Hivi hii ni kweli?

does this mean kama wewe haumo ndani ya system/serikali huwezi kuajiriwa in a senior position hata kama elimu yako inatakiwa uanzie huko juu...watu hawa naona vichwani ni makamasi tuu labda kada anaelewa kwanini?

Yaani pamoja na kutaabika kwangu kote kujisomea ili niitumikie sirikali naona sasa nachinjiwa baharini. Sijauelewa vyema huu uamuzi wa Hawa Ghasia na wenzake wa utumishi wa umma, sijajua mantiki hasa ya kufanya maamuzi haya ambayo kwa maoni yangu naona ni maamuzi ya ajabu kupita maelezo.

HOJA
1. Napinga suala la serikali kujitetea kwamba wanaepuka gharama za "On job training", hizi haziepukiki kabisa. Teknolojia mpya za utendaji kazi huwa zinabadilika kila leo, kwa hiyo mafunzo kazini hayakwepeki. Madhara ya kutowapa elimu mpya hao watumishi wa zamani ni makubwa sana kuliko hizo gharama wanazojifanya wanaziepuka, na hapo ndipo tunapoangamiza kabisa na zile juhudi kidogo tulizozionyesha katika utumishi wa umma. Wanataka turudi kwenye kuhifadhi mafaili "Manually", badala ya kutumia nyenzo? Mfano, mwishoni mwa miaka ya tisini, wengi tulitumia programu za kompyuta za "Windows 9x, yaani 95 na 98. Kuanzia mwaka 2000 kumekuja Windows mpya zikiwa na mambo mengi mapya. Windows hizi ni Millennium Edition (ME), 2000, XP, Media Cente Edition, Server na sasa vista. Sasa kama uliajiri watu wa kutumia windows 95 miaka hiyo, lazima watu hawa wapate elimu ya kutumia programu hizi mpya, ama uamue kubaki na teknolojia ya zamani na kupunguza ufanisi. Mpaka hapa lazima utafute mtu wa kuwapa elimu mpya hawa watumishi. Huu uhafidhina naona umefikia mahali pabaya sana. Huo ni mfano mmoja tu. Najua kwa watawala, mbinu za kiutawala hubadilika kuendana na mazingira na wakati, kwa hiyo kutokubali kubadilika ina manaa tunarudisha maendeleo nyuma.

2.Kasema kuwa wataajiri watendaji pale tu ambapo kutakuwa hakuna kabisa watumishi wa nafasi husika waliopo kazini kwa wakati huo. Sawa! Je hawa hawatapatiwa mafunzo ya utendaji? Sasa hapa unaepuka nini na unakwepa nini?

3. Kuna hizi tuhuma hapa Jf kwamba watoto wa vigogo wamejazana kule kunako pesa za sie walipa kodi. Ina maana kama hakuna mtu wa kuingia kutoka nje ya hao waliopo basi sisi wenye hizo pesa tunakosa imani na waliopo, hili nalo litafanya hata kile kidogo tulichohifadhi kitokomee kabisa. Nina wasiwasi na hili, labda nipatiwe ufafanuzi. Nina hofu na hizi ajira za vimemo.

4. Hoja nyingine ya Mheshimiwa Ghasia ni kwamba wanakwepa kuajiri watu ambao utendaji wao haujulikani. hili nalo mimi nalipinga kabisa. Sirikali haina uwezo wa kumjua kila mtu na utendaji wake, sawa, lakini kuna watu ambao wako nje ya utumishi wa umma na wanafahamika kuwa ni watendaji kazi bora sana. Mfano, kuna Dr Kimei wa CRDB ambaye utendaji wake unaonekana, kwamba benki anayoiongoza inazalisha faida na wanahisa wanapa gawio, tofauti na TOL. Sasa huyu naye watasema utendaji wake haufahamiki? Kuna wahandisi, mameneja, watawala na watafiti kibao sana wanaotumika nje ya utumushi wa umma na wanafahamika kwa utendaji wao, sasa kwa nini watiliwe shaka? Hali kadhalika kuna kipindi cha maangalizi (probation), mtu anapoanza kazi, kama utenaji wake hauridhishi basi anabadilishwa. Napinga kabisa kitendo cha sirikali kuogopa kuajiri watu eti kwa sababu utendaji wao haufahamiki. Huku ni kutokubali changamoto. Ingekuwa ni mtihani kwa Ghasia na wenzake ningewapa alama "G" kabisa, kwa sababu wamepitiliza kiwango cha mwisho cha kufelia ambacho ni daraja "F".
Huo ndio mtazamo wangu
Naomba kuwasilisha!
 
