MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 10,224
- 22,303
Mgao mkali wa umeme, gharama kubwa za Internet (mabando), uhaba wa sukari na vitu kuchelewa kutoka bandarini.
Ni wakati sahihi Mama kufuatilia wazembe wanaomhujumu na kuwachukulia hatua kali. Asiwachekee. Hizi siasa za waziri Bashe sio za kusikiliza. Apigwe tu chini maana kashindwa kazi. Bandarini nako kuna shida. Mizigo inakaa muda mrefu haitoki.
Imefikia wakati hata Simba wa bahari Silent Ocean ukiwapigia simu wanakujibu tuombe tu Mungu mizigo itoke mapema kwa sababu hata wao hawajui itatoka lini. Kuhusu umeme sina haja hata ya kuandika ni madhara kiasi gani yanatokea.
Watendaji wanatupa ahadi hewa zinazokera sana. Kama Mama kashaidhinisha malipo ya matrilioni inashindikana nini suala la umeme kuisha?
Nimeandika kama mtu ninayependa sana uongozi wa Mama Samia na nisingependa kuona 2025 anashinda kwa shida. Ushindi wake unatakiwa uwe wa mapema tu. Haya mambo kutokea 2024 haijakaa vizuri kimkakati.