Hivi Kweli Kuna Mtanzania, Mwenye Akili Zake Timamu, Anaweza Kuichagua Tena CCM?!. Kwa Lipi?!.

Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

Platinum Member
35,653
2,000
Wanabodi, zikiwa zimabaki siku 14 tufanye uchaguzi wetu, naomba kuuliza, hivi kweli kuna Mtanzania, mwenye akili zake timamu, anayefahamu maana halisi ya maendeleo, tangu tulipopata uhuru, tulikuwa na rasilimali gani, tungepaswa kuwa wapi, na kulinganisha na hapa tulipo sasa, halafu ukaelezwa sababu ya sisi Tanzania kuwa hapa tulipo, ni CCM, then hivi kuna Mtanzania kweli, mwenye akili zake timamu, bado ataichagua CCM?!.

Hili ni swali tuu!.

Mimi si miongoni mwa wale wanaodai CCM haikafanya kitu, no!, CCM imefanya mengi mazuri, but it is not enough!, Tanzania tuko hapa tulipo, kwa sababu kuna things CCM should have done, but it didn't, as a result, ndio tuko hapa tulipo!, ila kwa kumsikiliza Magufuli, you can see his genuinity to change things for the better, tatizo ni CCM!.

Hivyo wale wote wenye ufahamu na uelewa wa Tanzania tulipaswa kuwa wapi, hakuna hata mmoja anaweza kuichagua tena CCM, unless yuko kwenye moja ya makundi haya.

 1. Wana CCM wenyewe, ambao CCM ni chama chao, pamoja na madudu yake yote, ili kuonyesha upendo wa kweli, hawa wataichagua tuu CCM, despite all the odds.
 2. Wako wana CCM waliojiunga na CCM sio kwa sababu wanaipenda sana, bali wamejiunga CCM kusaka opportunities za kunufaika, hivyo hawa wataendelea kuichagua tuu CCM ili kulinda matumbo yao.
 3. Kuna watu ni waelewa kabisa wa CCM imefanya nini, na ilipaswa kufanya nini, tena wanaitambua fika kuwa CCM ni li zimwi, ila bado wataichagua tuu CCM kwa sababu hili ndilo zimwi likujualo, halikuli likakwisha. Hawa ni waoga tuu, na uonga ni ujinga fulani!.
 4. Sababu za why CCM should go nitaendelea nazo wuki ijayo, ila ukisoma baadhi ya hoja hapa chini, na bado ukasikia kuwa utaichagua CCM, wewe you seriously need your head to be examined, kwa sababu, utakuwa hauko timamu, bila wewe mwenyewe kujijua, unaweza kujikuta wewe ni kichaa tuu, na kuwa kichaa sio lazima mpaka mtu aokote makopo!.
 5. Kashfa na operesheni saba kubwa zilizotikisa taifa ni pamoja na Operesheni Uhujumu Uchumi, ufisadi katika Mfuko wa Kuwezesha Uagizaji Bidhaa kutoka Nje ya Nchi (Commodity Import Support – CIS) na Kashfa ya Rada. Nyingine ni ufisadi Akaunti ya EPA, kashfa ya Richmond, Operesheni Tokomeza Ujangili na ile ya uchotaji mabilioni katika akaunti ya Escrow.
Kama una muda, take time kufanya rejea
 1. Hii 'Vox Populi' ni 'Vox Dei' Kuhusu 'Jiwe Walilolikataa Waashi ...
 2. Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!.
 3. Yametimia!, CCM Imechokwa!, CHADEMA Ikulu Njia Nyeupe 2015!-
 4. Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target!,
 5. Kuelekea 2015: Ni Mbio Za Magari Kati ya "Mkweche" na
 6. Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa..
 7. Watanzania ni ignorants au tumelogwa? October 25, tutafanya
 8. Kuichagua tena CCM, Je ni kielelezo cha kufanya informed
 9. Edward Lowassa sio lazima yeye tu ndiye awe Rais wetu 201
 10. Hii 'Vox Populi' ni 'Vox Dei' Kuhusu 'Jiwe Walilolikataa Waashi
 11. Kufanya Kosa Sii Kosa, Kosa Kurudia Kosa!. Je Mwaka 2010 Tu
 12. Gesi asili: Is it "day light robbery?!"- watanzania tunaibiwa ..
 13. Topic: Hata ikithibitika Fedha za Escrow ni za Wizi, Nawahakikis
 14. Matokeo ya Serikali za Mitaa: Ni mwanzo wa mwisho wa CCM?!
 15. Escrow: Jee Watanzania ni Ignorants? au Tumelogwa?!.
 16. Kama Kashfa Escrow ni "Richmond", Then, Lowassa Alionewa
 17. Kagoda, Meremeta, Deep Green, Buzwagi, Bandari, nk
 18. Tanzania na tuhuma za rushwa:Kashfa ya fedha za EPA
 19. Meremeta & TANGOLD Revealed!
 20. ZAFANANA: Kashfa Zote Kubwa Zinaungwa na Nyuzi Zile Zile
Nawatakia Jumapili Njema.

