Chengdu: Moja ya miji ya kisasa zaidi duniani

Chengdu: Moja ya miji ya kisasa zaidi duniani

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
7,595
Reaction score
15,506
chengdu-xindu-1.jpg
Ukiangalia picha za Chengdu, unaweza kudhani kinachoifanya iwe modern ni skyscrapers na majengo yake marefu pekee. Lakini modernity ya Chengdu iko zaidi kwenye mfumo wa jiji kuliko majengo yenyewe.

Kama kuna vitu wachina hawana mpinzani basi ni kwenye suala la kujenga miji. Mji wa Chengdu ni combination ya vitu vingi sana

1. Urban planning
Chengdu imekuwa na mipango ya muda mrefu ya kupanua na kumodernize jiji. Mfano mkubwa ni Tianfu New Area, eneo jipya lililopangwa likiwa na CBD, makazi, biashara, technology parks, barabara, parks na public facilities.
Imesaidia sana jiji la Chengdu kuwa very organized badala ya kuwa tu majengo yaliyokusanyika bila mpangilio, kama huku kwetu Africa

📷 Chengdu Skyline
chengdu+china.jpg



2. Public transport
Chengdu imewekeza sana kwenye metro na mfumo wa usafiri unaounganisha sehemu mbalimbali za jiji. Metro railway, high-speed rail, airport na highways vinafanya kazi kama network moja.
Kwa nchi kama China modern city siyo tu kuwa na magari mengi mjini, bali kuwa na alternative nzuri za usafiri wa umma.
I wish na sisi tuongeze metro railway ya kisasa Dar es Salaam, pia tuanze mipango ya kuweka BRT system Arusha, Mwanza na Dodoma

📷 Chengdu BRT
Chengdu_Bus_Rapid_Transit.jpg


📷 Chengdu metro
458_reversing_at_Xihe_(20250404125547).jpg



3. Green city
Chengdu imejikita kwenye concept ya “Park City”, yani waliingiza parks, lakes, wetlands na green spaces ndani ya urban development.
Kwa hiyo unaweza kukuta CBD yenye skyscrapers lakini karibu yake kuna parks, water bodies na pedestrian spaces. Lengo ni kufanya jiji liwe modern lakini bado livable.

Miji yetu Tanzania ina uhaba wa parks mingine haina kabisa. Miji kama Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Tanga, Arusha, Dodoma nk inahitaji Green Parks nyingi ili watu wapate mahali pa kupumzika, kuvuta hewa safi karibu na miti na hata mazingira mazuri yanayopendezesha mji

📷 Chengdu Green Parks
What-Makes-Chengdu-a-Top-Investment-Destination-in-Southwest-China.jpg



4. Technology & industries
Chengdu pia ni kituo kikubwa cha technology na high-tech industries. Kuna software, AI, electronics, aerospace, biotechnology, research na digital industries.
Mfano ni Tianfu Software Park na maeneo mengine ya high-tech ambayo yanaunganisha companies, research, innovation na employment.

📷Tianfu Software Park, Chengdu
Chengdu_Tianfu.jpg

Chengdu_Tianfu_Software_Park.jpg



5. Modern infrastructure
Jiji lina modern commercial districts, skyscrapers, shopping complexes, wide roads, bridges, pedestrian areas na smart-city infrastructure.
Kinachovutia zaidi ni kwamba infrastructure za Chengdu zimeunganishwa na residential areas na public transport badala ya kujengwa kama projects zinazojitegemea, kama sisi tunavyojenga stand mbali na makazi ya watu mwisho wa siku zinafeli

📷 Chengdu Infrastructure
5cb1be61-99cf-4b15-be45-a0c2ac7e147a.jpeg
8ad7c896-f432-4eb4-8e58-d41489eebd0a.jpeg



6. Connectivity
Chengdu pia ni major transportation hub ya Western China. Ina airport kubwa, high speed railway, metro na highway networks zinazoiunganisha na miji mingine mikubwa ya China.
Hii ni muhimu kwa sababu modern city inahitaji connectivity, siyo majengo mazuri pekee.

📷 Chengdu Airport
airport1.jpg


Kwa kifupi jiji la Chengdu ni combination ya
  • Urban planning
  • Public transport
  • Green spaces
  • Technology
  • Manufacturing Industry
  • Connectivity
  • Modern infrastructure.
Ndiyo maana Chengdu inasemekana kuwa very modern city

Chengdu haikuwa hivi kwa siku moja. Ni matokeo ya miaka mingi ya planning, investment na deliberate urban development, lakini kwa level iliyofikia tunaweza kusema Chengdu imejengeka kwa kasi kubwa sana ukifananisha na miji mingi duniani

Kama Tanzania ingeamua kudevelop mji mmoja kwa mfumo huu, ni mji gani ungekuwa na potential kubwa zaidi; Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza au Mbeya?
 
Hapo jirani nimepakana na mzee **** Lee tee ana jeuri sema ana watoto wazuri
 
Kwa mazingira hayo. Inabidi tuwe na akili za kichina todauti na hivyo bado sana.
Viaongozi ni tatizo.
Mfumo ni tatizo
Wananchi ni tatizo .

Unategemea nini matokeo yake
 
Hao ndio binadamu wanaoishi sasa
Halafu huwa nikisema hapa Africa kuna vijiji tu vilivyochangamka huwa nashambuliwa balaa na mimi huwa nawaambia ukitaka kujua kama, mama yako anajua kupika au hajui nenda kale na kwa jirani
 
Unaiona dalili ya huyu mama kuachia madaraka 2030 ? Utasikia awamu yake ilianza 2025 ile 2021 watasema haikuwa yake alimalizia ya Magufuri
 
Inaonekana ni mji mzuri wa kitambo uliopangika vizuri tofauti ni kwamba Chengdu ni futuristic city, sidhani kama kuna mji wa Africa wa kuukaribia.
Kwa Africa itachukua muda sana kupata mji kama Chengdu. Continent nzima hatupo serious hata kwenye vitu basic, let alone building futuristic cities
 
Back
Top Bottom