Hivi Kuna Haja Gani JK Kwenda Kuhudhuria Mkutano wa ILO wakati kuna Waziri wa Kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Kuna Haja Gani JK Kwenda Kuhudhuria Mkutano wa ILO wakati kuna Waziri wa Kazi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Prophet, Jun 15, 2011.

 1. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mtoto wa bagamoyo kasepa zake Uswizi. kwa raha zake!
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  aende akae hata mwezi mzima kwani akibaki bongo analeta kauli za ajabu ajabu 'MAASKOFU WAUZA MISUBA'

  mimi najisikia ahueni JK akiwa nje manake hata akibaki hamna akifanyacho
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  yaani hata akiwa hayupo hakuna tofauti maana nchi haina rais....yaani huyu hata mkutano wa mameya wa miji mikuu duniani atataka naye aende
   
 4. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hahahahhah....hahahaha...hah.haha......ha..kekeke..kwikwikwiwi...
  Umenitengenezea siku yangu vizuri sana.ni maajabu sana mimi kucheka asubuhi yoe hii.
  Hata mimi nadhani ni bora aende huko huko ulaya akakae huko asubiri mikutano kuliko kurudi mara kwa mara huku.
  akikaa huko atapunguza garama ya mafuta ya ndege.
   
 5. k

  kazuramimba Senior Member

  #5
  Jun 15, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mwacheni Rais wetu ashinde angani kama popo.msimwingilie mawaziri wana deal na bajeti.
   
 6. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #6
  Jun 15, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Hio meeting vitu ambavyo vinakua addressed huko kweli kabisa hatikiwi huko
  Nafikiri ingekua busara kam Waziri wa Kazi ange husika... HB ni mtaalam saana wa
  ku delegate, but issue ya safari na sherehe humtoi.... Akirudi atasema alienda na kuomba..
   
 7. w

  wela masonga Member

  #7
  Jun 15, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 33
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Pamoja na kukwepa kutatua matatatizo ya ndani ya nchi na ugumu wa kuongoza nchi miaka minne iliyobaki, msisahau suala la posho za safari jamani. Siyo kila kiongozi anapenda posho zimpite
   
 8. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #8
  Jun 15, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Hivi akiwepo au asipokuwepo kuna tofauti gani maana akiwepo hana analofanya zaidi ya kuhudhuria sherehe na kufungua mikutano. Bora aende tuu tubaki tukijua hatuna rais wala nini. Na makamu wake nae hana jipya
   
 9. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #9
  Jun 15, 2011
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Tangu lini Mswahili ukamchukua serious
   
 10. chobu

  chobu JF-Expert Member

  #10
  Jun 15, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mimi sioni sababu ya kuwa na mawaziri lukuki, kumbe mhe. Rais anaweza kufanya kazi zote mwenyewe!
   
 11. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #11
  Jun 15, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  halafu safari hii hajaenda kwenye lile jimbo lake kule marekani aliko daktari wake au kikombe cha babu kime msaidia..
   
 12. Nyami2010

  Nyami2010 JF-Expert Member

  #12
  Jun 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  ILO iko katika utatu, yaani Employers, Workers and Government. Hiyo office ya ILO hapo Dar na kwingine kote duniani, ni secretariat ya kutekeleza kazi za utatu huo.

  Aidha, Tanzania ni miongoni mwa washirika wakuu wa ILO duniani. Mfano, mwaka 2001 Rais Benjamin Mkapa (mstaafu) alizundua mpango wa ILO duniani wa kutokomeza ajira mbaya za watoto. Vilevile, Tanzania tulikuwa miongoni mwa nchi tatu za kwanza, ikiwemo El-salvador, Nepal na Tanzania kutelekeza mpango huo wa kutokemeza ajira mbaya za watoto (Time Bound Programme on Worst Forms of Child Labour). Lakini, pia ujue Tanzania ni miongoni mwa mataifa machache duniani tunaopilot mirudi kadhaa ya UN, ikiwemo One UN-Delivering as ONe Program, Millenium Village, na sasa UNDAP.

