Siasa na Dini katika moja na kuja kwa Maitreya

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
24,504
28,692
Toka wakati ule wanadamu wameanza kusimika tawala zao duniani siasa na dini ilikuwa katika sarafu moja. Mfalme alikuwa ni mkuu wa serikali na kuhani kwa wakati mmoja, ni katika nchi ya Israeli pekee mfalme hakuruhusiwa kuwa kuhani, na kuhani hakuruhusiwa kuwa mfalme. Hizo nyanja mbili zilitofautishwa kabisa lakini katika mataifa mengine hizo nyanja ziliunganishwa.

Na katika hiki kizazi kipya ni taifa la Marekani pekee ndio lilikuja na utaratibu wa kushangaza wa kutenganisha serikali na dini na wakaweka sheria kali za kuzuia dini isiingilie majukumu ya kiserikali na serikali isiingile matakwa ya dini, bali dini ibakie kama jambo binafsi ama haki binafsi ya mtu. Marekani ikawa taifa la kwanza katika kizazi hiki kuwa na utawala wa rais ambaye anaongoza kwa muhura tu tena anayechaguliwa kwa kura tena asiye na mamlaka yote bali sehemu ya mamlaka, na mamlaka zingine wanagawana na bunge na mahakama. Na pia likawa taifa la kwanza katika kizazi chetu kutokuwa na kuhani mkuu ama papa wa kitaifa.

Ukomunisti nao ulijitokea mnamo karne ya 19 nao ukaiita dini kuwa ni bangi na kutaka dini si tu iondolewe katika siasa bali iangamizwe kabisa yaani isiwepo. Lakini ukifuatilia kwa ndani katika serikali zote zilizoundwa kwa falsafa za ukomunisti utaona kuwa Ukomunisti nao ni dini vilevile. Maana wale viongozi katika serikali za kikomunisti wanageuka kuwa miungu ambayo inatawala dhamiri za wananchi. Na katika serikali nyingi za kikomunisti utaona wamejenga sanamu kubwa kubwa za viongozi wao na kuwainamia mfano Korea kaskazini, wanazitolea ibada sanamu za waanzilishi wao. [tazama picha].

1649980378003.png


Na huko China X Jiping ametangazwa kuwa rais wa maisha na huyo ni kama kuhani mkuu wa China. Hata juzi hapa dunia imestajabu kuona kiongozi mkuu wa dini wa Urusi patriaki Kirill akiunga vita vya Urusi na Ukraine, na maskofu wake wakibariki silaha za Urusi ili zikaue wa Ukraine ambao wanaitwa waasi wa mfumo Urusi wa Kiorthodoksi kwa kuunga umagharibi. Hivyo tupo katika vita vya kidini kwa kivuli cha kisiasa. [Kumbuka vita vya msalaba pia + vita vya jihadi].

Hivyo basi mkuu wa serikali ya kikomunisti hana tofauti na papa, maana yeye pia ni raisi wa maisha kama papa alivyo askofu wa maisha. Mkuu wa kikomunisti anatawala nyanja zote za maisha ya taifa, yeye ni mkuu wa nchi, mkuu wa serikali, mkuu wa majeshi na mkuu wa chama, akiteua viongozi wote waandamizi, na papa pia ni mkuu wa Vatican, mkuu wa Kanisa zima na mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Vatican nk na mteuaji wa viongozi wote wa kanisa na vatican. Ukomunisti una aina ya mavazi yao, maisha yao na itikadi zinazofanana, hivyo ni dini kama dini ambayo inakataa ama kupinga au kutozipa dini zingine nafasi kama vile ukatoliki katika zama za kati ulivyozuia kwa kutozipa dini zingine nafasi. Kwahiyo basi si rahisi kwa leo kuchambua siasa na kuiweka dini kando, haya mambo yanahusiana kabisa aidha kwa wazi ama kwa siri. Lakini Kibiblia Yesu alisema ya Kaisari mpeni Kaisari na ya Mungu mpeni Mungu, hakutaka kuunganisha Kaisari (Serikali) na Mungu (Dini) maana ni hatari kuu.

Hata umoja wa mataifa una itikadi ya dini lakini si moja bali mchanganyiko wa dini katika umoja. Na ndio maana katika makao makuu ya UN kuna chumba kidogo cha tafakari (meditation room) ambacho dini zote zinakitumia kufanya ibada, kwahiyo mnaweza kujikuta mpo humo wakristo, wabudha, wahindu, washinto, waislam nk mkitafakari sala kila mtu na imani yake.

Na zaidi katika UN wanadai wa dini zote wameshirikishwa katika umoja huo zikiwemo dini za kishikina na uchawi na ndio maana kuna shirika la linalofanya kazi na UN linaloitwa Lucifer trust, lakini ili kuondoa sintofahamu ya wengi hasa kwa WAkristo ambao kwao Lusifa ni Ibilisi, UN iliomba walegeze jina na likaitwa Lucis trust hadi sasa. Na kuna manabii wa UN kama mchawi Alice Bailey ambaye ndiye muasisi wa shirika la Lucis trust mmoja ambaye ni sehemu ya kuunda mitaala ya elimu duniani, na mwingine ni Helena Blavatsky ambaye alikuwa mchawi wa kutupwa muabudu shetani lakini hoja zake zinakubaliwa na UN.