Paskali
 
Chakochangu

Chakochangu

JF-Expert Member
2,613
2,000
Mtu kama Mbowe ukimuangalia machoni tu anaonekana sio muaminifu halafu eti ndio umpe uwaziri mkuu kwenye serikali inayoongozwa na fisadi. Acheni mzaha jamani, sumu haionjwi...
Mbowe mashine kubwa,hamtamuweza. Mmejaribu kila mbinu kupitia mamluki wenu wasaliti ili kumng'oa Uenyekiti ikashindikana. Mnajua kabisa aking'oka Mbowe CHADEMA kwisha. Nawaambieni achaneni na Mbowe , huyo ni habari nyingine kabisa.
 
Z

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
13,584
2,000
Mbowe mashine kubwa,hamtamuweza. Mmejaribu kila mbinu kupitia mamluki wenu wasaliti ili kumng'oa Uenyekiti ikashindikana. Mnajua kabisa aking'oka Mbowe CHADEMA kwisha. Nawaambieni achaneni na Mbowe , huyo ni habari nyingine kabisa.
Ni kweli mashine kubwa. Angekuwa mashine ndogo vikao vya chama vingemzuia kuuza chama. One man show ya kuuza chama inaweza kufanywa na mashine kubwa tu...
 
Madenge Origino

Madenge Origino

JF-Expert Member
1,791
2,000
Watanzania wengi tumejielewa baada ya kuwa utumwani kwa muda wa miaka 54 chini ya mkoloni CCM. Tunamshukuru sana Mzee BWM kwa hotuba yake pale jangwani kwenye ufunguzi wa kampeni za CCM. Wengi wetu bado ni Malofa na wapumbavu na kwa mara ya kwanza kabisa ifikapo Oktoba 25, 2015 basi tutaudhihirishia ulimwengu kwamba watanzania wengi ni Malofa na wapumbavu! #mabadiliko
 
Rungu

Rungu

JF-Expert Member
3,935
2,000
Chadema imeshauzwa, ukichagua Chadema unakuwa bidhaa.
Halafu hawa ndio wanaofurahia wakiona vijana wanafagia na kupiga deki barabara ili "viongozi" wapite, na hapo hapo wanadai wanataka kumkomboa mtanzania toka kwa mkoloni mweusi. Wamechanganyikiwa mpaka wameamua kujiita malofa na wapumbavu.
 
Chakochangu

Chakochangu

JF-Expert Member
2,613
2,000
Na aliyekuja na majina matatu mfukoni! How many men show?
 
Chakochangu

Chakochangu

JF-Expert Member
2,613
2,000
Halafu hawa ndio wanaofurahia wakiona vijana wanafagia na kupiga deki barabara ili "viongozi" wapite, na hapo hapo wanadai wanataka kumkomboa mtanzania toka kwa mkoloni mweusi. Wamechanganyikiwa mpaka wanajiita malofa na wapumbavu.
Ile ni fasihi. Unaelewa maana ya kufagia?
 
Z

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
13,584
2,000
Halafu hawa ndio wanaofurahia wakiona vijana wanafagia na kupiga deki barabara ili "viongozi" wapite, na hapo hapo wanadai wanataka kumkomboa mtanzania toka kwa mkoloni mweusi. Wamechanganyikiwa mpaka wameamua kujiita malofa na wapumbavu.
Mtu akitulia kidogo tu kutafakari, hawezi kuchagua Chadema mwaka huu...
 