Mtanzania,

unajua hilijambo linatia hasira/uchungu/kichefuchefu kuona kwamba bado kuna watu wana mawazo ambayo hayawezi kufikirika...............very very un-reasonable and un-thinkable

In short utendaji wa Utumishi wa Umma utaendelea kuzorota kwa idea kama hizi. Siamini pia hili limepitia kwa Lowassa..............kwani kuna kipindi nilimpa credit EL kwa kuvalia njuga utendaji serikalini na nakumbuka alisema kuwa................watu serikalini wapewe mikataba kulingana na performance zao..................kusema kweli statement hii ilinitia moyo..................lakini hivi sasa naona mambo yanakuwa yakienda kinyume........shame to Waziri Ghasia! na waliompa ushauri wa UKILAZA namna hiyo.

Mtanzania sio kwamba siwakumbuki Watanzania walio nyumbani...hapana, nimewakumbuka sana hasa ukiangalia ile link niliyoweka, niliandika..........
hilo jambo linasikitisha sana.....................na hasa ukizingatia hivi sasa vigogo wanafanya kila namna kuwaingiza watoto wao both in Siasa na ktk System pia............ sisemi kuwa vijana wao hawafai no............isipokuwa the move behind ndio inatisha.........na hasa ukiangalia nafasi ya mwananchi wa kawaida

sina hakika kama JK kesha-endorse hiyo kitu....................namshauri asi-endorse huo mpango na badala yake

1. watu waajiriwe serikalini on merits and competetively hii ikijumuisha hata watu walio nje ya system...................kwani kuendelea na mfumo wa Waziri Ghasia ni ku-invite Wataalam kutoka NORWAY

2. ukiondoa zile sehemu nyeti Waajirwa serikalini wapewe contracts zenye malengo na ziwe re-newed based on performance (evaluation which is to be done by an independent consultant)

mawazo mengine mazuri tu yametolewa na Tom pamoja na Mwawado

Kwa hiyo waserikalikama mnasoma hapa chukuenimawazo hayo na muyafanyie kazi
 
Kweli hii ni ghasia tupu!
Serikali inakuwa kama 'Kingdom' walioko nje basi- walie tu! Au wakipenda waanzie ngazi za chini! Je mko hapo?
 
Jamani hii kitu ni very simple.Serikali hizi zimejaza watoto na wajomba zao kwenye nafasi za serikali.Sasa unafikiri lini watashika madaraka makubwa ili kulinda uovu wa baba zao.The government is a family circle in Tanzania.
 
Jamani hii kitu ni very simple.Serikali hizi zimejaza watoto na wajomba zao kwenye nafasi za serikali.Sasa unafikiri lini watashika madaraka makubwa ili kulinda uovu wa baba zao.The government is a family circle in Tanzania.

You got it right Nyangumi,


Hapa ni mwendo wa kujuana na kulindana period!
Kwamba nikuteuliwa?????? give me a break!

Tumeisha ziona teuzi zilifo fanyika na zinazo endelea fanyika, sasa wameona hizo haziwatoshi wana halalisha na hii ili wajazane tuuuuuuuuu! Hii sheria inabidi tuipinge kwa nguvu zote! haifai haifai haifai kabisa!
 
That bit about cost cutting is a sheer insult on Tanzanian's intelligence. This all boils down to insecure old guards making sure Young Turks do not come down with a Masters degree wakawatoa katika positions.
 
Huu ni ujinga ambao sijwahi kuusikia , yaani nikisoma mambo yanayfanyika Tz natamani kulia kwa sauti na kuikana ile nchi milele! At the end of te day, that is the only place we have to call home, masikini waTZ.Sasa hawa mawaziri ambao wameigeuza serikali ni kafamily section wanataka madaraka yawaendee wenyewe kwa wenyewe mpaka mwisho wa dunia, asikanyage mtoto wa kapuku hapo ambaye ataleta mabadiliko. Jk amka usingizini punguza smile hiyo anza kazi, watz hawakukuchagua uje uwakenulie na huku nchi inakwenda mrama, this is nonsense and it has to stop right away! acheni ujinga sasa mmezidi kuindesha Tz kama kichwa cha mwenda wazimu mkifikiri watu hatujasoma!
 
Kwa kweli inasikitisha sana kuona serikali inabagua wananchi wake katika ajira. Eti Ghasia anasema serikali haitaajiri mtu ambaye haimfahamu. Hii ina maana gani? kwa hiyo ina maana watakaofanya kazi ya serikali ni wale ambao tayari wamo na ndugu zao. Kama wewe ni mkurugenzi, katibu mkuu au waziri ni wazi utakaopendekeza waajiriwe ni watoto wako, shemeji zako, wapwa zako, wajomba zako, n.k. Watoto wa wale ambao hawako serikalini hawataonja kazi ya serikali. Sasa hawa wasio na ndugu zao serikalini watafanya kazi wapi?

