TUONGEE KIUME: Sisi tuko hivi, wanawake wanataka tuwe vile

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,447
Ukweli ni kwamba, hutakiwi kujichosha kuwa mwanamume anayemtaka mwanamke hatofanikiwa. Na sio wewe tu, tangu dunia hii ianze hakuna mwanaume aliyefanikiwa kwenye hilo.

Wakati mwanamume anataka mwanamke ambaye labda anampenda na kumuheshimu tu, wanawake wenyewe wanataka mwanaume mwenye mwili wa mazoezi, ambaye akichomekea anapendeza.

Mwanamume anayejua kupika ili wikiendi yeye akiwa anaangalia tamthilia, mwanamume aingie jikoni ampikie, amuandalie mezani na kumlisha huku akipooza chakula kwa kukipuliza kwa mdomo.

Pia, mwanamume huyo huyo mwenye mwili wa mazoezi na anayejua kupika awe ‘handsome’ ili wakitoka wakipiga picha aweze kupost kwenye mitandao, siye mwenye sura kama nyuma ya sufuria hatuwezi kupendeza hata picha zikihaririwa kwa kompyuta. Kisha huyo huyo ‘handsome’ anatakiwa awe na kazi nzuri. Awe kwenye ofisi moja kali ‘full’ kiyoyozi hapo mjini, Posta.

Na isiwe kazi nzuri tu, pia awe na pesa zinatosha kununua gari nzuri, kuishi kwenye nyumba nzuri. Pia, pesa za kutosha kutoka kila wikiendi. Bado unatakiwa uwe hupendi mpira, huvuti sigara, hunywi pombe , huna marafiki au kama unao basi wachache na sio wale wa kufuatana nao mara twende baa, sijui twende Taifa kwenye mechi ya Simba Yanga, hutakiwi.

Pia, uwe unapenda muziki, unajua kucheza sana na kuimba angalau kwa mbali. Pia, usiwe na mtoto au kama unaye usiwe unawasiliana na mama yake. Wanawake ndiyo wanataka mwanamume wa aina hii.

Ukisoma vigezo vyote hivi utagundua kuwa kwa neno moja wanawake wanataka mwanamume mzuri, kama ambavyo sisi pia tunapenda mwanamke mzuri. Lakini tofauti yetu na wao ni kwamba wenyewe wanachagua kwa kuangalia vitu vidogo vidogo sana ambavyo nikisema havina maana sijui kama hawataona nawatukana.

Wengine wanaweza kujitetea kwamba vigezo hivyo sio vya mwanamke, ni vya msichana. Ni kweli sio uongo, lakini kabla ya kuwa mwanamke, wanawake wote huwa wasichana. Na katika kipindi hicho ndipo wanawake wanafanya uchunguzi kwa wanaume kana kwamba wanataka kuajiri askari.

Matokeo yake wanashindwa kupata mwanaume ‘handsome’ mwenye hela, gari nzuri, nyumba nzuri, anayejua kupika, asiyekunywa pombe, kuvuta sigara, asiyekuwa na mtoto na mwenye marafiki wachache au asiyekuwa na marafiki kabisa.

Huwezi kupata mwenye sifa hizi zote kwa pamoja kwa hiyo wakishaanza kuona usichana wao unafifia na sasa wanaelekea kwenye kuwa wanawake ndipo wanaamua kuokota yeyote anayepita mbele. Wakishafikia hatua ya kuokota hapo ndiyo sisi wenye vitambi, tusiokuwa na kazi ya kueleweka, walevi, wavuta sigara, wenye watoto na tusiokuwa na hela tunapewa nafasi.

Sio mbaya kupenda vitu vizuri, lakini kufikiri unaweza kupata mwanamume ambaye ni mkamilifu ni kujidanganya. Sisi ni binadamu sio malaika, tumeumbwa kwa msingi wa kuchanganya mabaya na mazuri.

Credit: Mwananchi
 
Hizi habari sijui Mwanamke kwa Mwanaume sijui imefanyaje na imekuwaje haziwezi kuisha,cha msingi ni kuwa haya maisha tunapita ila neno Mwanaume na Mwanamke litabaki kuwapo tu,ishi maisha yako ya kila siku au ya boreshe haya maisha unayo ishi kila siku,matamanio mapya kila siku yanazaliwa hivyo ni ngumu kuendana nayo mengine ni kuyaacha yapite tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata kwa wanaume na wanawake, mtu anachagua anahisi tayari lakini mkianza kuishi ndio unagundua huyu mwenza wangu mbona ni kama mwehu, kitu kidogo atajisema masaa mengi, au unaona pisi kali kumbe inanuka mdomo , nachotaka kusema ni kwamba elimu ya mahusiano kutotolewa imekua ni tatizo sana na ndio maana mahusiano mengi hayadumu udhaifu uko pande zote, UVUMILIVU Haupo kwa siku hizi kwani teknolojia inatukimbiza sana kwa uongo
 
