Hivi hii ni kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi hii ni kweli?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtanzania, Dec 4, 2007.

 1. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #1
  Dec 4, 2007
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hapa sasa tusitegemee mabadiliko makubwa kwenye utendaji serikalini.

   
 2. K

  Koba JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2007
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  Hii siielewi maana siamini ninachokisoma,anyway ngoja niisome vizuri maana naona giza hapo,lakini sitashangaa kama kuna ukweli na ndio walichoamua ila itakuwa ni tragedy nyingine,sijui labda wana maelezo ya kutosha kuhalalisha hii kitu
   
 3. O

  Ogah JF-Expert Member

  #3
  Dec 4, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mtanzania,

  Yeah, ni kweli kama ulivyioaarifiwa........................inasikitisha sana kuona bado watu wanaendeleza UVIVU wa kufikiri..................anyway ndio serikali yetu tena.....

  ndg Morani pia aliazisha hiyo mada kama inavyoonekana hapa
  http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=7697
   
 4. green29

  green29 JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2007
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 312
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 35
  Kwani kuna gharama gani ambayo wanaiepuka katika kuwapa orientation Senior civil officers wapya. Nafikiri kama ni kweli ndio wameamua hivyo tutegemee gharama kubwa sana ya kufunga milango ya kukwepa ubunifu na mawazo mapya ambayo yamekuwa yanaletwa na Officers wapya wanaoingia serikalini.

  Ushindani katika ajira na vyeo umekuwa ni chanzo cha demokrasia katika ajira na utendaji mzuri makazini. Kuondoa ushindani ni sawa na kujenga mazingira ya kupendeleana na kulindana; ndio mwanzo wa subordinates kuwa ni kama ma-house boy na ma-house girl kwa wanaowateua.

  Sijui wamepanga utaratibu gani lakini hata wakiamua kutumia utaratibu huo wa kuteua wafanyakazi walio kwenye sekta ya uma ni muhimu kukawa na uwazi na namna flani ya ushindani miongoni mwa watumishi hao wa uma.
   
 5. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #5
  Dec 4, 2007
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Tanzania tuna kazi kubwa kweli kweli, hivi sisi tunataka kuendelea au tunafurahi kuona watu wetu wanakuwa maskini? Nashindwa kuona mantiki ya hii sheria.
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Dec 4, 2007
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,535
  Likes Received: 81,956
  Trophy Points: 280
  Hata mimi hili limenishangaza sana. Wanapiga debe kuweka mazingira mazuri ya Watanzania walio nje warudi nyumbani, halafu wanasema hawataajiri wafanyakazi toka nje ya serikali! Bado wanataka kuwa na watendaji wenye elimu na vision finyu na matokeo yake ni utendaji mbovu kila kukicha! Mtu anarudi Bongo na nondo kali, utaalamu aliokuwa nao unahitajika sana Tanzania lakini kwa urasimu wetu tunamwambia well we need people with your expertise, but we have a policy not to hire senior officials outside the government, bye bye. Akienda Namibia au Botswana tunaanza kulalama na kuwaita~Watanzania waliokimbilia nje! Mwe!
   
 7. K

  Koba JF-Expert Member

  #7
  Dec 4, 2007
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  does this mean kama wewe haumo ndani ya system/serikali huwezi kuajiriwa in a senior position hata kama elimu yako inatakiwa uanzie huko juu...watu hawa naona vichwani ni makamasi tuu labda kada anaelewa kwanini?
   
