Hivi huyu Mangi anapiga hesabu za wapi hizi?

Hivi huyu Mangi anapiga hesabu za wapi hizi?

Dude lao

Member
Joined
Dec 2, 2014
Posts
51
Reaction score
19
Jana mwanangu aliniuliza baba unalijua lile tangazo la airtel,nikamuuliza mwanagu ni lipi hilo,akasema lile linaanza na kijana anasema hili duka limejaa nitapata kila kitu,mangi anaitikia karibu kijana.

Kijana anauliza body spray,mangi anasema 15,000,feni mangi anajibu panga boy 50,000,kijana anasema Panga duu,na kisha anauliza na malapa je,mangi anasema 1000,kisha kijana anaomba jumla ngapi mangi anasema 65,500/=

Hapo ndipo mtoto wangu anashangaa badala ya jumla kuwa 66,000/=

Nisaidieni wana jamvi mtoto amuelewe Mangi na hesabu zake.
 
Mangi hakusema hilo yeye alisema jumla 65,500/=kisha akamwambia kwani wewe umejipangaje,kijana akasema ana buku tu,kisha mangi akamwambia ndorobooo we hiyo buku si ukanunue gazeti ujipepee
 
Mangi hakusema hilo yeye alisema jumla 65,500/=kisha akamwambia kwani wewe umejipangaje,kijana akasema ana buku tu,kisha mangi akamwambia ndorobooo we hiyo buku si ukanunue gazeti ujipepee

Sasa tukusaidieje? Kama unaambiwa discount unabisha. Basi mwambie mwanao Mangi kakosea hesabu. Nadhani ndo lengo lako la kuanzisha hii thread

Thread closed.
 
Mangi hakusema hilo yeye alisema jumla 65,500/=kisha akamwambia kwani wewe umejipangaje,kijana akasema ana buku tu,kisha mangi akamwambia ndorobooo we hiyo buku si ukanunue gazeti ujipepee

huu ni muendelezo wa zile kelele za wanaume wa kirombo apa

ivi wewe 50 elf + 15 elf +buku = na sh ngapi?
ukipata jibu utajua kwann alisema 65000/=
 
Lengo ni kwamba matangazo yenu mjitaidi kuyafanya kila mmoja ayaelewe maana watoto wetu wanajifunza kujumlisha sasa mnawapa tabu sana,kama kuna discount mseme maana mtoto wa chekechea ii umwambie hiyo hesabu ina punguzo unaweza kufanya achukie hesabu kabisa
 
Tangazo zuri sana mangi katoa discount juu kwa juu jamaa hataki ni ndogo
 
Mangi hakupiga hesabu, alisema ''si unaona ndo naandika hapa''?

So hapo hatujui kama alikuwa anaandika bidhaa inayotajwa au alikuwa anaorodhesha mpaka price yake!

Halafu mwishoni alitoa jibu la kuhisi hisi tu pale alipoulizwa jumla shs ngapi.

Alisema ''ni kama'' elfu 65 na mia 5!

Kumbuka katika hesabu za makadirio, 65 na mia 5 inakwenda kimahesabu na 66 elfu..

Btw, lile ni tangazo tu!
 
Mkuu tangazo linatakiwa liweze kuteka usikivu kwa kiwango cha juu sana,mwandaaji wa hili tangazo amafikia lengo kwa kiwango cha juu kabisa!hadi mtt anauliza swali hilo kama ni kweli ujue amesikiliza sii mara moja,na wewe na ss ambao hadi huku bado tunalo!huyu jamaa nampongeza sana kwa kufikiri.
 
Lengo ni kwamba matangazo yenu mjitaidi kuyafanya kila mmoja ayaelewe maana watoto wetu wanajifunza kujumlisha sasa mnawapa tabu sana,kama kuna discount mseme maana mtoto wa chekechea ii umwambie hiyo hesabu ina punguzo unaweza kufanya achukie hesabu kabisa

Target audience ya hilo tangazo sio watoto, hata wasipolielewa hamna athari.
 
Back
Top Bottom