Kifulambute
JF-Expert Member
- May 8, 2011
- 2,539
- 755
Mimi ni kijana 33 yrs now..katika kuishi kwangu nilibahatika kuoa na sijawahi pata mtoto...miaka minne ya ndoa yetu kuna kipindi.wife alipata ujauzito na ilipofikia siku ya kujifungua mtoto akafariki akiwa tumboni..tukakaa kama miezi saba akapata ujauzito.mwingine ambao ulisumbua sana, miezi minne tu ya ile mimba akaambiwa alazwe bed rest hadi atakapojifungua...tukakubaliana na hali akalazwa hosp for 4 month na ilipofikia miezi nane siku moja ikaonekana mtoto kama anataka kutoka wakamwahisha thearter bahati mbaya ile anafika tu chumba hicho mtoto akafariki...nilipata na simanzi sana nikamshauri wife tukae mwaka na nusu bila kushika ujauzito na sasa tuna mwaka na miezi saba..sasa wife amepatwa na issue ingine tena ya kubleed mfululizo for three month now, tumejaribu kila aina za dawa za hosp, kanisani na mwishowe kuna bibi fulani alitipa dawa ikapungua na sasa namshukuru mungu imekata. Sasa nawaza hivi kuna haja ya kutafuta mtoto kweli ama nipotezee tu niandike walizo kufa wanatosha?