Kwanini maandamano yoyote Tanzania yanatafsiriwa ni umwagaji damu hata yawe ya kupinga ufisadi wa mali za umma?

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,272
2,033
Wadau nawasabahi. Chama kikuu cha upinzania Tanzania Chadema kimetangaza kufanya maandamano ya amani tarehe 24 Januari 2024 ili kufikisha hoja zake kwa serikali na CCM ili ziweze kutekelezwa kwa haraka kwani serikali na ccm zimekuwa au hazitaki kutekeleza.

Baada ya tangazo hilo vyombo vya habari na baadhi ya watu ktk mitandao ya kijamii wamekuwa wakiilaumu chadema kuwa inataka kumwaga damu.

Najiuliza kama chadema wamesema wanafanya maandamano ya amani hiyo damu inamwagikaje? Nani atafanya vurugu ktk hayo maandamano hata damu imwagike?

Binafsi naamini vyombo vya habari na baadhi ya watu wanatumika kuyatafsiri hayo maandamano kuwa yatakuwa na umwagaji damu kama propaganda za kuwatisha wananchi wasiandamane.

Kwa uzoefu wa nchi hii vurugu za maandamano huanzia pale vyombo vya ulinzi na usalama vinapotumia nguvu kubwa kuyazuia badala ya kuyalinda na kuhakikisha yamemalizika salama kwa mujibu wa sheria kwani haki ya kuandamana ipo kwa mujibu wa katiba ya nchi. Kwa mfano maandamano yaliyofanyika wakati wa uchaguzi wa marudio jimbo la kinondoni na kumuua binti akwilina ni jeshi la polisi lililofyatua risasi na kupelekea yale mauaji. Wakati waandamanaji walikuwa hawana hata fimbo mikononi.

Ushauri kwa CCM iache siasa za kizamani za kuwatisha wananchi na kueneza hofu na uogo kwa waandamanaji kuwa maandamano yatamwaga damu. Atakayesababisha damu imwagike ni yule atakayeyazuia haya maandamano kwani ni ya amani.

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Wadau nawasabahi. Chama kikuu cha upinzania Tanzania Chadema kimetangaza kufanya maandamano ya amani tarehe 24 Januari 2024 ili kufikisha hoja zake kwa serikali na CCM ili ziweze kutekelezwa kwa haraka kwani serikali na ccm zimekuwa au hazitaki kutekeleza...
Kama ni maandamano ya amani tunafanyaga kila siku kwenda kazini na kurudi, tunajaa kwenye magari na mabus na mwendokasi na boda boda na kwa mguu: hayo ni maandamano ya amani hatumgusi mtu. Hii ya sasa ni vurugu na matusi na kero za njia, haikubaliki.
 
Bawacha walifanya 2023
 
kiongozi anayejihami kwa polisi na wanajeshi ni kiongozi dhaifu, wenzake wanakuja na hoja wao wanaleta polisi?
kazi ya polisi ilitakiwa kuyalinda maandamano na kuzuia uvunjwaji wowote wa sheria kwa waandamanaji hao, ikiwemo vibaka kujichanganya na kuibia watu. ila kutumia polisi kuwatisha wanasiasa wenzaki halafu kesho unasimama kanisani na kusema uombewe, ni UZWAZWA... ni muda wanasiasa wajue nchi ni mali ya kila mtanzania, na demokrasia inasema wengi waamue na wachache wasikilizwe, sasa kama lichama likubwa la ccm linaogopa movement za amani za kichama kinachojifia CHADEMA, ni aibu hata kujisifu na mama yenu
 
🌈
 
Hawako tayari kujua ukweli kuhusu hisia za wananchi. Wanajua wakikubali maandamano yanaweza kuwa na watu wengi, hivyo kuliko wajue ukweli wa watu wengi, ni bora wapige marufuku.

Hawa nawafafanisha na mtu anayeogopa kupima ukimwi hata kama ana dalili nyemelezi, maana anajua akifahamu ukweli atabaki na mfadhaiko, ni bora asiujue ukweli aishi kwa matumaini.
 
Kama ni maandamano ya amani tunafanyaga kila siku kwenda kazini na kurudi, tunajaa kwenye magari na mabus na mwendokasi na boda boda na kwa mguu: hayo ni maandamano ya amani hatumgusi mtu. Hii ya sasa ni vurugu na matusi na kero za njia, haikubaliki.
Kuna baadhi ya majibu humu ndani kwa kweli yanatia kichefuchefu kabisa. Ifike mahali tuache kuabuse hii forum. Sio kila mkusanyiko ni maandamano, maandamano ni mkusanyiko maalum wenye lengo mahususi; kusifia, kupongeza, kukemea, kutoa tahadhali, kupeleka ujumbe fulani n.k. Na yanakuwa organized na theme inakuwa shared pamoja na ratiba. Mwisho wa maandamano lengo kuu linatolewa ufafanuzi.

Kama mtu huna hoja ni bora unyamaze, kuliko kuchafua hali ya hewa. Kwa kifupi tunasafari ndefu kufikia kujitambua, na viongozi wanalijua hilo ndio maana hawaogopi.
 
Wadau nawasabahi. Chama kikuu cha upinzania Tanzania Chadema kimetangaza kufanya maandamano ya amani tarehe 24 Januari 2024 ili kufikisha hoja zake kwa serikali na CCM ili ziweze kutekelezwa kwa haraka kwani serikali na ccm zimekuwa au hazitaki kutekeleza.

Baada ya tangazo hilo vyombo vya habari na baadhi ya watu ktk mitandao ya kijamii wamekuwa wakiilaumu chadema kuwa inataka kumwaga damu.

