Uchaguzi 2020 Hivi Kamati Kuu ya CCM hamuwezi kututeulia wagombea wapya kabisa wa Ubunge? Ziara za Rais Magufuli zilithibitisha Wabunge wengi ni mizigo

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,975
Kwa bahati nzuri niliweza kufuatilia ziara zote za Rais Magufuli katika awamu yake ya kwanza ya uongozi.

Kila aliposimama kusalimia wapiga kura wake alielezwa matatizo lukuki na wananchi wa maeneo hayo kana kwamba hawana mbunge na hii ni ishara kuwa Wabunge wengi wa awamu hii ni mizigo.

Haiwezekani matatizo yamsubiri Rais Magufuli aje kuyatatua wakati wabunge wapo na wengine ni mawaziri kabisa.

Hebu fikiria mambo yaliyoibuka Kibiti, Rufiji, Mkuranga na Kilosa unaweza kuamini hawana wabunge kabisa.

Ni wakati sasa chama kikateua wagombea wenye wito wa utumishi na siyo hawa wafanyabiashara waliojazana bungeni kwa maslahi binafsi na kusaka fursa.

Nawatakia Ijumaa kareem.

Maendeleo hayana vyama!
 
johnthebaptist,

Bwashee unausingizi au una tatizo gani leo? Ni kweli kwenye majimbo yanayoongozwa na wabunge wa CCM kuna matatizo, au unajua kuliko Rais mwenye?

Rais anasema kwa kinywa chake kuwa majimbo yaliowachagua wabunge wa vyama pinzani ndiyo ya hovyo kimaendeleo kwasababu hawakumchagulia watu wanaomsikiliza anachowaelekeza. Sasa wewe ni wapi majimbo ya CCM yenye maendeleo duni?

Mfano mzuri kule Morogoro bahati nzuri mbuge alikua wa CCM, haya juzi juzi tena kwa "Bwege" na kuwaambia wakae na "Bwege" wao.
 
johnthebaptist,

..wabunge wa CCM walijielekeza mno kwenye kumsifia Magufuli wakasahau kuwatetea wananchi.

..ndani ya bunge kazi ya wabunge wa CCM ilikuwa kuwashambulia na kuzima hoja za wabunge wa upinzani.

..wabunge wa CCM walikuwa hawazungumzii kabisa matatizo ya wapiga kura wao.
 
Johnthebaptist nao sasa umekubali kuwa makada wa CCM katika ngazi za utumishi wa umma RC, DC, RAS , DED, DAS wameshindwa kuwatumikia wananchi.

Mfano mzuri mkoani Dar es Salaam wajumbe hawakujali kama RC ni kada mwenzao waliona mapungufu makubwa na kuamua kumtumia ujumbe Mwenyekiti wao wa Taifa kwa kumtosa mwanaye mpendwa.
 
..wabunge wa ccm walijielekeza mno kwenye kumsifia Magufuli wakasahau kuwatetea wananchi.

..ndani ya bunge kazi ya wabunge wa ccm ilikuwa kuwashambulia na kuzima hoja za wabunge wa upinzani.

..wabunge wa ccm walikuwa hawazungumzii kabisa matatizo ya wapiga kura wao.
Bali nyie Chadema ndio mlikuwa mnaongelea matatizo ya Watanzania na kujinufaisha na Billioni 8 za ruzuku na michango juu bila kuwa na uwazi, hizo pesa anakula DJ Mbowe pekee.
 
Johnthebaptist nao sasa umekubali kuwa makada wa CCM katika ngazi za utumishi wa umma RC, DC, RAS , DED, DAS wameshindwa kuwatumikia wananchi.

Mfano mzuri mkoani Dar es Salaam wajumbe hawakujali kama RC ni kada mwenzao waliona mapungufu makubwa na kuamua kumtumia ujumbe Mwenyekiti wao wa Taifa kwa kumtosa mwanaye mpendwa.
Wakati wa JK mbona NSSF mlikuwa hamsemi, au ni kwa sababu mlikuwa wafaidika?
 
Kada johnthebaptist anafahamu nchi hii imetawaliwa na CCM miaka yote hivyo lawama zinakwenda kwa CCM na kiongozi / viongozi waliopo madarakani kipindi hiki.
 
Uzuri moja nyie ni wale wale, huwa hamjibu hoja iliyo machoni kazi kubwa ni kupindua meza na ulaghai. Huko mmebobea hatuwawezi. Sasa hao viongozi wengine si mlikuwa nyie mkifaidi?
 
johnthebaptist,

Hao wabunge mzigo wa CCM unaowasema wewe ndio wanamwela mjini Baba wa familia magogoni. Ubora wao hauko kwenye kuwatumikia wananchi bali kulinda maslahi ya chama na ikulu tu.
 
Johnthebaptist nao sasa umekubali kuwa makada wa CCM katika ngazi za utumishi wa umma RC, DC, RAS , DED, DAS wameshindwa kuwatumikia wananchi.

