Lidafo
JF-Expert Member
- Sep 26, 2019
- 813
- 1,566
Habari wanajamvi!
Kwa kipindi kirefu nimekuwa nikifuatilia siasa za Tanzania na kuna mengi ya kuzungumza japo muda ni mchache ila kwa hili la maandamano ya chadema yanayotarajiwa kufanyika tar 24 mwezi huu wa kwanza nikaona si vibaya na mimi nikatoa mtazamo wangu hasa baada ya nguvu kubwa ambayo serikali inatumia kukwamisha maandamano hayo.
Nianze kwa kusema kuwa CCM kama chama tawala kimepitia siasa za panda shuka tangu kuanzishwa kwake na wanauzoefu wa kutosha juu ya siasa za Tanzania na wanajua ya kuwa hali ya nchi kwa sasa si yamatumaini na raia wengi hawana matumaini na serikali hii ya CCM.
Tokea CHADEMA itangaze kutakuwa na maandamano tuliona reaction ya serikali, Kwanza kabisa Mh. Chalamila mkuu wa mkoa husika ambao maandamano yamepangwa kufanyika yaani Dar es salaam alitangaza kutakuwa na usafi ambao utafanywa na Jeshi La Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na jeshi la polisi lakini pia Mh. Paul Makonda Katibu mwenezi wa CCM huyu nae akasema anataka mdahalo na CHADEMA kwani haoni sabaabu ya Chadema kuandamana hasa kupinga miswaada ya sheria za uchaguzi, Tatu baadhi ya kundli la wanasiasa wa vyama vingine tofauti na CHADEMA wakasema hawaungi mkono maandamano hayo, Nne Baadhi ya wafanyabiashara wa kariakoo wakasema hawataandamana, Tano baadhi ya viongozi wa dini.
Swali la msingi ni Kwanini nguvu kubwa inatumika kuyazuia maandamano hayo? Hali yakuwa ni haki ya kikatiba na ni maandamano ya Amani?
Kwanza ni lazima tujue siasa ni Sayansi yenye sanaa ndani yake na kutokana na hili zifuatazo ndio sababu serikali haitaki CHADEMA waandamane.
1. HOFU JUU YA HASIRA WALIZONAZO WANACHI DHIDI YA SERIKALI.
Tutambue kuwa CHADEMA wanataka kuandamana kupinga miswaada ya sheria za uchaguzi lakini hiki ni kipindi ambacho kundi kubwa la wanachi lina hasira na serikali kwakuwa Umeme unasumbua, Huduma mbaya za maji, Elimu lakini Ufisadi umetamalaki kwa kiwango kikubwa na uwajibikaji na uwajibishwaji umeshuka kwa kiwango kilekile ambacho Ufisadi umepanda.
Hili halihitaji jicho la msomi wa PHD kugundua kila mwenye macho anajionea jinsi mambo yalivyo tafrani, Katika kipindi kama hichi serikali haiwezi kuruhusu maandano kwani huenda yakaanza kama maandamano ya kupinga mswaada wa sheria za uchaguzi mwisho yakamalizika kama maandamano ya kupinga mfumuko wa bei, Umeme ,Ufisadi , Rushwa n.k mambo ambayo yanamgusa kila Mtanzania na kwa kiasi kikubwa litawafungua macho watu wengi kitu ambacho CCM hawataki kukisikia kabisa kwani ujinga wa watanzania wengi ni mtaji wao wa Kisiasa.
2. KUIZUIA CHADEMA KURUDISHA NGUVU WALIYOIPOTEZA KWA JAMII.
CCM hawataki CHADEMA wawe karibu na raia kwa namna yeyote kwani wanajua hapo ndipo nguvu ya CHADEMA ilipo. Hivyo kuruhusu maandamano ni kuwafanya CHADEMA kuwa karibu na wanachi jambo ambalo CCM wameshajifunza katika uchaguzi wa 2010 na 2015 kuwa Wananchi wananguvu kubwa hivyo hawawezi kuruhusu nguvu ile CHADEMA waliokuwa nayo wawe nayo tena.
Kwa sababu hizo ndio maana Serikali ya CCM imeamua kuanza hatua za kiushawishi za kuzuia maandamano hayo na njia watakazotumia ni mbili tu.
Moja, ni kuyazuia kabisa kwa kutumia vyombo vya dola jambo ambalo pia linaweza leta taswira mbaya kimataifa kuwa hakuna demokrasia au Mbili kuyaruhusu ila kwa kuyapunguza nguvu maandamano hayo yaani hapa wanatumia mlango wa nyuma alafu wanatokea palepale kwa aliyetumia mlango wa mbele na hii ndio njia ambayo wameamua kuanza nayo kitendo cha kumtumia chalamila na viongozi wa Kisiasa na wafanyabiashara na jeshi kufanya usafi hii yote ni kudhoofisha nguvu ya maandamano hayo na usishangae siku hiyo ya maandano kama yatakuwepo kukajitokeza watu na mabango ya mama anaupiga mwingi, Hili usishangae likitokea ndio siasa za Tanzania lakini pia vyombo vya habari havitaruhusiwa kurusha habari za maandano hapa zitabaki online TV chache ambazo chadema zina mkono wake na labda JF hapa ambapo wamekuwa wakitoa habari pasi upendeleo.
Endapo hili la njia ya pili litatokea maana yake ni kuwa Serikali itakuwa imewapa CHADEMA maji ya vuguvugu ambayo hayakati kiu yaani wamewaruhusu waandamane lakini maandamano yasiyo na matokeo yaliyo kusudiwa.
Katika kuyaepuka yote haya ili CHADEMA Waweze kufanya maandano yenye matokeo waliyoyakusudia ni lazima wachukue hatua mbadala na wao watumie mlango wa mbele na watokee palepale sawa na aliyetumia mlango wa nyuma.
Swali la msingi ambalo Mh.Freeman Mbowe na CHADEMA kwa ujumla wanatakiwa kujiuliza ni nini Kifanyike ili Maandamano waliyokusudia yatimie kwa matokeo makubwa?.. Nitarudi baadae Kwasasa ngoja kwanza nitoke nikatafute mlo wa Mtanzania aneishi chini ya dola moja.
Kabla sija-log off niseme tu kwa yanayoendelea kwa sasa Nchini katika mawanda ya Kisiasa tunapata picha ya kuwa Mama anataka kugombea 2025 na yupo serious na hilo , CCM imepoteza nguvu yake kama chama na tumaini pekee lipo kwa vyombo vya dola na mwisho ni kuwa CHADEMA imepoteza ushawishi wake kwa jamii.
Asanteni.