Saidama
JF-Expert Member
- Jun 10, 2022
- 500
- 942
Hawa jamaa bana ni miyeyusho yani sijui hata wanafanya vipi kazi. Ukiangalia kwa sasa kasi ya watu kujenga maeneo ya pembezoni mwa mji imekua kubwa lakini hawa jamaa siwaoni kabisa wakitimiza majukumu yao ya kupima viwanja kwa kasi ili watu wanapojenga, haya maeneo mapya angalau yawe na mpangilio mzuri sio kama mitaa ya zamani (mfano uswahilini).
Sasa hawa mipango miji bana, unaweza jitutumua ukajenga ka nyumba kako taratibu hata kwa miaka miwili huwaoni kuja kukwambia chochote ila ukisha kamilisha ndio wanakuja kukuwekea 'X bomoa'. Hivi mi nijenge nyumba yangu kwa biashara yangu ya miogo kwa kudunduliza kwa miaka hata miwili taratibu halafu nikamilishe we uje tu from nowhere uniambie nibomoe, haiingii akilini.
Sasa cha kushangaza kuna maeneo mengine hata hayapo mbali na mji, yani unakuta hata ni km20 tu kutoka katikati ya mji ila bado hayajapimwa na unakuta ni maeneo ambayo yameanza kuendelea tangu 2015. Sasa hawa jamaa hua wako wapi. Wanafanya vipi kazi!
Huu ujinga ndo hata haya maeneo mapya yataishia kua na mpangilio kama wa Manzese.