Hivi kuna ukweli wanawake wazuri sana huwa hamnazo kichwani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kuna ukweli wanawake wazuri sana huwa hamnazo kichwani?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by M'Jr, Jan 4, 2012.

 1. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Nimekuwa naisikia sana hii kwamba wanawake wazuri sana huwa mara nyingi hazimo sana kichwani. Hii ni kwa dunia nzima, kwa mfano ukisoma novel nyingi za waandishi wakubwa wa novel duniani wanapomportray mwanamke mzuri (Kwa wao wa kizungu) huwa wanamalizia na dumb. Lakini hii hasa imekuwa inawaangalia zaidi models na wale wanaoingia kwenye mashindano ya urembo, hivi kuna ukweli juu ya hili?
   
 2. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,980
  Likes Received: 6,632
  Trophy Points: 280
  hahahahaaaa....!!. Mkuu unataka kusema kichwani wana mapepo au?. Mia
   
 3. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Yaani inadaiwa kuwa uwezo wao wa kufikiri, kuchambua na kuamua uko chini sana mkuu
   
 4. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  SI kweli, mara nyingi sana wanawake wazuri, na akili zao zinakuwa nzuri...Lakini niliwahi kuona mmoja wao mzuri lakini hana hana vile.
   
 5. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Hazimo kicwani aje? Labda usemw wanaume kwa wanawake wazuri hazimo kichwani.maana wengine tu na mivuto yetu ya kuungakuunga tumeweza kupata
  a
  b
  c
  d
  ndo useme hazimo kichwani? Fafanua labda
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  KWANINI usifanye kautafiti kadogo kwa warembo wetu wa hapa Bongo?
  Na unaposema Wanawake wazuri unamaanisha Ma'Miss'au hadi wa Uswazi?
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Jan 4, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 160
  Kwanza uzuri wa mwanamke ni nini?

  Kwa mzungu mzuri, mwembamba, athletic, blond hair n.k
  Msukuma mzuri mweupe, mnene, meno meupe, anyejua kulima kikakamavu.
  Mkurya mzuri anayejua kukamua na kuchunga ng'ombe, kakeketwa.

  Na hizo akili unazoongelea ni kwenye kitu gani?
  Na ni uzuri upi unaoongelewa hapa?
   
 8. P

  Pure nomaa JF-Expert Member

  #8
  Jan 4, 2012
  Joined: Dec 10, 2011
  Messages: 1,051
  Likes Received: 1,077
  Trophy Points: 280
  Inawezekana mkuu.Hakuna kizuri kinachokosa kasolo
   
 9. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #9
  Jan 4, 2012
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Lina ukweli, lkn si kwa wanawake wazuri bali wanawake warembo. Lakini nalo lategemea malezi alopata utotoni. Kama alilelewa kama Princess na kusifiwa na wazazi wake kwa urembo hata akikohoa basi hicho kichwa hakiwi na kitu. Wa pili kumuharibu huwa ni wanaume. Mwanamke anapobaini kuwa kuna rundo la wanaume linamhusudu akili yake huamia huko na hakuna kingine anafanya zaidi ya kuandaa mbinu na mwonekano wa ku-draw attention za wanaume.

  Ukitaka kujua upande wa pili, angalia wengi wa wanawake waliofanikiwa kwa juhudi zao (ambao hawakuwa promoted kwa hisia za wanaume) ni wale wasio warembo. Hawana muda na suala la kujipara kwa kuwa wanaamini wana asset nzuri zaidi kichwani. Ukiona kitoto kirembo cha kike kinasukuma mkoko wa bei mbaya, usije ukadhani labda maisha yake yana furaha 100%, upo uwezekano kanamegwa na m'babu kama Mh.wa kusinzia mjengoni lkn wkt wa mambo kanalazimika kutabasamu ili kasikatiwe supply ya matanuzi.
   
 10. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #10
  Jan 4, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Inategemea mkuu! Uwezo wa mtu kufanya/kuamua/kufikiri/kuchambua mambo unategemea na kiwango cha aliyonayo shule ingawa kuna special cases ambazo hazikosekani. Kutokana na hiyo sababu, wanawake wengi (siyo wote) wazuri wanakuwa wanayo mentality ya kuwa kwa kuwa wao ni wazuri hakuna haja ya kujisumbua saaana kunoa bongo zao huku mtaji wao mkubwa ukiwa ni huo uzuri.

  Kwa hiyo hapa 'The principle of equilibrium' inakuwa inafanya kazi yake kiaina.
   
 11. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #11
  Jan 4, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,231
  Trophy Points: 280
  inawezekana, maana wanaume wazuri wote vichwamaji, handsome boys zero kabisa, inawezekana na warembo ikawa hivyo.

  ila uzuri wa mtu uko machoni mwa mtu, sasa sijui unaongelea uzuri gani
   
 12. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #12
  Jan 4, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  U r exceptional, kuwapata kama wewe its hard kwasababu ni 1:100...........Lol!
   