Hapo ulipokaa mwana JF , fikiria katika akili yako zamani mtoto wa kiume alichaguliwa binti wa kuoa kijijini kwao, kwahivo hata kama yuko mjini atarudi nyumbani kuoa tu, atapata mke wanaeongea lugha moja, wanachangia mila, desturi na tamaduni, vigezo kwa pande zote ilikua ni kwao mwanamke au mwanaume 1. Wasiwe na asili ya uvivu, 2. Wasiwe ni wezi au majambazi 3. Wasiwe na magonjwa ya kudumu kama ukoma 4. Wasiwe wachawi au wawanga 5. Wasiwe na tabia za kudhulumu hapo kijijini

Hivo ni baadhi ya vigezo vya zamani.
Jenga picha kijana anaitwa jackson na binti anaitwa neema, tayari wanayaanza maisha kijijini wanaanza kutafuta maisha pamoja, fikiria wanavuka mto wa kijiji kwenda shambani kusaka mali, jackson kavaa suruali ya mtumba na shati chakavu mikono mirefu chini kavaa matairi ya gari au katambuga, mkononi kashika panga, na neema kajifunga kanga yake ya kawaida kabeba dumu la maji ya kunywa.

Hapo ndio safari ya kusaka mali inapoanza na ndio ulikua utamaduni, na walifanikiwa kujenga familia bora na uchumi ulikua maana kila wakivuna wanaweka malengo, wengi walianza kujenga nyumba ya bati hata vyumba viwili, misimu mingine walijitahidi wakivuna waanzishe biashara ya duka kijijini hapo, unaona hawa watu uchumi wao unakua kila mwaka hadi wanafikia malengo yao,
 
Hata kwa wanaume na wanawake, mtu anachagua anahisi tayari lakini mkianza kuishi ndio unagundua huyu mwenza wangu mbona ni kama mwehu, kitu kidogo atajisema masaa mengi, au unaona pisi kali kumbe inanuka mdomo , nachotaka kusema ni kwamba elimu ya mahusiano kutotolewa imekua ni tatizo sana na ndio maana mahusiano mengi hayadumu udhaifu uko pande zote, UVUMILIVU Haupo kwa siku hizi kwani teknolojia inatukimbiza sana kwa uongo
Point
 
Kwa hiyo vigezo kwa pande zote vimebadilika kutokana na teknolojia kubadilika, lakini kwa kijana wa sasa anamaliza degree ana miaka 27 , bado hawezi kujitegemea, anatafuta kazi miaka 5 nayo hapati kazi ya kueleweka hapo ana miaka 32 , bado yuko kwa wazazi, anafika 35 ndio anachanganyikiwa maana kama alikua baharia ana watoto 3 nje huko nao hawatunzi, anakutana na binti wa tiktok keshakua singo maza na kajigongea 33 miaka bila ndoa, wanaplan chap chap kuoana kweli wanafunga ndoa fasta halafu kamwe hawawezi kumaliza miaka miwili ndani ya ndoa maana wote wana stress za maisha hivo ndio hao mara wameuana, mara wamechomana moto, kwahiyo ndoa inakua sio maisha isipokua ni vita na vurugu sana
 
Pamoja na yote hayo bado kuna wanawake wenye akili na wenye uwezo wa kujenga familia imara kabisa na watulivu wapo, hata wanaume imara ambao wanajimudu kusimama kama wanaume wapo na wanaweza kuwa Baba bora hivo kijana wa kike au wa kiume angalia malengo yako na ulienae mwelekeze na muoneshe kua tukifanya hivi na vile kwa umoja na upendo tutafika pale mhakikishie kabisa huyo binti naamini akiona mwanga atatulia tu na unaweza kubadili mwenendo, ukajenga familia bora ( back to roots) angalia mambo muhimu tu,
 
Mtoa maada umeangalia upande wa mabinti kutupa lawama na vigezo vingi kwa wanaume, unasahau kwa sasa hata wanaume vigezo nao ni vingi anataka lazima binti awe na tako kubwa kama behewa, anaacha mpenzi wake aliemvumilia huko kwenye dhiki kisa anataka warembo haswa hapo ndio kijana anaanza kupotea njia rasmi
 
Hizi habari sijui Mwanamke kwa Mwanaume sijui imefanyaje na imekuwaje haziwezi kuisha,cha msingi ni kuwa haya maisha tunapita ila neno Mwanaume na Mwanamke litabaki kuwapo tu,ishi maisha yako ya kila siku au ya boreshe haya maisha unayo ishi kila siku,matamanio mapya kila siku yanazaliwa hivyo ni ngumu kuendana nayo mengine ni kuyaacha yapite tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Well noted
 
Kila mtu hutaka "the best"
Hata wewe pengine unataka mwanamke mwenye tako kubwa na awe na akili na muaminifu ...na asiende hela.....
Je inawezekana???..
Mwisho WA siku kila mtu huja Ku "settle" sehemu ambayo sio lazima aliitamani hapo mwanzo
 
Back
Top Bottom