Hivi kwanini wanawake hampendani?

Maxmizer

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
4,807
4,215
Habari wakuu poleni na majukumu ya kila leo natumaini wikiendi ilienda vizuri,

Leo nipo na wakina mama/wanawake nauliza kwanini hampendani, nimefanya utafiti mdogo tu wa kuchunguza kila usafiri wa public/daladala nikagundua hampendani wala kuoneana huruma.

Unakuta kapanda mdada ama mmama mjamzito, mwenye mtoto mdogo ama mzee nilitaraji wao ndio wawe wa kwanza kuonyesheana upendo na huruma kwa kuwapisha kundi hili la watu lakini inakua kinyume kabisa wanakaa kimya na miwani ya tinted wanavaa ghafla kwamba hawajamuona inabidi wanaume ndio wawapishe hawa wajawazito, wazee na wenye watoto wadogo.

Hii si nzuri abadani leo wewe upo sawa ila baadae nawewe utakua mjamzito , utakua na mtoto mdogo,utakua mzee utahitaji kufanyiwa favour hii hii kwa abiria wenzako.

Naomba/Nashauri tuacheni tabia hii pendaneni kama mnavyopendana mkiwa saloon, mkipiga soga, kwenye sherehe zenu na vikundi vyenu.

AHSANTENI
 
Yanii wamama huwezi kuta kampisha mzee au mjamzito au mgonjwa akae..!! Kamwe... Sema saa nyingne ina keraa unaweza mpisha mmama akae na ujauzito wakee au na mtoto afuu Hata Kusemaa Ahsanteee hakunaaaa na hapo.ukute mnaenda mbali sana..!! Huwa nakerekaa piaaa sana tuuu... Wanadhani sijui ni wajibu wetu kuwapishaaa... Ndo maana saa nyingne huwa najikausha... Wabibi lazima aseme ahsante...shida wamama yanii!!
 
Mi nionavyo kwa kuwa mmeshatujua basi nyie wanaume jitahidini kuwapisha wakae nadhani itasaidia na kufanya kutokupendana kwetu kusionekane. Ila kusimama saa nyingine. Mmh.

Pia nikwambie tu sio kwenye madaladala pekee hata makazini, mitaani, kwenye biashara yaani sehemu zilizo nyingi wanawake hatupendani kwa sababu tulio wengi tuna roho za wivu na hiyo ndio sababu kuu yaani ni kumi kwa mmoja wenye kuona mwanamke mwenzangu kafanikiwa namimi nichape kazi nimfikie tulio wengi tunawaza aharibikiwe.

Hivyo tusameheni tu saa nyingine.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom