Hivi inampasa mtoto kumtumia fedha mzazi wake hata kama mzazi hana shida ya pesa?

Idrissou02

JF-Expert Member
Jul 31, 2018
354
646
Nipo na ajira nashkuru mungu inayofanya nisogeze maisha. Nina mshahara mdogo tu lkn kwa ubachela wangu unanitosha.

Mdingi wangu (mzazi pekee nliyebaki nae kwa sasa) ana kipato cha uhakika na hana shida ya pesa ndogondogo. Kipato chake ni mara 5 zaidi ya changu kwa mwezi.

Nimekuwa nikiumiza sana kichwa kwamba inanipasa kumtumia mzee percent ya kipato changu kwasababu tu ni mzazi ama nikaushe niweke akiba inisukume kwenye harakati zangu
 
Usimtumie hela in cash..

Ni mzee wako unamjua vizuri..mpelekee zawadi ya kitu apendacho! Hata kama ni cha buku!

Fika nyumbani na parcel yako then mpatie. Inaleta faraja sana..pia itakufungulia milango ya baraka zaidi..
 
Wanakuzd mara tano tena uwahudumie? Unatakiwa ukachek afya ya akili.

Cha kuwasaidi wewe hakipo, wape wazo la biashara akupe mtaji nawe utajirike.
Naungana na mdau aliye sema afrika umaskini hautaisha.
 
Kwa mzazi asiye na uhitaji sioni sababu ya kuhangaika naye. Sana sana labda hivyo vizawadi kama walivyochangia wadau wengine.
 
Watoto, Mke wako na wewe kama wote wako sawa Wazazi labda ndiyo wafwatie, lkn wazazi wasiwe kipaumbele chako na wala usiwaendekeze watakupoteza, wao walishakuwa na maisha yao na wewe kuwa na yako, angalia Mke na watoto kama mmejaliwa kwanza!
Mimi ni mzazi.
Nafahamu raha ya uhusiano na mawasiliano bora kati ya mzazi na mwanae.

Mwelewe/msome zaidi mzazi wako.
Wazazi tunatofautiana.
Kuna wanaopenda kupewa pesa, kuna wanaopenda zawadi, kuna wanaopenda pesa na vitu.
Kuna tunaopenda MAWASILIANO THABITI NA MAENDELEO ya wanetu.
Namaanisha tunatamani kuthaminiwa.

Naunga mkono kujijenga na kujenga familia yako kwanza kwa kuzingatia uwezo wa mzazi.
 
Mimi kwa upande wangu wote ni vipaumbele vyangu
 
Mimi ni mzazi.
Nafahamu raha ya uhusiano na mawasiliano bora kati ya mzazi na mwanae.

Mwelewe/msome zaidi mzazi wako.
Wazazi tunatofautiana.
Kuna wanaopenda kupewa pesa, kuna wanaopenda zawadi, kuna wanaopenda pesa na vitu.
Kuna tunaopenda MAWASILIANO THABITI NA MAENDELEO ya wanetu.
Namaanisha tunatamani kuthaminiwa.

Naunga mkono kujijenga na kujenga familia yako kwanza kwa kuzingatia uwezo wa mzazi.

Labda kama siyo mtoto wako, yaani mtoto wako mwenyewe na damu yako unaweza kumuweka namba 2 baada ya binadamu mwingine yoyote yule? Mimi kwangu mtoto wangu damu yangu ni zaidi yangu na hakuna zaidi yake, kila mtu na kila kitu kinakuja second lkn mtoto wangu ni namba 1 na hilo halijadiliki!
 
JF ya zamani itarudi lini ndugu Mero? Jukwaa hili lilikuwa muhimu na mada nyingi zilikuwa za kujenga na si kupotosha kama hii!
 
Mbona mada ni nzuri na watu wamechangia vizuri kabisa?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom