BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 422
- 1,049
Moja ya jambo ambalo inawezekana changamoto ni miundombinu au labda ni vyombo vyetu vya usafiri, bado huwa nashindwa kuelewa vizuri, yaani ikitokea mvua imenyesha kidogo tu kwenye Jiji la Dar es Salaam hasa maeneo ya town, lazima foleni barabarani ziibuke kwa kasi.
Najiuliza, hivi tatizo ni miundombinu yetu kuwa haina uwezo au vyombo tunavyotumia kusafiria ndiyo vibovu, kiasi kwamba mvua ikinyesha vinavuja au vinaharibika, mfano leo imenyesha mvua kidogo tu lakini foleni hadi watu wanachelewa kwenye mishe zao.
Huu mji kuna vitu inabidi vifanyike, hili siyo jambo zuri kiuchumi na siyo kitu kizuri kwa faida ya Taifa.
Nasema hivyo kwa kuwa Dar ndio Mji mkubwa kibiashara, sasa kunapokuwa na foleni za kinomanoma kama hivyo, unadhani inamaanisha nini kiuchumi? Tunafeli wapi?