Hivi kuna maandamano yoyote yaliyoitishwa Tanzania juu ya Serikali kisha yakafanikiwa?

Na ukiangalia vizuri hata hivyo vizazi vinaweza visiwe na huo uwezo kwa sababu wengi wa watanzania wanafundisha watoto wao kudeal na mambo ya msingi na yenye tija kwao na kujiepusha na vitu ambavyo vinaweza kuwaharibia maisha yao. Sidhani kama kuna mzazi wa Kitanzania anamfundisha mtoto wake siku Serikali ikifanya hivi, unaniona mimi nilichofanya? Nimeingia barabarani kuandamana na kupinga hilo, na wewe unatakiwa uwe hivyo, badala yake wapo wanaowafundisha watoto wao wakae mbali na hayo mambo kwa kutolea mifano ya yanaowakuta baadhi ya watu. Kwa mfano, mzazi anaweza kumwambia mtoto wake, “Mwanangu usije jifanya mjuaji mbele ya mamlaka kwa sababu wazazi wako ni maskini. Fikiria kama yanakukuta kama yaliyomkuta Lissu, unafkiri utabaki hai yakikukuta wewe? Tafuta maisha achana na mambo yasiyo na faida kwako utaishia jela au uuliwe”.
Uko sahihi sana mkuu
 
Mimi sifahamu, ila tunachohitaji ni majibu ya hoja zinazowafanya watu watake kuandamana....

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Jikite kwenye mada
 
Mbona ni juzi juzi tu tumetoka kushuhudia Maandamano ya BAWACHA au mna amnesia?
BAWACHA maandamano gani? Hata UVCCM pia huwaga wanaandamana. Mi sihesabii yale kama maandamano kwa sababu kwanza hayakuwa na ajenda fulani. Mi nachkulia ile kama “Road Walk” tu waliamua kunyoosha miguu. Sidhani kama una umri mdogo wa kutokufahamu maandamano ya kushinikiza Serikali kufanya jambo au kulaani kilichofanywa na Serikali.
 
Ajenda ilikuwa ni KATIBA MPYA.
Narudia tena, sijaona maandamano pale. Ile ni road walk ambayo malengo ilikuwa ni kuelekea mahali ambayo walikuwa wanaenda kukutana kwa ajili ya mkutano. Maandamano hayana hotuba wala speech, ni kukutana mahali fulani, tunaelekea mahali fulani kupitia barabara fulani. Unaandamana kuhusu katiba mpya wakati unaandamana kuelekea ukumbi wa kufanyika mkutano ambako Hakuna hata katibu anaehusiana na masuala ya katiba? Wangeandamana kuelekea hadi Wizara ya katiba na sheria ningejua ni maandamano kweli.
 
Wakuu na wajuzi wa mambo naomba kuuliza swali.

Binafsi tangu nimepata akili zangu, sijawahi ona hata maandamano moja iliyoitishwa ama kuratibiwa kwa ajili ya kuishinikiza Serikali ama kulaani jambo fulani lilifonaywa na Serikali kisha hiyo maandamano ifanikiwe. Hapa sizungumzii maandamano ya kina Mange Kimambi na diaspora wanaoandamana kwenye balozi za Tanzania zilizopo nchi za nje ila nazungumzia maandamano kama maandamano yaliyoshirikisha wananchi hapa Tanzania na kuteka mji fulani au miji fulani ndani ya Tanzania. Mara ya mwisho kuskia joto ya kufanyika maandamano nchi nzima niliishia kuona maandamano kwenye Twitter na Facebook lakini barabarani sikuona mtu.

Vipi kuna yeyote mwenye kumbukumbu ya maandamano kubwa kutokea hapa Tanzania bara (achana na ya Zanzibar kwa sababu nilishaona mara kadhaa wananchi kufanya maandamano licha ya polisi kuonesha kuzuia) na yakafana?
Sahivi utayaona watu wamechoshwa na huu utawala dhalimu
 
Watanzania hawakufunzwa uhjinga wa vurugu zisizo na msingi.

Imagine ukaandamane Kwa sababu Lisu amekaidi amri ya Polisi,wewe unaweza?
Sio watanzania hawakufunzwa, maana hakuna aliyefunzwa kuwa kondoo, bali kizazi hiki cha watanzania kilipandikizwa uoga, na huo uoga umeendelea hadi sasa. Lakini taratibu kizazi hiki kinaanza kuonyeshwa kuwa uoga wao dhidi ya kigenge kidogo cha wala cake ya taifa ndio hasara yao.

Tutafika huko lazima, maana tawala zinazokaa madarakani kwa shuruti, hutolewa kwa machafuko ama mapinduzi ya kijeshi tu.
 
BAWACHA maandamano gani? Hata UVCCM pia huwaga wanaandamana. Mi sihesabii yale kama maandamano kwa sababu kwanza hayakuwa na ajenda fulani. Mi nachkulia ile kama “Road Walk” tu waliamua kunyoosha miguu. Sidhani kama una umri mdogo wa kutokufahamu maandamano ya kushinikiza Serikali kufanya jambo au kulaani kilichofanywa na Serikali.
Arusha kulifanyika maandamano kugomea meya wa mchongo hadi watu watatu wakafariki, matokeo ya maandamano yale ulipofanyika uchaguzi mwingine haikuwezekana kuchakachua tena, na Arusha wakapata meya wa upinzani.
 
Mimi sifahamu, ila tunachohitaji ni majibu ya hoja zinazowafanya watu watake kuandamana....

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Waraka
 
Tofauti yake ni nini?
“PROTEST” ni uelezeaji au tamko la pingamizi la kutoidhinishwa au kutokubaliana ama kupinga jambo ambalo mtu hana uwezo wa kuzuia au kuepuka.

“PROCESSION” ni kikundi cha watu au vyombo vya moto kutembea barabarani au njiani na kwa utaratibu maalum, na mara nyingi huwa kama sehemu ya kuidhimisha sherehe.

Nipe tofauti yako unayoifahamu wewe, mtaalamu.
 
Back
Top Bottom