Hivi dini ni imani au ni jina?

eddy brown

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
414
310
Napataga kigugumizi sana nikisikia mtu kabadili dini kisha anabadilisha na jina, eti jina la Kiislam au la Kikristo.

Kwani ukibaki na jina lako na kuendelea na ibada za kumuabudu Mungu kwani haikubaliki? Nimebahatika kwenda Japan, China na Russia. Nimekuta kuna Waislaam wengi na wakristo, ila sijakuta mtu anaitwa Muhammad au William.

Kumjua mtu dini yake hadi umuulize lakini sio kwa jina. Sasa tunaomini hivyo tunakwama wapi?
 
Ni imani.
Jina unaulizwa...
Je...? Unataka kubadili jina
Ndiyo.... Taja jina ulipendalo.
Hapana... unaendelea na Jina lako.
 
Dini Ni jina. Sio kila Mkatoliki ana imani sawa na mwenzake. Imani ni vitendo.

Yakobo : Mlango 2​

13 Maana hukumu haina huruma kwake yeye asiyeona huruma. Huruma hujitukuza juu ya hukumu.Imani bila Matendo Imekufa
 
Dini ni Imani, lakini pia inaweza kuwa a central part ya utambulisho wa mtu.

Utambulisho unahusisha: Jina, mavazi, utamaduni n.k.

Umetoa mfano wa Wachina, Wajapani na Warusi kwamba huwezi kukuta mtu anaitwa Muhammad au William japo baadhi yao wana dini zao za Kiislam na Kikiristo.

Yawezekana ikawa kweli, lakini ukizama sana utakuta hayo majina yao yana vielementi vya Uislam au Ukristo na wenyewe wanajua huyu ni wa imani yangu na yule siyo wa imani yangu.
 
Kuna watu wanatafuta kufanana na waarabu. Ndio hao wanafanya assimilation, tena ukikaa vibaya nadhani wanaweza hata kujichubua na kuweka nywele relaxer ili wafananie na waarabu kabisa.

Na kuna watu wanadeal na imani hawa wanajifunza mafunzo bila kutaka uarabu. Kuna uelewa mdogo sana wa imani Tanzania watu wanafanya ili kuonekana na sio kufuata usafi wa imani husika.

Ndio maana leo usishangae mtu anatumia ile kanuni ya wake wake wanne kufanya umalaya kwa uhalali wa dini ile hali imani yake imeelekeza kwa namna tofauti sana juu ya kuwa na wake wanne.
 
Hata Mungu alibadili majina ya watu alipowakusudia jambo fulani, mfano Abrahamu aliitwa Ibrahimu, Sarai aliitwa Sara na Yakobo aliitwa Israeli.

Japo Mungu alikuwa hamaanishi 'dini' katika tafsiri yetu, lakini ilimpasa kubadili majina, hii ni kwa mujibu wa Biblia.
 
Umeshindwa kumjibu mwenye swali,umekuja na porojo,chuki ila ukweli utabaki palepale
Kuna watu wanatafuta kufanana na waarabu. Ndio hao wanafanya assimilation, tena ukikaa vibaya nadhani wanaweza hata kujichubua na kuweka nywele relaxer ili wafananie na waarabu kabisa.

Na kuna watu wanadeal na imani hawa wanajifunza mafunzo bila kutaka uarabu. Kuna uelewa mdogo sana wa imani Tanzania watu wanafanya ili kuonekana na sio kufuata usafi wa imani husika.

Ndio maana leo usishangae mtu anatumia ile kanuni ya wake wake wanne kufanya umalaya kwa uhalali wa dini ile hali imani yake imeelekeza kwa namna tofauti sana juu ya kuwa na wake wanne.
 
Huku kwetu wanaona zaidi jina ni dini. Mimi jina langu nilikua naambiwa ni la kiislam wakati mimi ni Mkristo.
 
Dini ni imani na imani haiendi Bila vitendo.

Nashangaaa Watu eti wanabadilisha majina wakihama dini. JINA NDO NINI.
kwani mtu ukiitwa Judy huwezi kuwa Muisilamu Hadi uitwe jina jingijne.

Watu wa Dini sijui kwanini huwa wanakomalia Watu wabadili majina.

DINI SIO JINA NI IMANI NA MATENDO.
 
Back
Top Bottom