Rungu

Rungu

JF-Expert Member
3,935
2,000
Ile ni fasihi. Unaelewa maana ya kufagia?
Hukuiona ile picha ya vijana wanafagia barabara na kupiga deki ili Lowassa apite kule Tarime? Mbona unaanza kujibaraguza. Ukombozi hautaletwa na mabwanyenye.
 
Doto Dotto

Doto Dotto

JF-Expert Member
3,042
2,000
wapumbavu na malofa + mbumbumbu watachagua chadema chama cha wanywa viloba na vibaka. but wenye akili timamu watachagua ccm chama kinachotuweka pamoja watanzania bila kujali kabila, dini, wala kanda. ninyi chadema mnaotaka kutuletea ukanda mtasubiri sana
 
TheChoji

TheChoji

JF-Expert Member
1,665
2,000
Kitu nilichogundua ni kwamba Watanzania huwa tunashabikia siasa kama tunavyoshabikia mpira wa miguu! Kwamba mimi kama ni mshabiki wa Man U au Yanga basi natakiwa kuishabikia na kuitetea timu yangu. Ishinde, isishinde, ifanye madudu isifanye mi nitaitetea tu..!
Tunachosahau ni kwamba, tofauti na ushabiki wa MPIRA ambao hauna athari zozote kwa shabiki, ushabiki wa siasa una kila aina ya athari kwa kila Mtanzania. Siasa ndio inaayohamua mustakabali wa maisha ya kila mtanzania. Mimi kwa mfano, huwa siwaelewi kabisa watu wanaoishabikia sisiemu halafu wakirudi nyumbani wanaenda kulala gizani kisa hakuna UMEME! Ila acha tuendelee kuchapika. Ipo siku watu wataelewa tu, kama sio mwaka huu ni baada ya miaka mitano au kumi au ishirini.. Kwasababu ninachoamini mimi sisiem HAITABADILIKA KAMWE!
 
Rungu

Rungu

JF-Expert Member
3,935
2,000
Swali hilo hilo watu werevu wanajiuliza. Hivi kuna mtu na akili zake atachagua fisadi papa awe rais? Labda tuwe tumerogwa na freemasons
Na ndio maana Lipumba aliamua kujitoa na kusema nafsi yake inamsuta. Baada ya hapo aliamua kwenda Maka kuhiji, ili ajitakase roho. Lakini hawa akina Kingunge na genge lake, wasioamini dini bali pesa, wamepofuliwa macho ili wasione kipigo kinachowasubiri. Hizo "nyomi" wanazotengeneza kila kukicha zitawatokea puani mwaka huu.
 
Rungu

Rungu

JF-Expert Member
3,935
2,000
Kitu nilichogundua ni kwamba Watanzania huwa tunashabikia siasa kama tunavyoshabikia mpira wa miguu! Kwamba mimi kama ni mshabiki wa Man U au Yanga basi natakiwa kuishabikia na kuitetea timu yangu. Ishinde, isishinde, ifanye madudu isifanye mi nitaitetea tu..!
Tunachosahau ni kwamba, tofauti na ushabiki wa MPIRA ambao hauna athari zozote kwa shabiki, ushabiki wa siasa una kila aina ya athari kwa kila Mtanzania. Siasa ndio inaayohamua mustakabali wa maisha ya kila mtanzania. Mimi kwa mfano, huwa siwaelewi kabisa watu wanaoishabikia sisiemu halafu wakirudi nyumbani wanaenda kulala gizani kisa hakuna UMEME! Ila acha tuendelee kuchapika. Ipo siku watu wataelewa tu, kama sio mwaka huu ni baada ya miaka mitano au kumi au ishirini.. Kwasababu ninachoamini mimi sisiem HAITABADILIKA KAMWE!
Wewe mwenyewe hapo ulipo unaandika kiushabiki shabiki.
 

Forum statistics


Threads
1,424,590

Messages
35,067,920

Members
538,026
Top Bottom