Dada yangu, ni vizuri kwa mtu aliyesilimu kuchagua jina la Kiislam kwa ajili ya utambulisho wake lakini pia tumeambiwa tuchague majina mazuri.
Pia kuna wakati mtu atalazimika kubadili jina mfano mtu anayetumia jina katika majina ambayo ni maalum kwa Allah tu. Mfano mtu kuitwa Al-Khaaliq (Muumba) au Ar Razzaq (Mwenye Kuruzuku). Hii haifai.
Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimbadilisha mtu aliyesilimu aliyekuwa akiitwa Abul-Hakam (baba wa Hukumu) akimwambia kuwa Allaah Pekee Ndiye Mwenye sifa hiyo ya Al-Hakam, na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamuuliza kama ana watoto na majina yao, yule mtu akataja wanawe watatu, Shurayh, Muslim na 'Abdullaah. Basi Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: “Kuanzia leo wewe ni Abuu Shurayh.” [Abu Daawuwd].
Ni vyema kuwaita watoto au kuwaita watu (mfano aliyesilimu) kwa majina ya Allah kwa kufuatanisha na neno 'Abd (Mja). Mfano kumuita mtu 'Abdur-Razzaaq (Mja wa Mwenye Kuruzuku) au 'Abdu-Allah (Mja wa Allah).
Inafaa kwa mtu kutumia majina ambayo ni sifa za Allah lakini pia ya WanaAdamu kama vile Maalik (Mfalme).
Haifai pia mtu kujiita au kuitwa 'Abdur-Rasul (Mja wa Mtume) au 'Abdun-Nabbiy (Mja wa Nabii) au 'Abdul-Hussain (Mja wa Hussain), kwa sababu uja ni wa Allah pekee na si wa kiumbe chochote. Majina yenye Shirki hayafai. Hata Swahaba Abu Hurayrah alikuwa akiitwa 'Abdush-Shams (Mja wa Jua) lakini aliposilimu Mtume alimbadilisha jina akamuita 'Abdur-Rahmaan (Mja wa Mwingi wa Rehma)
Mtu Mwenye jina lenye maana mbaya pia halifai. Na Uislam unamruhusu mtu kubadilisha jina lolote lenye maana mbaya hata kama alipewa na wazazi wake.
Mengi katika niliyoandika nimeyatoa Alhidaaya.com.
Soma pia yafuatayo kwa faida zaidi;
Fiqh Ya Kuwaita Majina Watoto
Jamii
Fiqh Ya Majina Ya Watoto
www.alhidaaya.com
Ni Sunnah kutunza jina zuri, na katika majina mazuri ni:
'Abdullaah (Mja wa Allaah Subhanahu wa Ta'aala)
na
'Abdur-Rahmaan (Mja wa Mwingi wa Rahmah);
na majina ya ki kweli hasa ni:
Al- Haarith (Anayezaa)
na
Humaam (Hodari);
na majina mabaya zaidi ni:
Harb (Vita)
na
Murrah (Chungu)
Hadiyth ifuatayo imethibitisha:
((Majina yanayopendezewa kwa Allaah (Subhaana wa Ta'aala) ni 'Abdullaah na Abdur-Rahmaan.)) [imeripotiwa na Muslim.
Kwa Abu Daawuud kuna nyongeza((Na majina ya ki kweli hasa ni Al-Haarith na Humaam, na mabaya zaidi ni Harb na Murrah)).
Na majina mabaya, na yale ambayo yanamaanisha vitu vibaya katika kutokuwepo kwao, ni makuruhu (Yasiyopendeza), kama vile:
Nujayh (fanikiwa),
Barakah (baraka),
Kulayb (kijimbwa),
Harb (vita),
Murrah (chungu),
Shihaab (kimondo),
Himaar (punda),
Aflah (fanikiwa sana),
Yasaar (wepesi),
Rabaah (faida), na
Naafi` (kunufaika)
na majina kama:
Sittun-nisaa (mwanamke wa wanawake wote) ni yanayogombezewa sana.
Na Mfalme wa Wafalme limekatazwa, kama ilivyokuwa:
'Shahenshaah',
na
Aqdhwaal-Qudhwaat (hakimu wa mahakimu).
Na inapendelewa kubadilisha majina mabaya na ambayo yanamaanisha vitu vibaya katika kutokuwepo kwao.
Na inapendelewa kwa mtoto wa kiume, mwanafunzi au mfanyakazi kutomwita kwa jina lake, na kwamba watu wazuri (wanaume na wanawake) wawe wana kun-yah, hata ikiwa hawana watoto wa kiume, na kun-yah huhusiana na mtoto wa kiume wa mwanzo.
Na imekatazwa kuwa na Kun-yah ya 'Abul-Qaasim kwa mtu ambaye jina lake ni Muhammad na vile vile kwa watu wengine, katika kipindi cha Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na vile vile baadae ya hapo.
Tanbihi:
Kuna khitilafu baina ya madhehebu juu katika nukta hii- wengine wameshika kwamba katazo lake (kutumia kun-yah ya Abul-Qaasim) liliwekwa katika kipindi cha uhai wa Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) tu na si baada ya kufariki.
Na aliyeruka mipaka (faasiq) au mzushi asipewe kun-yah mpaka kukiwepo hofu ya fitnah, au ikiwa kwa sababu ya utambulishi, (kama vile Abu Lahab).
Na inapendelewa kwamba mtu asitumie kun-yah yake pekee (yaani bila ya kutimiza jina lake pia), isipokuwa akiwa anajulikana kwa kun-yah yake na sio kwa jina lolote isipokuwa hilo.
Na pia imekatazwa (Haraam) kumtania mtu kwa jina ambalo halipendi. Kama ikiwa anajulikana kwa jina jengine (ambalo halimchukizi) na hata kama jina hilo lina dhamiria kitu ambacho kinamhusu yeye ambacho ni cha kweli.
Kun-yah (Lakabu au Jina la kupachika)
Ushahidi uliombwa wa kuchukuliwa kun-yah kuwa ni Sunnah. Kuna vidokezo mbali mbali juu ya hili katika Hadiyth.
Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa na kun-yah, na hakuna ushahidi wowote wa kuonyesha kwamba kuwa na kun-yah ilikuwa kwa yeye pekee, na hii ndio inayoamua ni Sunnah (kumfuata mtu katika kitu ambacho hakikua kwa ajili yake pekee (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).
Zaidi, kuna Hadiyth iliyoripotiwa na At-Tirmidhiy katika "Ash-Shamaail"
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwita mvulana mdogo kwa kun-yah, kuonyesha kwamba si muhimu kuwa na mtoto kabla ya kutumia kun-yah.
Mazungumzo zaidi ya Hadiyth hizi yanapatikana katika Fat-h al-Baariy (maelezo ya Swahiyh Al-Bukhaariy).