Mfano mzuri mkoani Dar es Salaam wajumbe hawakujali kama RC ni kada mwenzao waliona mapungufu makubwa na kuamua kumtumia ujumbe Mwenyekiti wao wa Taifa kwa kumtosa mwanaye mpendwa.
Kama wajumbe wa Kigamboni au wa Dar es salaam wangepewa fursa ya kumchagua mgombea urais wa ccm hata Jpm wangempiga chini
 
johnthebaptist,

Bwashee unausingizi au una tatizo gani leo? Ni kweli kwenye majimbo yanayoongozwa na wabunge wa CCM kuna matatizo, au unajua kuliko Rais mwenye?

Rais anasema kwa kinywa chake kuwa majimbo yaliowachagua wabunge wa vyama pinzani ndiyo ya hovyo kimaendeleo kwasababu hawakumchagulia watu wanaomsikiliza anachowaelekeza. Sasa wewe ni wapi majimbo ya CCM yenye maendeleo duni?

Mfano mzuri kule Morogoro bahati nzuri mbuge alikua wa CCM, haya juzi juzi tena kwa "Bwege" na kuwaambia wakae na "Bwege" wao.
Jimboni kongwa kwa spika Ndungai ndipo kwenye umasikini wa kutisha sana
 
Bali nyie Chadema ndio mlikuwa mnaongelea matatizo ya Watanzania na kujinufaisha na Billioni 8 za ruzuku na michango juu bila kuwa na uwazi, hizo pesa anakula DJ Mbowe pekee.
Ruzuku ya CCM ndiyo inapigwa kifisadi hakuna mfano akina polepole waliingia masikini sasa ni matajiri mwambie CAG akague hesabu za ruzuku ya CCM muone kama wote hawajakwenda jela mpaka wasitaafu akina Kinana makamba na wenzao
 
Kama wajumbe wa Kigamboni au wa Dar es salaam wangepewa fursa ya kumchagua mgombea urais wa ccm hata Jpm wangempiga chini
Makonda Bashite katengeneza njama Majungu fitna report za kumhujumu mshindi wa kwanza wakose wote amba jina lake lipite na kurejea kugombea ubunge, Kigamboni kuna vioja vitatokea endapo kamati kuu haitamuogopa mungu ikapokea fitna za wivu toka kwa Bashite
 
johnthebaptist,

..wabunge wa CCM walijielekeza mno kwenye kumsifia Magufuli wakasahau kuwatetea wananchi.

..ndani ya bunge kazi ya wabunge wa CCM ilikuwa kuwashambulia na kuzima hoja za wabunge wa upinzani.

..wabunge wa CCM walikuwa hawazungumzii kabisa matatizo ya wapiga kura wao.
Wabunge wa CCM ni 20% huzingumza Bungeni wengine 80% ni kchukua posho kurudi nyumbani na wakiwa Bungeni ni kugonga meza tu siyo zaidi
 
Bali nyie Chadema ndio mlikuwa mnaongelea matatizo ya Watanzania na kujinufaisha na Billioni 8 za ruzuku na michango juu bila kuwa na uwazi, hizo pesa anakula DJ Mbowe pekee.
Usitukumbushe Trillion 1.5 mkuu, inatuuma sana mtu mmoja kubugia fedha yote hiyo peke yake.
 
johnthebaptist,

..wabunge wa CCM walijielekeza mno kwenye kumsifia Magufuli wakasahau kuwatetea wananchi.

..ndani ya bunge kazi ya wabunge wa CCM ilikuwa kuwashambulia na kuzima hoja za wabunge wa upinzani.

..wabunge wa CCM walikuwa hawazungumzii kabisa matatizo ya wapiga kura wao.
Na walikuwa wanatunzwa kwa kazi hiyo. Ukiongea shida za wananchi unakuwa mpinzani
 
Sasa kama mnalielewa hilo hii kauli ya kwamba CCM itabeba idadi kubwa ya wabunge inatoka wapi? Majimboni zaidi ya 75% wameonyesha kushindwa kabisa kufanya chochote kuchochea maendeleo, hadi jimbo la KONGWA la Ndugai.

Kwa nini wananchi wawarudishe tena wabunge was CCM Bungeni wakati wamefail na hata nyie makada mnaliona hilo?
Wabunge wa CCM walikuwa wanashindana kutoa sifa kwa Magufuli na kumalizia kuunga mkono kauli za serikali 100% na wengine waliunga mkono in advance 200% yaani wanaunga mkono hata ambavyo havijajadiliwa.

Mbunge yupo Tunduru anajitapa kwa wapiga kura wake eti serikali ya CCM imejenga SGR, hivi Myao wa Tunduru SGR au ndege za ATCL kwake ni habari ya kuvutia?

Habari za kuwa wapinzani kama kura zao zitaheshimika WATASHINDA KWA KISHINDO sio za kubeza, CCM imeshindwa kuulinda ushindi wao kwa kutimiza wajibu. Mbunge anategemea kutaja mambo ya Magufuli kwa wananchi wasio na maji, madarasa, madawa nk?
 
Wapya watoke wapi chama chenyewe Kizee hicho.

Na mtawaambiaje walioshinda kura za maoni?!
 
Back
Top Bottom