  Please, mambo mengine siyo tu kuponda Rais wetu, labda kama una jingine. Kwenda kwake katika ILO-Governing Body ni sahihi na wakati mwingine anahitajika yeye kama Head of State and Government.
   
 13. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #13
  Jun 15, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Ukiona rais anapigania vi- perdiems vya mameya na mawaziri huyo ni wa kuogopa. Unafikiri ni kitu gani kinampa motisha kama siyo hivyo vi- perdiems kwa sababu kama ni kusafiri nje amesafiri sana akiwa waziri wa mambo ya nchi za nje.
   
 14. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #14
  Jun 15, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  jamani hatuwezi kumwachia huyu jamaa awe anasafiri tu bila mipango,kwani waziri hawezi kumwakilisha huyu mzee??mnajua tunadharauliwa sana kwa hilo?
   
 15. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #15
  Jun 15, 2011
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,988
  Likes Received: 20,391
  Trophy Points: 280
  Umeeleza vizuri mkuu, lakini inakuwa vipi pale kila siku ni yy tu ndo anahudhuria tena wakati mwingine anaoenda kukutana nao si watu wa kada yake kabisa, kikubwa hapa nadhani rais wangu anapenda sana kusafiri
   
 16. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #16
  Jun 15, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Ni mandatory yeye kuhudhuria kwa sababu inabidi rais awe na aibu kwani tangu arudi kutoka SA hana hata siku tatu ameshatoweka. Wewe unayosema ni sawa je hairuhusiwi ku- delegate mkuu au anaona hana cha kufanya hapa TZ bora akanyooshe miguu. Halafu nakuuliza Head of state ni position au ni a specific individual? . Kama head of state ni JK na siyo position inayoshikiliwa na mtu aitwaye JK you must be wrong. na kama ni Position basi it's delegable kwa sababu pale wanamtaka rais awe amemtuma mtu kwa niaba au yeye . Sasa akirudi ukawepo mkutano mwingine itabidi aondoke?

  Mbona in the same meeting Urusi imewakilishwa na waziri mkuu (Vladimir Putin )pamoja na Palestina ina maana hao hawana heads of states.
   
 17. Nyami2010

  Nyami2010 JF-Expert Member

  #17
  Jun 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Katika hili, hamjamtendea haki Rais wetu. Rais Kikwete ni lobyist mzuri sana. Mfano, umeweza kuwashawishi wadanish kutoa msaada wa USD 24m kwa ajili ya mradi wa Youth Entrepreneurship Facility (YEF) kwa nchi za Kenya, Uganda na Tanzania. Ni mradi unaotekelezwa na ILO ukilenga kupunguza tatizo la ajira miongoni mwa vijana.

  Hakika, kwenda kwake Geneva ni sawa maana pengine ILO wanataka kumpongeza kwa jitihada zake personally katika kupata donge hilo nono la wadanish! UN hususani ILO wako beneti na J.K, ata ukiua vipi jamaa yupo juu!
   
 18. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #18
  Jun 15, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Anapata posho
   
 19. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #19
  Jun 15, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Hizo hela angeliweza kuzipata hapahapa Tanzania bila kumpigia mtu magoti......

  Yaani Matonya wa Kimataifa nayo imekuwa ni sifa.... Hela zenyewe $24.mls kwa nchi, ...... khaaaa!!!!!

   
 20. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #20
  Jun 15, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Hivi unaweza kuwa Lobbyist halafu ukawa mtu ambaye huna foresight au shortsightedness? Kama ni Lobysit nzuri ameshindwaje tangu 2005 ku lobby akatokomeza mgao wa umeme unaotutesa sana hapa Arusha na sehemu nyingi za TZ. Umeme umeua kabisa mradi wangu wa kuangua vifaranga na si mimi tu na wengine wamepoteza ajira ktk makarakana mengi tu hapa Ar. Sasa huyu anatakiwa akae kitako atambue matatizo makubwa ya mTZ. Dola Mil 24 kwa nchi 3 ni peanut ndugu yangu kwanza kwa calibre ya rais ni kujidhalilisha kwani anatakiwa kwa calibre yake afanye zaidi. Hiyo anayofanya inaweza kufanywa na mbunge yoyote mkuu.
   
Loading...