Helena Blavatsky alifanya kazi ili kujenga msingi wa dhana ya udugu wa ulimwengu wote wa wanadamu ambao hauwezi kutenganishwa na hisia ya heshima kwa kila watu, kila utamaduni, na kila mtu. Hivyo alifanya kazi ya kuunganisha ulimwengu wote wa kichawi katika umoja na kutaka usibuguziwe na imani zingine kama za Kikristo na Kislamu, bali imani zote ziishi pamoja (co exist). Eneo hili umoja wa mataifa umelichukua na kumfanya Helena kama greter thinker na filosofa wa kizazi kipya ambaye anautakia ulimwengu wetu mema.

Wapo mafilosofa wengi katika UN kutoka katika dini mbalimbali kama Ubudha, Uhindu, Katoliki nk na wote wanakubaliana pamoja katika kuujenga ulimwengu mmoja wenye tofauti lakini katika "UMOJA. Naam umoja wa mataifa hautaki kabisa mtu mwenye dini kumhubiri mtu mwingine mwenye dini, unadai kila dini ina wokovu haina haja ya kuamini dini fulani au mtu fulani ili uokoke. Na umoja wa mataifa unamwamini Kristo lakini si Kristo wa Biblia bali Kristo wa ulimwengu (COSIMIC CHRIST) ambaye anajifunua katika dini zote.

Kwa Wakristo kama Yesu, na kwa Wahindu kama Krishna, na kwa Wabudha kama Budha au Maitreya na kwa Waislam kama Issa au imamu Mahid na kwamba atakuja duniani akitimiza nabii zote za kila dini na kuleta zama mpya za dhahabu. Na UN ni nabii wake wa kuunganisha mataifa ama kuyaandaa mataifa kumpokea na kabla hajakuja atahutubia dunia nzima kupitia flat screen, smart phone na sreen zote za miji na mbazo zitakuja kuwekwa katika miji na vijiji ili anapotoa hotuba dunia nzima imsikilize na kumwona. Hivyo hata kama utakuwa umezima sim ama TV yako zitajiwasha zenyewe tu.

Kwahiyo umoja wa mataifa si inshu ya siasa ama uchumi tu bali na "DINI" umoja wa dini ambao ndio kiini kikuu cha umoja huu. Maana ukiroho/ukidini ndio umeshika sehemu kubwa ya mawazo ya mwanadamu na machafuko duniani yanaundwa na fikra za kidini. Hivyo ukishika eneo la dini umeshika dunia, na ndio maana sasa kuna bunge la dini la dunia, kuna umoja wa dini, kuna umoja wa Wakristo (Ukumene) na kinachofuata ni umoja wa dini na serikali na hilo ndio litakuwa goal la umoja wa mataifa na utimizo wa agenda ya miaka mingi.

Kama navyosema daima ni kwamba hii migogoro ya kiulimwengu ambayo wachambuzi wengi wapo kisiasa zaidi basi kiini kikuu cha hii migogoro ni "DINI".....siasa ni kifuniko tu.

Dunia ipo katika vita ya kidini, nyuma ya Putin kuna baba askofu ambaye anachochea vita hivi na kabla ya vita waliziombea na kuzibariki silaha pamoja na jeshi ambalo liliwekwa wakfu ili kupigana vita vitakatifu ili kuirejesha Ukraine iliyo asi katika ushirika wa Patriaki wa Urusi. Kumbuka zama za Hilter, maskofu wa Katoliki walimbariki kijana wao Hilter ili kupigana vita vitakatifu naam kwa madai kuwa anaupigania Ukristo. Hilter alisifiwa sana na viongozi wa dini husika kama sasa Putin anavyosifiwa na mababa wa Orthodoksi, na moja ya kigezo ni kuwa Ukraine iliidhinisha maandamano ya mashoga katika nchi ambayo kanisa la Urusi lilizaliwa, hivyo kipigo ni halali yao.

1649980942264.png
 
Haya tena yametoka wapi tena mbona hakuna reference kwenye points ili kukazia hoja,sijaona kutaja serikali za kiislamu kuna ajenda gani tena hapa

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu umetirirka haraka haraka sanaa! Ni kama ulitaka kuelezea jambo lakini ukajikuta umeongea mambo mengi mpaka hayahusiani!

Vijana wa kirusi wanapokwenda vitani wakiombewa na viongozi wao wa kidini ndio wanakwenda kupigania dini?

Kule kwetu vijana waliopevuka wanapotoka kwa ajili ya kwenda kuiba ng'ombe vijiji vya mbali huombewa na wazee wa kimila/dini na wakirudi salama hutambikiwa na kupoozwa.
 
Back
Top Bottom