 8. green29

  green29 JF-Expert Member

  #8
  Dec 4, 2007
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 312
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 35
  Ni kweli kabisa Bubu, hawa wanataka kubariki A CLOSED SYSTEM ambayo itaanza kufanya utendaji katika sector ya uma ukose uhai. Sijui wanapigaje mahesabu wanaposema wanataka kupunguza gharama. Kupunguza gharama katika mantiki ipi sababu unaweza kupunguza gharama in a short run lakini ukalia in a long run. Huu utaalamu kotoka nje ya sekta ya uma unaoanza kupigwa vita ndio ungepunguza gharama kwa kuwapa wafanyakazi waliokuwemo kwenye sekta ya uma nafasi ya kujifunza vitu vipya na kuboresha utendaji wao.
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Dec 4, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Hatimaye taifa letu limeamua kujijenga mfumo rasmi wa political patronage. Hawa jamaa sasa nadhani wameshindwa hata kufikiri, niliposoma mara ya kwanza jana nilidhani moja wapo ya zile email za utani, but then naona hili ni kweli. Kama hujaingia serikalini bora uingie sasa.
   
 10. t

  tz_devil JF-Expert Member

  #10
  Dec 4, 2007
  Joined: Jun 21, 2007
  Messages: 272
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Kama ni kupunguza gharama mbona kuna maeneo mengi ya kuanzia kama kutonunua magari ya mil 100/-, na safari zisizokuwa na msingi.

  Suala la kuto recruit watu wengine inamaana hakutokuwa na diversity serikalini, kisha tutaendeleza ujinga ule ule. Hizi si habari nzuri ki ufanisi.
   
 11. YournameisMINE

  YournameisMINE JF-Expert Member

  #11
  Dec 4, 2007
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 2,451
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 145
  Wasee,
  Sasa huyo waziri anaitwa "Ghasia," sijui nyie mlikuwa mnategemea nini!!?(joke). Mwendo mdundo, legacy ya Nyerere hiyo!.
   
 12. O

  Ogah JF-Expert Member

  #12
  Dec 4, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  brazamen alishatuambia kuwa watu wachukue mikoba..............watu fanyeni kweli hakikisheni mmepata hiyo mikoba ya huko mliko................mkirudi nyumbani mnarudi kama experts.............mnafungua kampuni zenu.............consultants!!
   
 13. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #13
  Dec 4, 2007
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Kwa Mtindo huu,inaonekana wazi kuwa Waziri Huyu anayehusika na Utumishi ni Kilaza.Hauwezi kujiwekea mipaka ya kuajiri wenye uwezo kwa sababu tu ya kutaka kuwabeba au kuwanufaisha waliomo kwenye ajira hiyo.Kunakuwa hakuna maana ya "Competitive selection",kwa mtindo huu kutaziacha Idara za serikali na Wizara zake kuwa na mawazo duni na ya kizamani,kwa sababu ya kufungwa nafasi ya kuingia mawazo mapya na ya kisasa zaidi.

  Kwa Mtazamo wangu napendekeza kwamba Sera ya Ajira ijali zaidi Elimu,Uwezo na Uzoefu wa Mwombaji,Na nafasi ziwe wazi kwa Mtanzania yeyote bila kujali Ukoo,Rangi au mipaka ya Nchi ili mradi tu awe na sifa zaidi kuliko wengine katika Mchakato huo.

  Kukubali Mawazo na Ushauri wa akina Hawa Ghasia ni kudumaza Maendeleo ya Nchi yetu!!,Kwani yule anayefanya kazi Tanzania Breweries au Sigara si Mwenzetu?Kwa maelezo yao haya wanatutaka wote tufanye kazi serikalini?Nani ataendesha mashirika binafsi?Mkazo uwe kwenye Elimu na Uwezo na SI VINGINEVYO.
   
 14. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #14
  Dec 4, 2007
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Jamani lazima tuelewe psyche ya watumishi wa umma wa sasa.
  Kwanza kabisa wengi wao wana inferiority complex, wanajua kwamba elimu, uwezo na ujuzi wao ni duni, na wale wachache (respect!) wako wachache na mara nyingi very lonely!
  Sasa wanataka kulinda nafasi hizo maana hawataki mtu aruke foleni (tihihi!) hivyo wanapunguza wasomi wanaovamiavamia foleni ya kupandishwa cheo!
  Sasa kutokana na kuwa serikali hii ya JK ni the most populist ever! Basi wameamua kuwaridhisha watumishi wa umma, maana unafikiri kungekuwa na job application na job interview mawaziri wangapi wangepata nafasi zao hizo?
  Mi nakubaliana kabisa na brazamen, just open your consultancy alafu watakapohitaji your brains, make sure they pay through their noses, and then we will see who has the last laugh!
   
