Hivi huyu Mangi anapiga hesabu za wapi hizi?

Hivi huyu Mangi anapiga hesabu za wapi hizi?

Mii nimependa kuskia duka la BODY SPRAY, linauza PANGABOI na ndio duka hilo hilo kunauzwa MALAPA.

Yaani hii nadhani ni zaidi ya supermarket.

Halafu kuna sehemu mteja anasema kwa sauti ya chini "tayari nshammaliza"

Hapo alikuwa anataka kufanya nini MANGI?
 
Lengo ni kwamba matangazo yenu mjitaidi kuyafanya kila mmoja ayaelewe maana watoto wetu wanajifunza kujumlisha sasa mnawapa tabu sana,kama kuna discount mseme maana mtoto wa chekechea ii umwambie hiyo hesabu ina punguzo unaweza kufanya achukie hesabu kabisa

Aliyekwambia tangazo la kuwafundishia watoto kuhesabu nani?:becky:
 
Jana mwanangu aliniuliza baba unalijua lile tangazo la airtel,nikamuuliza mwanagu ni lipi hilo,akasema lile linaanza na kijana anasema hili duka limejaa nitapata kila kitu,mangi anaitikia karibu kijana.

Kijana anauliza body spray,mangi anasema 15,000,feni mangi anajibu panga boy 50,000,kijana anasema Panga duu,na kisha anauliza na malapa je,mangi anasema 1000,kisha kijana anaomba jumla ngapi mangi anasema 65,500/=

Hapo ndipo mtoto wangu anashangaa badala ya jumla kuwa 66,000/=

Nisaidieni wana jamvi mtoto amuelewe Mangi na hesabu zake.

Hili tangazo limekaa kiakili zaidi. Walifanya hivyo makusudi ili kuzua mijadala kama hii. Wanaamin kabisa watajitangaza zaidi na hii mijadala itafanya watu walitafute ili kusikiliza hiyo kasoro. Wakati anasikiliza kasoro atapata ujumbe wa tangazo lao. Wenyewe wanakuambia Marketing Strategy.

Safi sana marketing manager
 
Back
Top Bottom