 13. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #13
  Jan 4, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Ni wanadamu wachache saana walizaliwa na wakajitune kua na akili ya kufikiria na kuzingatia yalo ya muhimu bila kufundishwa na familia ama jammi husika ambayo anatoka. Sio maneno mazuri ulotoa, ila tu bahatai mbaya saana yana ukweli ndani yake. Mtoto wa kike ama wakiume anapokua toka mtoto ni mzuri mno.... Ndio mara nyiingi saana hushika hatamu ya kum define as a kid and youth.

  Watu wakiumuona ni huyu mtoto mzuri jamani.... kila apitako na kila amuonae.... Hii ni mbaya saana for inamjenga akili mtoto (kwa bahati mbaya yupo too young kujua madhara) aendelee kuangalia uzuri wake kama vile ndo kitu cha msingi na cha maana katika maisha, hasa katika kupata atakacho ama kufika atakako. Mpaka leo hii sio siri bana kua mnapokua katika jamii katika huduma mbali mbali yule ambae ni mdada mzuri saana OR yule kaka hendsamu na mtanashati hua wapendelewa katika kupata huduma. It is nature but ndo ukweli huo.

  Madhara yake inakua sasa kua mara nyingi hupata vitu kwa urahisi saana.... For instance kupendelewa mtaani akiwa mtoto mdogo, katika kundi zima la watoto labda yeye atapewa pipi ndo agawe na kwa wenzie, akiwa shuleni adhabu sio kali kivile kama hilo kosa afanye mwingine.... binti akienda interview na mwenzie hata kama hayupo bright kama opponent aweza pata kazi na cheo kupanda mara moja.... na vitu vingine kibao.... Hio in some way yapunguza ufikikiri wa ubongo kupata majibu ama kuweza find ways of fighting kupata utakacho.
   
 14. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #14
  Jan 4, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Utafiti nimewahi kuufanya kwasababu nimewahi kuwa kwenye sehemu ambayo nilikuwa nadeal moja kwa moja na hawa mabinti (Mamiss na wanamitindo) well kwa wale niliokuwa nadeal nao 80% walikuwa wanaongozwa na that thing between their legs na ni 20% tu waliokuwa wanatumia vichwa vyao na hata maisha yao kwa sasa yako tofauti na hao wengine
   
 15. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #15
  Jan 4, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Achana na reference za wasukuma na wakurya wa kwetu huku, ndio maana nimetoa category mbili ambazo wote tutakuwa tunaongea the same language coz ukianza kucategorize kwa mtindo wako hatutafika mwafaka (wanamitindo na wale walioko kwenye mashindano ya urembo)
   
 16. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #16
  Jan 4, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Wanasema wanawake warembo /wazuri huwa hawana mengi mazuri ya kufurahisha,unaweza kuwa naye ila usi-enjoy company yake zaidi ya sura yake au umbo lake tu.
   
 17. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #17
  Jan 4, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Sio kweli, wapo wazuri wa sura moyo na akili vile vile wamejaaliwa.
   
 18. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #18
  Jan 4, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Okay so jamii ndio inawatengeneza kuacha kufikiria mambo mengine na kukoncertrate na uzuri wako kama strength yao kuu. Unajua kuna ka mfano watu huwa wanapenda kukatumia sana, ukienda pale chuo kikuu cha Dar es salaam kitengo cha uhandisi kuna wasichana ofcourse lakini huwa inadaiwa idadi kubwa hawana mvuto na ndio sababu inayopelekea wao kutumia strength yao kubwa ambayo ni vichwa vya
   
 19. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #19
  Jan 4, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Mi nakubaliana na wewe kabisa, lakini hebu weka mizani kati ya hao unaowasema wana kila kitu na wale wenye mapungufu, na ndio maana nikasema wale walio wengi
   
 20. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #20
  Jan 4, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180


  Take note kua haina maana kua wanawake wooote wazuri ni vilaza..... Kumbuka kua masomo yanayompleka mtu Chuo ni yale ambayo tayari alishajenga foundation toka huko nyuma.... kama ni Science, Arts, Economics na the like. Hilo la Uhandisi pia lina ukweli ndani yake.... Yale masomo hayataki lele mama, kwamba uende ukashinde wajitazama kwenye kioo... Uende ukafanye shopping kuangalia which clothes will look sexy on you.... yoote hio ikiwa imesukumwa na the attention anayopokea katika jamii hasa from the opposite sex. Unapokua huna walezi/wazazi wakukuweka katika mstari kwa kukukazania umuhimu wa kujenga future na kwamba beuty is there to stay uwe mvumilivu... Yaweza kabisa haribu mwelekeo wa one's future.

  Wanawake woooote uwe mzuri ama mbaya twapenda sifa (mradi zisikithiri) toka from the opposite sex once in a while katika jamii yako... hasa zilo postive. Na twajua jinsi binti anapokua mzuri pale anapokua anavosumbuliwa na vijana huko mtaani kwa kutoongozwa na kusifiwa ni mzuri. In some ways hii yaweza mpunguzia concetration katika masomo ukifanananisha na yule ambae hasumbuliwi kabisa ana nafasi kubwa saana katika masomo than the other.... How ever hii sio absolute.
   
Loading...