Maxmizer
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 4,806
- 4,215
Habari wakuu poleni na majukumu ya kila leo natumaini wikiendi ilienda vizuri,
Leo nipo na wakina mama/wanawake nauliza kwanini hampendani, nimefanya utafiti mdogo tu wa kuchunguza kila usafiri wa public/daladala nikagundua hampendani wala kuoneana huruma.
Unakuta kapanda mdada ama mmama mjamzito, mwenye mtoto mdogo ama mzee nilitaraji wao ndio wawe wa kwanza kuonyesheana upendo na huruma kwa kuwapisha kundi hili la watu lakini inakua kinyume kabisa wanakaa kimya na miwani ya tinted wanavaa ghafla kwamba hawajamuona inabidi wanaume ndio wawapishe hawa wajawazito, wazee na wenye watoto wadogo.
Hii si nzuri abadani leo wewe upo sawa ila baadae nawewe utakua mjamzito , utakua na mtoto mdogo,utakua mzee utahitaji kufanyiwa favour hii hii kwa abiria wenzako.
Naomba/Nashauri tuacheni tabia hii pendaneni kama mnavyopendana mkiwa saloon, mkipiga soga, kwenye sherehe zenu na vikundi vyenu.
AHSANTENI