Hivi huyu Mangi anapiga hesabu za wapi hizi?

Hivi huyu Mangi anapiga hesabu za wapi hizi?

Jana mwanangu aliniuliza baba unalijua lile tangazo la airtel,nikamuuliza mwanagu ni lipi hilo,akasema lile linaanza na kijana anasema hili duka limejaa nitapata kila kitu,mangi anaitikia karibu kijana.

Kijana anauliza body spray,mangi anasema 15,000,feni mangi anajibu panga boy 50,000,kijana anasema Panga duu,na kisha anauliza na malapa je,mangi anasema 1000,kisha kijana anaomba jumla ngapi mangi anasema 65,500/=

Hapo ndipo mtoto wangu anashangaa badala ya jumla kuwa 66,000/=

Nisaidieni wana jamvi mtoto amuelewe Mangi na hesabu zake.

Mkuu sikiliza vizuri mangi anasema kama sitini na tano amekadiria kabla ya kufanya uhakiki wa hesabu kwa usahihi alikuwa anafunga bado mzigo wa mteja.
 
Mangi alimpunguzia bei mteja wake, ungekuwa unafanya biashara ungejua
 
Hahahahaha.... manake kama baba anashindwa kumwelimisha mwanae jambo dogo kama hili mpaka aje aombe msaada huku... hatuna jinsi tunalazimika kuwa wapole....
Hakika hekima imetumika.
 
Mangi huyo ametoka rombo jamani, ana lile tatizo la ROMBO DEFICIENCY SYNDROME
 
Hii ni dharau kwa magazeti. Faida zake kuu ni kujipepea kuliko kuelimisha au kutoa habari. kazi kwenu

Mkuu gazeti kama uhuru utanunua ufanyie nini zaidi ya kujipepea na kufungia vitumbua???
 
Biashara ni zaidi ya kujumlisha kutoa na kugawanya. Huyo mwenye buku alikua anafanya biashara pia......
 
Back
Top Bottom