwenyewe na utovu wa adabu dhidi ya wanachama wa vyama hivyo.

Hao waliomo ndani ya vyama hivyo unavyoviita magenge ndiyo kila siku wanateswa, wanauawa, wanazuiwa kufanya mikutano ya hadhara, vyama vyao vinaingiliwa kila siku na msajili wa vyama vya siasa, wakishiriki chaguzi wanaporwa ushindi wao, hao watanzania wenzako wanaofanyiwa kila aina ya ufidhuli ni binadamu kama wewe, inakuwaje wewe unaona sawa. hizo ni akili timamu kweli?
 
Ndugu yangu Allen Kilewella, Tanzania iliwahi kuitwa kisiwa cha amani nyakati fulani. Sifa ya Tanzania ilijulikana huko nje hadi watoto walipozaliwa wazazi waliona fahari kuwapa majina ya Kitanzania.

Mtanzania aliheshimiwa na katika nchi nyingi hukuhitaji hata hiyo viza kuingia. Ilikuwa ukionesha pasipoti ya Tanzania tu mlango unafunguliwa uingie uendelee na shughuli zako bila bughdha.

Hivi sasa inabidi Rais wa nchi ashiriki katika filamu inayoitwa Royal Tour eti kuitangaza Tanzania. How did we sink this low? What happened in between? Jibu ni rahisi sana, taifa letu pendwa limetekwa!

Wengine wetu tukikumbuka zama hizo tunajikuta tunalia na kutoa machozi. Lipo genge limeiteka nchi yetu na hivi sasa wengi tunaishi ndani ya taifa letu kama mateka...genge hilo si lingine bali CCM!

Sasa hivi iko sera isiyo rasmi inaitwa jaribu uone...likosoe hilo genge uone cha moto. Wapo ndugu zetu wamemwagwa mitaani na mtandaoni kama huyo Jay One, Mtanzania anatishwa na kuwindwa kama nguchiro ndani ya taifa lake!

Kosa? Kudai haki, kudai usawa, kudai uhuru wa mawazo, kuikosoa serikali yetu wenyewe Watanzania, kuwakosoa viongozi watumishi wetu, kupinga uonevu katika sura zake zote, kudai utawala wa sheria na kudai Katiba mpya.

Ukiwa na akili timamu huwezi kuishabikia CCM!
 
Na mimi nasisitiza...ukiwa na akili timamu huwezi kuishabikia CCM, full stop. Eti deep thinking! Deep thinking na UCCM ni kama mwanga na giza.

Adui mkubwa wa taifa hili ni CCM na hadi siku Watanzania watakapozinduka na kulielewa hilo, taifa la Tanzania halitafanikiwa lolote chini ya hilo genge, CCM.

Vitisho havisaidii kitu, vitisho havitakuondoa kwenye tope la ujinga na vitisho vinazidi tu kukuanika tu usivyo na akili na kwa CCM hiyo ni sifa ya kutwaa uongozi!
Mkuu Mag3, with due respect, wewe ni GT humu, you can't be missing the point hivi kudhani adui mkubwa wa taifa hili ni CCM, CCM haikujiweka yenyewe imewekwa!. CCM haijichagui yenyewe, inachaguliwa hivyo adui mkubwa sio kilichowekwa bali aliyekiweka!. Adui mkubwa sio CCM kilichochaguliwa bali yule aliyekichagua!.
Karibu pande hizi Elections 2015 - Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni ...
P
 
Its true nilipata kura moja, kuendelea kusema sema kuhusu mimi kupata kura moja ni kunisimanga. Uchaguzi 2020 - Wana JF, nipeni Pole. Msinicheke wala msinibeze; nimegombea ubunge Kawe kupitia CCM nimeambulia kura 1. Ama kweli CCM ina wenyewe! niliwaomba humu msinibeze wala msinisimange kwa hiyo kura moja!.

Mimi huwa sisimangi wala sishoboki, ukiona nimesema jambo ujue ni la kweli.
P
Hapana Bro Wewe Si Mungu! Hadi Wewe Ukisema Jambo Liwe Ni La Kweli. Kuna Mambo Mengine Unasema Na Unakuwa Umekosea Ingawa Kwenye Ulimwengu Wako Unaona Ni Kweli.
 
Mkuu Mag3, with due respect, wewe ni GT humu, you can't be missing the point hivi kudhani adui mkubwa wa taifa hili ni CCM, CCM haikujiweka yenyewe imewekwa!. CCM haijichagui yenyewe, inachaguliwa hivyo adui mkubwa sio kilichowekwa bali aliyekiweka!. Adui mkubwa sio CCM kilichochaguliwa bali yule aliyekichagua!.
Karibu pande hizi Elections 2015 - Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni ...
P
Hivi Pasco unaposema CCM imechaguliwa unamaanisha katika uhiyari (Free will) wa watanzania ama ni katika haya mazingaombwe yao wanayoyaita uchaguzi? Kwa mfano unataka kusema mwaka 2019 CCM ilichaguliwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na nchi nzima vyama vingine wakakataliwa?
 
Mkuu Mag3, with due respect, wewe ni GT humu, you can't be missing the point hivi kudhani adui mkubwa wa taifa hili ni CCM, CCM haikujiweka yenyewe imewekwa!. CCM haijichagui yenyewe, inachaguliwa hivyo adui mkubwa sio kilichowekwa bali aliyekiweka!. Adui mkubwa sio CCM kilichochaguliwa bali yule aliyekichagua!.
Karibu pande hizi Elections 2015 - Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni ...
P
Masikini Pascal Mayalla, acha unafiki, unafiki hupofusha! Kama kweli humuoni wala humjui nani anayeichagua CCM, vua hilo koti la unafiki angalau kwa muda mfupi na kama bado humjui hutamjua kamwe hata ukikutana naye uso kwa uso!

Tafadhali sana tena sana, najua kubambikia Watanzania mambo wasiyohusika nayo ni kawaida kwa wana CCM lakini hii ya kudai eti ndio wanaichagua CCM imevuka mpaka!

Unajua, na kila moja anajua kuwa uchaguzi ukiwa huru na wa haki CCM haiwezi kushinda
na hapo nimemnukuu aliyewahi kuwa kiongozi mwandamizi wa CCM, Humphrey Pole pole!
 
Back
Top Bottom