Najiuliza kama chadema wamesema wanafanya maandamano ya amani hiyo damu inamwagikaje? Nani atafanya vurugu ktk hayo maandamano hata damu imwagike?

Binafsi naamini vyombo vya habari na baadhi ya watu wanatumika kuyatafsiri hayo maandamano kuwa yatakuwa na umwagaji damu kama propaganda za kuwatisha wananchi wasiandamane.

Kwa uzoefu wa nchi hii vurugu za maandamano huanzia pale vyombo vya ulinzi na usalama vinapotumia nguvu kubwa kuyazuia badala ya kuyalinda na kuhakikisha yamemalizika salama kwa mujibu wa sheria kwani haki ya kuandamana ipo kwa mujibu wa katiba ya nchi. Kwa mfano maandamano yaliyofanyika wakati wa uchaguzi wa marudio jimbo la kinondoni na kumuua binti akwilina ni jeshi la polisi lililofyatua risasi na kupelekea yale mauaji. Wakati waandamanaji walikuwa hawana hata fimbo mikononi.

Ushauri kwa CCM iache siasa za kizamani za kuwatisha wananchi na kueneza hofu na uogo kwa waandamanaji kuwa maandamano yatamwaga damu. Atakayesababisha damu imwagike ni yule atakayeyazuia haya maandamano kwani ni ya amani.

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
Kimsingi kinachoifanya ccm/serekali waogope maandamano ni kwa kuwa wanajua wamechokwa, hivyo kitendo chochote Cha maandamano wanahofia turnout ya waandamanaji itaonyesha hisia za wananchi na wingi wao. Na wanajua ni kutoa political mileage kwa wapinzani wao.

Hivyo hawataki kutoa nafasi ya wengine kuonekana kukubalika hasa kwa ajenda zao ambazo ni hatari kwao, na wanajua pia wakitumia mabavu kuzuia maandamano hayo, wanajitengenezea chuki kwenye jamii. Ifahamike ccm wanataka kuonekana kwa wananchi na jumuia ya kimataifa kuwa ni wema. Na wakati huohuo hawako tayari kufanyia kazi madai halali ya wapinzani wao.

Ifahamike wanauza ulaghai uitwao 4R, ambayo ni ulaghai kama ulaghai mwingine. Hivyo hawako tayari picha hiyo ya kilaghai iharibike kwenye macho ya wananchi, na Dunia kwa ujumla, na wanajua fika maandamano haya yakifanyika hata kwa uchache, yataharibu picha hiyo ya kilaghai waliyoitengeneza.

Cc: Nguruvi3, Pascal Mayalla, Bams, proved,
 
huwezi kutatua tatizo kwa kutegemea watu wale wale waliotengeneza tatizo.

sasa unataka watu wale wale waliotengeneza sababu za nyie kuandamana ndio wawape nyie kibali cha kuandamana?.

Matatizo ya Tanzania yataishi kwa mapinduzi ya kiraia yatakayoiondoa CCM na nchi kurudi kwenye mikono ya wananchi wenyewe watakaoamua hatma ya nchi yao.

Shetani hana rafiki.
 
Wadau nawasabahi. Chama kikuu cha upinzania Tanzania Chadema kimetangaza kufanya maandamano ya amani tarehe 24 Januari 2024 ili kufikisha hoja zake kwa serikali na CCM ili ziweze kutekelezwa kwa haraka kwani serikali na ccm zimekuwa au hazitaki kutekeleza.

Baada ya tangazo hilo vyombo vya habari na baadhi ya watu ktk mitandao ya kijamii wamekuwa wakiilaumu chadema kuwa inataka kumwaga damu.

Najiuliza kama chadema wamesema wanafanya maandamano ya amani hiyo damu inamwagikaje? Nani atafanya vurugu ktk hayo maandamano hata damu imwagike?

Binafsi naamini vyombo vya habari na baadhi ya watu wanatumika kuyatafsiri hayo maandamano kuwa yatakuwa na umwagaji damu kama propaganda za kuwatisha wananchi wasiandamane.

Kwa uzoefu wa nchi hii vurugu za maandamano huanzia pale vyombo vya ulinzi na usalama vinapotumia nguvu kubwa kuyazuia badala ya kuyalinda na kuhakikisha yamemalizika salama kwa mujibu wa sheria kwani haki ya kuandamana ipo kwa mujibu wa katiba ya nchi. Kwa mfano maandamano yaliyofanyika wakati wa uchaguzi wa marudio jimbo la kinondoni na kumuua binti akwilina ni jeshi la polisi lililofyatua risasi na kupelekea yale mauaji. Wakati waandamanaji walikuwa hawana hata fimbo mikononi.

Ushauri kwa CCM iache siasa za kizamani za kuwatisha wananchi na kueneza hofu na uogo kwa waandamanaji kuwa maandamano yatamwaga damu. Atakayesababisha damu imwagike ni yule atakayeyazuia haya maandamano kwani ni ya amani.

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
Nchii ukipinga ufisadi mafisadi watakuonesha cha Mtema Kuni.
 
Tuanze kuangalia dola inashughulikaje na wanaoanikwa na ripoti ya CAG ndo ujue kwa nini ukilaani ufisadi Tanzania dola inakuua
 
HIVI IKITOKEA WANANCHI WAKATAKA KUANDAMA,SABABU KUTOKANA NA GHARAMA ZA MAISHA..MFANO NAULI NK
MTAWAZUIA

ova
 
Back
Top Bottom