 15. T

  Tom JF-Expert Member

  #15
  Dec 4, 2007
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Utaratibu mzuri zaidi ya huo mpya unatakiwa ili kupata ushindani endelevu.
  Nchi zingine km China kuajiriwa serikalini hua kuna ushindani mkubwa sana kwa kua kazi hua ni za kudumu (kwa wawajibikaji)na pia zina marupurupu mazuri. Hivyo ili kutoa nafasi sawa, watu waliofuzu chuoni ambao wanaotegemea kuomba kazi ama kuajiriwa serikalini hutakiwa kufanya mitihani maalumu iliyoandaliwa na kusimamiwa na idara za serikali. Kama utafaulu huo mtihani basi utakua na nafasi ya kushiriki ktk ushindani wa kuajiriwa ktk kazi zitokeazo serikalini na ushindi hautafuata kufaulu huo mtihani na elimu yako pekee, bali na uzoefu, general suitability and skills za mwombaji.
   
 16. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #16
  Dec 4, 2007
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Mhh huu ushauri mbona unatamanisha sana...yaani kila kukicha sababu za kukata tamaa kwenda kuishi maisha bora nyumbani zinazidi kuongezeka. Sasa kwa mwendo huu wa hawa viongozi wetu ambao tunapenda tuamini kwamba wana vision, kuna haja hata ya kudai huo uraia wa nchi mbili kweli?!!
   
 17. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #17
  Dec 4, 2007
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Sera huanzia kwa waziri na Katibu Mkuu wake. Wakiwa na sere za kipuuzi basi tunaelekezwa huko huko. Hebu fikiria Waziri sijui anaitwa Mungai, aliunda sera ya kuua elimu nchini na ikatekelezwa hadi alipokuja huyu wa sasa Sita na kibadili.

  Naona Ghasia kaja na sera kutoka nyumbani kwake. Nafikiri tumchambue .Kama Kuna mwenye data zake atupe hapa maana inawezekana ni another Kihiyo au alikuwa anatelezea skuli.
   
 18. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #18
  Dec 4, 2007
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Ndio mkuu, lakini vipi watanzania wenzetu kwa maelfu ambao hawawezi kwenda nje na kupata hiyo mikoba?

  Mapambano ya sasa lazima yalenge kumkomboa mpaka MTanzania wa chini. Ikibidi kutakuwa mpaka kurusha ngumi kama bi Karume.

  Kuna haja ya kulivalia njuga hili suala na kumwandama na hili swali JK mahali popote atakapokuwa.

  Kwa kweli sioni mantiki kabisa ya hili. Kuna uozo mkubwa kwenye utendaji wa baadhi ya maofisa wa serikali wizarani, njia ya kuimarisha ni kuwapambanisha na Watanzania wengine wenye uwezo kama wao au hata zaidi yao.
   
 19. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #19
  Dec 4, 2007
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Someni hii japo haina uhusiano wa karibu sana na hii ya Ghasia. Lakini Mwenyekiti huyo hana tofauti na baadhi ya wafanyakazi wa wizara:

  Kikwete acharuka

  2007-12-04 10:28:45
  Na Maura Mwingira, Mkuranga


  Rais Jakaya Kikwete amesema viongozi wanaokimbilia vyeo na madaraka na kushindwa kuvifanyia kazi, wanamchefua. ``Msiombe vyeo kama hamuwezi kuvitumikia, msinichefue, leo ziara imeaanza vibaya,`` alisema akionyesha kukasirika.

  Kauli hiyo ya Rais ilitokana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Bw. Juma Abeid, kushindwa kuelezea Halmashauri yake imepewa kiasi gani cha fedha kwa shughuli za maendeleo katika bajeti ya 2007/08.

  �Haya Mwenyekiti wa halmashauri sema mmepewa kiasi gani katika mwaka huu wa fedha, simama na useme siyo kuvaa koti tu na kukunja mikono hapa,� alisema.

  ``Hizo hizo alizotaja Mkuu wa Wilaya shilingi 239,`` alijibu Mwenyekiti wa Halmashauri.

  ``Nimesema mmepewa shilingi ngapi za shughuli zenu, haiwezekani kuwa ni shilingi 239, sema mmepewa shilingi ngapi za shughuli zenu,`` alihoji tena Rais kwa ukali, na kujibiwa tena na mwenyekiti huyo. ``hizo hizo kama aliyosema Mkuu wa Wilaya.

  Jibu hilo lilimkasirisha rais na kusema ``hivi mmepewa uongozi mkafanye nini, msiombe vyeo kama hamuwezi kuvifanyia kazi.

  Mkurugenzi wa Wilaya alimnusuru Mwenyekiti wake kwa kueleza kuwa mwaka huu halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga ilikuwa imepatiwa Shilingi bilioni tisa kwa shughuli za maendeleo. Shilingi milioni 239 alizozitaja mkuu wa wilaya zilikuwa ni kwa ajili ya ukarabati wa barabara.

  �Sasa kumbe mmpewa shilingi bilioni 9 kwa nini unashindwa kueleza, na kama uongozi wenyewe ndio kama huu, ni wazi utashindwa kuthibitisha fedha hizo zimetumikaje.�

  Rais ambaye yuko katika siku yake ya pili ya ziara ya kukagua shughuli za maendeleo katika mkoa wa Pwani, jana alikuwa Wilayani Mkuranga, ambako alilazimika pia kumkatisha kauli mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya korosho kwa kushindwa kutoa maelezo ya kina ya namna gani Bodi hiyo imejiandaa kuwanusuru wakulima wa korosho ambao bado wanakorosho nyingi majumbani mwao.

  Mwakilishi huyo alipotakiwa na Mkuu wa Wilaya kuelezea mbele ya Rais ni namna gani umejipanga kuwasaidia wakulima wa korosho wilayani humo, alieleza kuwa ndio kwanza bodi iko katika vikao vya maandalizi kwa kile alichosema kuwa utaratibu wa vyama vya ushirika wa kununua korosho msimu huu ni mpya hivyo bodi ndio inajipanga.

  ``Kumbe ndio kwanza mko kwenye maandalizi, nenda kakae chini,`` alisema rais akionyesha kukerwa na maelezo hayo.

  Naye Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula, Bw. Christopher Chiza akijaribu kutoa maelezo kwa Rais kwa nini kumekuwa na kusuasua katika ununuzi wa zao hilo, alisema kuwa kinachojitokeza hivi sasa ni kwa vyama vya ushirika kushindwa kuwafikia wakulima kutokana na ukosefu wa magari ya kuwafikisha kwa wakulima.

  ``Mheshimiwa Rais tatizo si mtaji kwa sababu mabenki yapo tayari kukopesha, tatizo ni kuwa vyama vingi ikiwa ni pamoja na CORECU havina uwezo wa kuwafikia wakulima wala uwezo wa kufikisha fedha kwa wakulima. Juhudi zinafanywa za kuviongezea uwezo ili vyama hivi viweze kufika vijijini,`` alisema.
   
 20. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #20
  Dec 4, 2007
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Another step, kwa hiyo sisi tusio serikalini ndiyo basi. Tukitaka kuingia huko tufanyeje mbona hajafafanua hilo? Katoa mada mbichi haijaiva hii.
   
Loading...