Hivi huyu Ghasia yeye aliajiriwa kwa sababu serikali ilikuwa inamfahamu au kwa sababu rais alikuwa anamfahamu au kwa vile alikuwa na sifa za kutosha kuruhusu ateuliwe kwenye wadhifa alio nao? kwa kweli inatakiwa Ghasia aombe msamaha kwa watanzania kwa kuwatukana. Hivi serikali chini ya Kikwete imekuwa ni klabu ya watu fulani tu? Hii inaeleza kwa nini yule kijana wa kidato cha kwanza kule Ukerewe alipomuuliza Waziri Mkuu kwa nini mtu mmoja anahodhi nyadhifa nyingi serikalini waziri mkuu alishindwa kujibu na kuanza kumtisha.

Ni wazi kwamba watoto wa sasa hivi wanapata taarifa na habari nyingi kuliko wazazi wao kwa sababu ya maendeleo ya teknolojia na wingi wa vyombo vya habari. Hivyo upeo wao wa kuona na kuhoji mambo yatokeayo katika jamii ni mkubwa. Hivyo pia kwa watu wazima. Mara zote serikali au viongozi walioko madarakani ndiyo huleta mafarakano ndani ya nchi zao kwa sababu ya tamaa za kutaka kutawala milele au jamaa zao.

Nawaonya hao walioko madarakani na ambao wanadhani kwamba vijana walioko vyuoni, sekondari na hata shule za msingi watakubali nchi itekwe na watu wenye uchu wa kuifilisi kwa kurithishana madaraka na jamaa zao. Ni juzi tu Chavez wa Venezuela alidhani anaweza kuwaendesha watu wake anavyotaka lakini akaumbuka. Alidhani anapendwa sana kwamba lolote analotaka wanamnchiwake watakubali. Kwa hiyo na Kikwete na kundi lake wasijewakadhani watanzania wamelala au wnawapenda sana kiasi cha kuwaruhusu watende watakalo hata kama ni la uozo.
 
Hii sasa inapingana na katiba ya nchi ya haki ya kupata kazi , sasa nafikiri kuna haja ya kuwaburuza mahakamani ili wajue kufanya maamuzi sahihi na sio kufanya utumbo kama huu .

Kama hawataki kupata watui kutoka nje ,je hofu yao ni kitu gani.

Kama mtu hajiendelezi atawezaje kupewa cheo kwa vile tuu yupo hapo serikal;ini, jamani hapa tutawafanya watendaji kuwa miungu watu kuwaq hata kama hawajiendelezi basi watapanda cheo kiulaini tuu.

Kwa hili mimi sipo na tena sitakuwepo huu ni upuuzi .
 
Hii sasa inapingana na katiba ya nchi ya haki ya kupata kazi , sasa nafikiri kuna haja ya kuwaburuza mahakamani ili wajue kufanya maamuzi sahihi na sio kufanya utumbo kama huu .

Kama hawataki kupata watui kutoka nje ,je hofu yao ni kitu gani.

....

Hapo ndugu yangu umeongea!
Naomba nipendekeze ya kuwa:
1) Kufanya utafiti kama hii ni kweli na kama imeshakuwa sheria kubwa au ndogo au by law or whatever.
2)Wanaharakati wafungue kesi mahakamani wakiomba ifutwe kwani inapingana na katiba (discrimination, there's no equal opportunity)
3) Kama ni internal memo au sera, basi serikali ishtakiwe kwani hakuna sheria ya kuomba kufutwa. This will be better maana utamshtaki waziri au waziri mkuu au rais, yeyote aliyesaini memo au sera (policy) hii

Sasa naomba kazi itendeke!

Lakini naomba niongezee tu kwamba mimi sivutiwi kabisa na kazi za serikalini. Kama wewe kweli unataka kutenda na kuchapa kazi, ofisi hizi za serikali zinafrustrate! Lakini, hey! That's my opinion, niko tayari kuchangia mawazo ili wengine wapate nafasi because at the end of the day, we need educated, decent civil servants not greedy, selfish ones like the ones we have now who do not serve us but lord over us!
 
huu mkisema ni ushauri wa ghasia mtakuwa mnamuonea bure.
ushauri huu alikuja nao kikwete kwenye safari yake ya kwanza nje ya nchi,

alipohutubia na wananchi wa ughaibuni alisema kuwa serikali inawapa umbele watu waliopo serikalini, na kwamba iwapo kutakuwa na 'ofisa mtendaji mzuri aliyekaa kazini kwa muda mrefu, basi hakutokuwa na haja ya kuchukuwa mtu mwengine kutoka nje ya idara ile japo kama ana elimu kubwa zaidi, kwa vile hana uzowefu na idara ile na aliyekuwepo chini anafaa pia"

sasa kama ameshindwa kuifanya hivyo alivyotaka au alikusudia hivi ilivyokuwa, nashindwa kumuelewa. ....ila kwa hali hii ya sasa hatufiki
 
Hapa sasa tusitegemee mabadiliko makubwa kwenye utendaji serikalini.

Katika hali ya kawaida kabisa mambo mengi kwa sasa ni kwa ushindani na si kwa kutumia vigezo ambavyo mwisho wa siku uleta upendeleo. Mfano pale ambapo tumeonekana kupungukiwa ni mfumo wa ajira BOT. Mara nyingi kazi zao hazitangazwi lakini wanaajili na mwisho wa siku watoto wa vigogo wanaonekana kuwa na taarifa zaidi za nafasi ya kazi kuliko watanzania wengine.
Nachukia sana kutoa nafasi kwa kigezo kama hiki ambacho Hawa amekitangaza. Ukichukulia serikalini, watu wenyekujituma na kuthamini kazi zao ni wachache hivyo kuweka ushindani ni jambo la msingi. Hapo ambapo serikali ya huyu mweshimiwa inatuweka ni pagumu kwetu na hana tofauti na aliyekuwa waziri wa elimu Mungai aliyeleta mabadiliko ya hovyo kwa kuondoa michezo mashuleni, kufuta somo la kilimo, biashara huku mawaziri wenzake akiwemo JK wakibaki kimya. Si ajabu ndivyo walivyo sikio la kufa halisikii dawa.
 
Nilisema siku tatu zilzopita kuwa inabidi nifanye utafiti yakinifu wa suala la kutoajiri watu nje ya serikali kushika nafasi za juu. Majibu yake ni kama yafuatayo.
UAMUZI WA SERIKALI SI SAHIHI.. Tangu Tanzania ipate uhuru serikali ilibakia kuwa muajiri mkuu wa raia wa Tanzania. Hii ilitokana na sera za Azimio la Arusha za kuktaza shughuli za kiuchumi kuwa mikononi mwa watu binafsi. Kwa hiyo kuanzia mashirika ya Umma na idara za serikali zote zilitegemea kuajiri watu, na wote walikuwa chini ya Wizara husika.
Matokeo yake ni kuendelea kudorora kwa utendaji wa serikali hasa kusimamia shughuli zake na za kiuchumi. Ikaongezewa na hali ya mabadiliko ya kiuchumi Duniani. Hakukua na njia nyengine isipokuwa kutema mashirika na kuyauza chee au kuyafuta kabisa. Mbadala ukawa kukaribisha sekta binafsi Nchini. Ili serikali ifanye kazi yake kama serikali.
Sasa basi kwa kuzingatia sera za free market economy amabzo hapa nitaongelea Labour economy. Ni kuwa watu wana uhuru wa kuuza nguvu kazi yao pale wanapopata maslahi ya kuwafaa iwe ni fedha au mafao mengine katika maisha yao. Kwa hiyo makampuni binafsi ytawajiri watu kwa ushindani wa competence na skills zao ili kuleta Tija. Na ndiyo maana yanafanikiwa. HAKUNA KUBEBANA.

Sasa serikali inapoamua kuwa hakuna kuajiri watu wa ngazi za JUU kwa kuepuka gharama za training. That is unproffessional statement. Inaonekana watalaam waliompa waziri kuropka hayo ni watendaji wa serikali ambao sio competent. wanalinda vyeo vyao. Maana wakishajenga ukuta huo ina maana kupanda cheo ni mpaka ujipendekeze. Au kwa maana nyengine utapanda cheo kulingana miaka uliyokaa Kazini badala ya kujali tija yako. Hivyo utaratibu huo unampa fursa bosi aliyeko juu kuendela hapo mpaka astaafu hata kama anafanya madudu Maana Tanzania hatuna utaratibu wa accontability. Saana saana tutarudia palepal ukikorofisha hapa wanakuhamisha kwenda pale!

Hivi serikali yote na hasa idara ya utumishi mbona najua kuna watu pale wana Ma PhD na Ma masters ya Management tena wamesoma aidha ughaibuni aau hapohapo Tanzania, ilikuwaje wakatoa advise kama hiyo? Msimlaumu waziri ni idara ua utumishi, ina Tecnhocrats wake( wakiongozwa na katibu mkuu) waziri ni political symbol.

Hitimisho: ukweli ni kuwa Tanzania sera zake zitaendelea kutomfaa mtanzania wa karne 21. hakuna mabadiliko yakinifu yatakayokuja. Ni dhahiri watendaji wamelewa nafasi walizo nazo, wanazilinda kwa udi na uvumba. Ndiyo maana hata akichaguliwa Rais mzuri kama watendaji wa serikali ambao wamekabidhiwa dhamana kubwa kuwajibika wanafanya madudu kama hayo basi ni dhahiri uozo, rushwa, uzandiki, upendeleo, kijicho, uvivu, umangimeza na kutowajibika vitaendelea kitawala serikali yetu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom